Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Wengi hawafahamu ya kuwa uislam ni chombo au mpango wa waarabu kueneza tamaduni, mila na desturi zao. Nachelea kusema hivyo kwa sababu wenyewe waislam wanasema uislam is a total way of life.

Kwa maana nyingine ni utamaduni jumla wa maisha ya watu. Mambo yafuatayo ndiyo yanayonifanya niamini kwamba uislam ni mpango wa waarabu ku assimilate watu wengine wafuate mila za kiarabu.

1. Lugha inayotumika kufanya ibada yao ni kiarabu.

2. Muanzilishi wa dini yao alikuwa muarabu

3. Kitabu chao kimeandikwa kwa lugha ya kiarabu

4. Majina ya waumini wao ni ya kiarabu

5. MAvazi ya waumini wao ni ya tamaduni za kiarabu

6. Majengo yao ya ibada yana mtindo au architectural design ya uarabuni

7. Ala za muziki zinazotumika katika nyimbo za ibada zao ni za asili ya kiarabu

8. Vyakula au mapishi (cuisine) ni ya kiarabu

9. Namna ya kucheza muziki wa sherehe zao ni za kiarabu.

10. Mirathi, ndoa na maziko ni desturi za kiarabu
Kuna mambo mengi ambayo ukiyachunguza yanaenda zaidi ya imani. Yana taka yawe katika ujumla wote wa maisha ya Mtanzania.

Changamoto ni kwamba, kwenye secular state ni ngumu sana kutekeleza desturi hizo, kwa maana serikali yetu haifungamani na dini yoyote.
Karibuni wadau katika kujadili hili mkiwa na akili huru.

CC: Bwana Utam kahtaan FaizaFoxy Kosugi
Uzuri wa haya mambo hakuna wa kulazimisha wewe tu mwenyewe ukiamia unayafuata na kama hutaki unaachana nayo
 
Dini zote duniani zina basis ya mila na tamaduni fulani

Kama waislam watakavyo kataa dini yao kuwa na basis za mila na tamaduni za kiarabu basi hata wewe pia utakataa dini ya ya Ukristo kuwa na basis ya mila na damaduni za Warumi kwa kiasi kikubwa

Mimi sibishi kuhusu mila na desturi za wengine kuhusu dini. Shida yangu ni; uislam umekuwa mtumwa wa uarabu. Huwezi ku practice uislam bila kuwa endeleza uarabu.

Mfano mdogo tu. Hata wakisalimiana watatumia kiarabu, swala 5 watatamka maneno yale kwa lugha ya kiarabu. Sasa hapo utofauti wanaousema kati ya vitu hivyo viwili.
 
1 unaelewa maana ya ibada kwanza kijana 2 muanzilishi yupi wa uislam alikua muarabu kama unamaanisha s a w basi unakosea sababu uislam haukuanzia kwake 3 qur an kweli imeandikwa kwa kiarabu ila uislamu haukuanzia kwenye qur an vilipita vitabu vingi kabla ya qur an 4 uislam hauna majina maalum kijana la msingi Jina liwe zuri hata happy unaweza ukajiita uislam sio Jina kijana 5 waarabu hakua na utamaduni wa kuvaa kwakujistiri kabla ya ujio wa qur an walikua wanavaa vaa tu hovyo hovyo 6 Majengo ndio nini kijana uislam hauna hizo mambo ndio maana watu wanasali popote pale muhimu pawe Safi tu 7 uislam hauna ibada ya musiki wala nyimbo kijana 8 uislam hauna mapishi ya kiarabu kijana uislamu una ruhusu kula chochote maadam ni halali na kizuri 9 Muziki sio sehemu ya sherehe za waislam kijana acha kupotosha watu 10 kabla ya uislam waarabu walikua hawazikani walikua wanafukiana tuuu mwisho waarabu wasiokua waislam nao tunawaeka upande gani wenyewe
Uislamu umeletwa na Muhamad. Hilo hatuhitaji kuwa laghai watu. Miaka hii wameelimika wanaifaham Quran tofauti na zamani.
 
Uzuri wa haya mambo hakuna wa kulazimisha wewe tu mwenyewe ukiamia unayafuata na kama hutaki unaachana nayo

Uko sahihi. Lkn ukipata fursa ya kutoa mawazo yako m'badala kwa wengine jaribu kufanya hivyo kwa njia inayoeleweka.

Mfano mwingine ambao napenda juutoa kwa watu, wanasiasa ni kuwa, CCM chama dola ni ngumu sana kuitenganishq na serikali. Hivi kwamba watu wa kawaida wakiona chama kinagombea dola na CCM ktk uchaguzi kinaonekana kama vile kinataka kuipindua serikali. Kwa sababu kwao wanaona CCM ni serikali. Kwa hiyo jambo la msingi ni kutoa elimu kwamba CCM siyo serikali ni chama cha siasa kama vingine. Licha ya kuwa CCM inatembelea nyota ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Hivyo wengi hupata shida kujua kwamba ni chama kilichotokana na muunganiko TANU na ASP. Lakini siyo zao la muunganiko wa serikali zilizokuwepo.

Na waislam wanapaswa kuelimishwa hayo pia.
 
Yesu alikuwa Myahudi lakini ameeneza ukristo japo wafuasi wake wamekuwa wakijipendekeza kwa Wayahudi.
 
Dini yetu haiend hivo mkuu..!

Labda sijakuelewa, inanmaana ukitaka kuongea na muumini mwenzako kumshauri kwamba (mf) aache zinaa si unamtqzamisha aya katika kuruwani? Au ukitaka kuwaasa watoto waiting wazazi si kuna aya utawasomea?
Sijui ulimaanisha nini!!!
 
Sasa wewe hufikiri kwa nini iwe kiarabu na isiwe kihindi au kichina
iyo itakuwa
Sasa wewe hufikiri kwa nini iwe kiarabu na isiwe kihindi au kichina
kumbe unachukia kiarabu kutumika.wewe ulitaka iwe lugha gani?sikuzote lugha moja unganisha jamii ya watu ndio maana mugu akatuambia sisi waislam kwamba ameitelemsha qurani kwa lugha ya kiarabu iliwenyepesi kwetu kutumika
 
Yesu alikuwa Myahudi lakini ameeneza ukristo japo wafuasi wake wamekuwa wakijipendekeza kwa Wayahudi.

Baadhi ya wakristo hawajui aya zinasemaje. Pia hawajui kuwa wayahudi hawaamini katika Yesu ambaye walimuua. Wenyewe wanamuita mtoto wq fundi seremala. Kuna Yesu wao ambaye ndiyo wanayemtarajia.
 
Iko sahihi sana, na hapa ndio watu Huwa wanashindwa kuelewa tofauti ya Uislam na Ukristo.

Kwamba wakati Uislam ni dini yenye basis ya Mila na desturi, Ukristo ni dini iliyobase katika Imani kwa njia ya YESU Kristo.
Mila na desturi ni nini na ukristo maana yake nini
 
Kwa hiyo linguistic environment ya watu wote duniani iko sawa?

Moja ya sababu inayofanya elimu iwe dhaifu Tanzania 🇹🇿 ni lugha ya kufundishia. Ni kwamba mtoto anafundishwa kwa lugha ambayo siyo mama. Hivyo haelewi kikamilifu. Maana akiwa darasani anafundishwa kiingereza, akitoka nje anaongea katika lugha ya mama. Hivyo linguistic environment is not supporting the learning process.
Hilo likoje katika uislam nje ya ulimwengu wa kiarabu? Wote wanaelewa sawa?
Mnataka kutumia kiswahili kufundishia physics? Mwambie mtoto afafanue quantum mechanics au theory of general relativity kwa kiswahili kama hamalizi ufafanuzi akiwa na kifafa
 
iyo itakuwa

kumbe unachukia kiarabu kutumika.wewe ulitaka iwe lugha gani?sikuzote lugha moja unganisha jamii ya watu ndio maana mugu akatuambia sisi waislam kwamba ameitelemsha qurani kwa lugha ya kiarabu iliwenyepesi kwetu kutumika

Sichukii kiarabu. Ila nashangaa jjnsi idadi kubwa hivyo ya watu duniani walivyonaswa kwenye mtego huo.

Pia nioneshe kifungu ndani ya kuruwan kinachosema msahafu umetelemshwa kwa lugha ya kiarabu ili iwe rahisi kuielewa.
Hata hujiulizi hadhira iliyokuwa inapelekewa kuruwan ilikuwa ni jamii ya lugha gani?
 
Naheshimu maoni yako. Lakini kuwa na fikira tunduizi siyo dhambi. Na labda ukadhani wewe usiyehoji mambo na kutafakari mambo ni mtakatifu. Haiwezi kuwa hivyo.
Pia jua ya kuwa, magharibi hakuna dini iliyoanzia huko. Dini hizi mbili za ukristo na uislam chanzo ni mashariki ya kati au Asia 🌏 ndogo.

Mwisho muache kusalimiana asalam aleykum, pia muache kutaja yale maneno ya swala tano kwa kiarabu (bali yatamkeni kwa lugha yenu ya eneo husika duniani kote) ili tujue uarabu si kitu katika uislam.
Huko kuhoji kwanini usikuhoji kwenye dini yako iliyo jaa makado kado kibao ila uwashwe washwe na kuhoji dini zingine zisizo kuhusu.
Kama ww unataka waisilam waache kutumia kiarabu basi na nyinyi acheni kutumia biblia iliyo buniwa na paulo badala yake mtengeneze ya kwenu waswahili.

Ebu nitajie dhehebu lolote la kikiristo ambalo waasisi wao hawakokea Ulaya?
 
Mnataka kutumia kiswahili kufundishia physics? Mwambie mtoto afafanue quantum mechanics au theory of general relativity kwa kiswahili kama hamalizi ufafanuzi akiwa na kifafa

Ila kuishi Afrika ni mzigo wa kuni. Sasa wewe kwa uelewa wako unafikiri physics inayofundishwa Urusi, China, ujerumani, Korea, Iran nk ni ya kiingereza?
Kwa nini isiwezekane kuwa na quantum physics kwa kiswahili?
 
Huko kuhoji kwanini usikuhoji kwenye dini yako iliyo jaa makado kado kibao ila uwashwe washwe na kuhoji dini zingine zisizo kuhusu.
Kama ww unataka waisilam waache kutumia kiarabu basi na nyinyi acheni kutumia biblia iliyo buniwa na paulo badala yake mtengeneze ya kwenu waswahili.

Ebu nitajie dhehebu lolote la kikiristo ambalo waasisi wao hawakokea Ulaya?

Endelea kujisomesha ili upate maarifa ya kujenga hoja kwenye mijadala mizito kama hii.
 
Lusekelo alisema kuzika kwenye masanduku ni utamaduni wa wazungu. Sio dini ya ukristo. Niambie leo hii ni mwafrika gani mswahili anazikwa bila sanduku? Maamuzi yote ya dini ya kikristo hasa ukatoliki unatoka vatcan kwa mzungu. Mzungu wa vatcan ndio anaamua wewe mzaramo wa msanga uzikwe vipi au usizikwe sasa hapo unasemaje? Bikira Maria, Brian Deacon(yesu) wakuchongwa waliojaa makanisani mwenu wote wana rangi nyeupe(wazungu) kama nyie wanaume chongeni weusi kama papa hajawafuta kwenye dhehebu
Papa kutufuta kwenye dhehebu? Narudia tena nilichoandika awali; Ukatoliki unatokomea bara la Amerika na unatokomea ulaya; the last stronghold ya Ukatoliki ni Afrika na bara la Asia A.K.A bila sisi hawana chao ndani ya miongo miwili mitatu
Na ndio maana nimeandika kwa confidence yote kwamba tutapata Papa Mwafrika kabla ndugu zetu Waislamu hawajapata kiongozi wa Kiroho ambaye sio mwarabu; in fact Nina confidence kubwa kwamba kanisa Katoliki halijahalalisha ushoga kwasababu linaelewa kufanya hivyo ni guarantee ya mpasuko na kanisa Katoliki la Africa
 
Ila kuishi Afrika ni mzigo wa kuni. Sasa wewe kwa uelewa wako unafikiri physics inayofundishwa Urusi, China, ujerumani, Korea, Iran nk ni ya kiingereza?
Kwa nini isiwezekane kuwa na quantum physics kwa kiswahili?
Kwasababu tumekwisha chelewa!
Tukubali tukatae dunia inaenda kuwa na lingua franca moja au mbili ; badala ya kupoteza muda kukaririsha watu misamiati mipya ambayo ni technical kwanini tusifanye kama wahindi ambao wanatumia kihindi panapohitajika na kiingereza kwenye masuala technical
 
Asante sana kwa kutaja hilo vizuri sana. Ni kweli Yesu alikuwa myahudi lkn alikataliwa na mayahudi. Mpaka viongozi wa dini ya mayahudi yalipanga njama ya kumuua. Hilo linadhihirisha nini? Linadhihirisha kwamba mafundisho ya Yesu yalikuwa yakiyakinza mafundisho ya uongo ya mayahudi. Kulikuwa na mayahudi yaliyoitwa mafarisayo na masadukayo. Mayahudi hawa walikuwa wakifundisha uongo na kuwabebesha watu mizigo ya kiimani kulingana na mtazamo na desturi zao. Sasa ujio wa Yesu ulikuja kuyapindua mafundisho hayo. Na ndipo ugomvi ulipoanzia.

Hata mimi binafsi najiuliza, hivi baadhi ya wakristo wanaowaabudu mayahudi wanaelewa kweli kwamba ukristo haufungamani na uyahudi? Kwamba mayahudi hawaamini kwamba Kristo ndiye yule aliyezaliwa miongoni mwao? Kwamba wanaamini atakuja, lkn siyo yule aliyeuawa na wenyewe?


Pia umesema ni mjinga tu ndiye ambaye anafungamanisha uislam na uarabu. Kimsingi binafsi nina maoni tofauti. Ingekuwa uislam haujafungwa kwenye uarabu ningekuelewa. Sasa uislam uko ndani kabisa ya uarabu. Na ndiyo maana huwezi kubobea kwenye dini ya kiislamu bila kuwa mjuvi wa lugha ya kiarabu. Huo ni mfano mmoja wapo ulio wazi kabisa. Na hata katika zile swala zenu tano, hakuna la maana mnalotamka zaidi ya kutaja maneno yale yale katika lugha ya kiarabu. Ambayo wengi wa watu hawayajui. Wamekariri. Kifupi niseme tu uislam kuingia nje ya ulimwengu wa kiarabu umepotea njia, na unaleta shida. Bora unge baki katika ulimwengu huo, kama wenzao wa Buddha, Hindu 🕉, Shinto nk ambao wako katika maeneo yao ya asili.
Wewe jamaa nimegundua kama huna hoja ama hujui unacho kisema huko juu unakubali kisa Jesu kapingwa na wayahudi ndio uyahudi unakua sio dini ila huku kwa s a w hujui ama hutaki kujua ama kuelewa kwamba hata s a w alipingwa na kupigwa vita na wenye dini zao ambao hawakuwa waislam wakiwemo maquraysh na waarabu wengine hili hulijui ume wasifia Mabudha nk unadhani kama wewe utataka kufata dini ya kibudha ukasoma kibudha mienendo yake utakua umefata Mabudha au imekuaje jamaa huna hoja hata s a w alipingwa na waarabu wakati anahubiria uislam mpaka wakawa wanamkashifu kwakumwita yatima na majina mengine ya hovyo hovyo
 
Back
Top Bottom