Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Hata Pepo Yao ni lugha ya kiarabu
 
Papa MUAFRIKA? 🤣🤣🤣🤣
Yes, hilo lazima litokee maana katika Miongo michache ijayo kutakuwa na Waafrika Wakatoliki wengi kuliko Wazungu na Waasia; epicenter ya Kanisa inakuwa kwetu
 
Tofauti kubwa ya Ukristo na Uislamu ni hii hapa; huwezi kuutenganisha uislamu na uarabu wakati unaweza kuutenganisha Ukristo na Wazungu; tutapata Papa Mwafrika kabla hatujapata Mufti Mzungu
Kwani Mufti wa Tanzania sio Mwafrika mkuu?
 
Haijalishi ukristo umeanza na nani bali nani aliuchukua na akaamua kuuleta kwetu huku Sub-sahara
 
Iko sahihi sana, na hapa ndio watu Huwa wanashindwa kuelewa tofauti ya Uislam na Ukristo.

Kwamba wakati Uislam ni dini yenye basis ya Mila na desturi, Ukristo ni dini iliyobase katika Imani kwa njia ya YESU Kristo.
 
Haijalishi ukristo umeanza na nani bali nani aliuchukua na akaamua kuuleta kwetu huku Sub-sahara
Huyo alouleta huku sub Saharan Africa ana ufahamu mkubwa wa dini hiyo kuliko Waebrania na Waaramic waliokuwa na Yesu alipokuwa duniani?
 

Attachments

  • Screenshot_20241114-114122.jpg
    302 KB · Views: 8
Usimtukane mjibu tu kama ulivyomjibu kwenye maelezo yako ya juu
 
Huyo alouleta huku sub Saharan Africa ana ufahamu mkubwa wa dini hiyo kuliko Waebrania na Waaramic waliokuwa na Yesu alipokuwa duniani?
Ndugu yangu, tumeletewa sisi "King James version/edition" ya Biblia na sio ile ya Waebrania au hao Waaramic
 
Sasa wao kufuata hizo tamaduni za kiarabu kwako imekuathiri nn kwenye maisha yako?
Kinacho shangaza ni ww kujiona una uhuru wa kufuata tamaduni za kimagharibi ila wakati huo unaona wengine hawana haki ya kufuata tamaduni unazo ziita za kiarabu.
 
Wewe siyo mstaarabu?
 
Uislam ni dini ilikuwapo tangu enzi za adam (a.s), haikuanzishwa na arabs.

Ktk uislam hakuna mizik wala nyimbo za ibada.

Mavaz tunayovaa ni kwa sababu mtume katuamrisha tuyavae, na sio kwa sababu ya auarabu wake.

Hiyo quran hata waarabu wanafundishwa kuisoma, lugha yake inahitaji utaalamu iliuisome vizuri.

Kiufupi waislamu hatuwafuati waarabu na tamadun zao kwa sababu hata hao arabs wanatamadun za kijinga sana.

Uislam unafuata maamrisho ya Allah na mtume..!
 

Asante sana kwa kutaja hilo vizuri sana. Ni kweli Yesu alikuwa myahudi lkn alikataliwa na mayahudi. Mpaka viongozi wa dini ya mayahudi yalipanga njama ya kumuua. Hilo linadhihirisha nini? Linadhihirisha kwamba mafundisho ya Yesu yalikuwa yakiyakinza mafundisho ya uongo ya mayahudi. Kulikuwa na mayahudi yaliyoitwa mafarisayo na masadukayo. Mayahudi hawa walikuwa wakifundisha uongo na kuwabebesha watu mizigo ya kiimani kulingana na mtazamo na desturi zao. Sasa ujio wa Yesu ulikuja kuyapindua mafundisho hayo. Na ndipo ugomvi ulipoanzia.

Hata mimi binafsi najiuliza, hivi baadhi ya wakristo wanaowaabudu mayahudi wanaelewa kweli kwamba ukristo haufungamani na uyahudi? Kwamba mayahudi hawaamini kwamba Kristo ndiye yule aliyezaliwa miongoni mwao? Kwamba wanaamini atakuja, lkn siyo yule aliyeuawa na wenyewe?


Pia umesema ni mjinga tu ndiye ambaye anafungamanisha uislam na uarabu. Kimsingi binafsi nina maoni tofauti. Ingekuwa uislam haujafungwa kwenye uarabu ningekuelewa. Sasa uislam uko ndani kabisa ya uarabu. Na ndiyo maana huwezi kubobea kwenye dini ya kiislamu bila kuwa mjuvi wa lugha ya kiarabu. Huo ni mfano mmoja wapo ulio wazi kabisa. Na hata katika zile swala zenu tano, hakuna la maana mnalotamka zaidi ya kutaja maneno yale yale katika lugha ya kiarabu. Ambayo wengi wa watu hawayajui. Wamekariri. Kifupi niseme tu uislam kuingia nje ya ulimwengu wa kiarabu umepotea njia, na unaleta shida. Bora unge baki katika ulimwengu huo, kama wenzao wa Buddha, Hindu 🕉, Shinto nk ambao wako katika maeneo yao ya asili.
 

Mnajenga hoja nzuri sana kuhusu uwepo wa uislam kabla ya Muhammad. Lakini hamtoi tangible authority kuhusu madai mnayoleta mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…