Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Huwezi kutenganisha Uislam na Uarabu wakati uislam Mwanzilishi na Muenezaji wa dini hiyo alikuwa Mwarabu

Papa kutufuta kwenye dhehebu? Narudia tena nilichoandika awali; Ukatoliki unatokomea bara la Amerika na unatokomea ulaya; the last stronghold ya Ukatoliki ni Afrika na bara la Asia A.K.A bila sisi hawana chao ndani ya miongo miwili mitatu
Na ndio maana nimeandika kwa confidence yote kwamba tutapata Papa Mwafrika kabla ndugu zetu Waislamu hawajapata kiongozi wa Kiroho ambaye sio mwarabu; in fact Nina confidence kubwa kwamba kanisa Katoliki halijahalalisha ushoga kwasababu linaelewa kufanya hivyo ni guarantee ya mpasuko na kanisa Katoliki la Africa
Wewe bado ni mtumwa wa fikra
 
Ndugu yangu, Wakoloni na Wamisionari walikuja kwenye hili bara na wakalikuta katika mifumo ya kijamii lipo nyuma kwa makarne na makarne; hawakukuta mifumo imara ya kuabudu bali kulikuwa na imani za kimakabila (mamia kama sio maelfu ya makabila ambayo hayajaungana)
Suala langu sio kwamba sijivunii uafrika wangu bali naangalia tu uhalisia wa hali ya sasa na uhalisia kwa kipindi hicho
Wewe umejuaje kuwa mifumo ya jamii zetu za kuabudu haikua imara?!,kilichotokea kwa waafrika ni kuwa tumeacha mila na tamaduni zetu tukafuata za watu,mtu anajiua historia ya uzao wa Ibrahim au Joseph kuliko ya mababu zake halafu anajiona yupo sawa kichwani,kama mleta mada alivyosema uislam ni mila za kiarabu kutokana na sababu alizoziorodhesha hapo juu na basi na dini ya ukristo sio imani za waafrika,waafrika tuna imani zetu kutokana na jamiii/kabila husika
 
Ww mbona haujibu hoja na maswali unayo ulizwa badala yake unakimbilia kumshambulia mleta hoja na kumwambia aende akasome sijui hana elimu?
Ili mjadala uwe na hoja zenye mantiki ni lazima muanzisha mjadala awe na elimu ya kutosha kuhusu kitu alicho kileta kijadiliwe ,sasa ww umeanzisha mjadala wa kitu usicho kuwa na elimu nacho na ndio maana ukibanwa na hoja unakimbilia kususa na kutafuta makosa ya kimaandishi kwa aliye leta hoja ili upate pakukimbilia.

Kiufupi hii mada hukuianzisha kwa ajili ya majadiliano na kutaka kuelimika kuhusu uislam bali ulikuwa umeianzisha kwa misingi ya kejeli ili watu waje humu na kuudhihaki uislam sema lengo lako limefeli maana hata wagaratia wenzio wamekupuuza.

Unapojadili hoja jaribu kutofautisha kati ya hisia na uhalisia. Nimeuliza maswali mengi lkn hakuna hoja hata moja mliyoijibu. Badala yake mnanishukia mtoa hoja. Jibuni zile hoja 9 kwa kutumia authority husika. Usilete brah brah. I'm a scientific minded person. Nataka hoja kwa hoja
 
Lugha iliyotumika katika Qur-an ni Kiarabu sanifu kama tu navyoj ifu nza katika Qur-an yenyewe:

"Na namna hii tumekufunulia Qur-an kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembezoni mwake. Na uwaonye siku ya mkutano, siku isiyo na shaka. Kundi moja litakuwa Peponi na kundi jingine Motoni " (42:7)


Kwa nini Qur-an Imeshushwa kwa Lugha ya Kiarabu?
Walimwengu walio wengi wakiwemo baadhi ya Waislamu wanaitakidi kuwa lugha ya Kiislamu ni Kiarabu na Uislamu ni dini ya Waarabu. Bila shaka mawazo haya yamejitokeza kutokana na kutoujua Uislamu kwa upeo wake. Uislamu ni Dini ya Walimwengu wote wa nyakati zote na ni Dini iliyofundishwa na Mitume wote. Je, Mitume wote walikuwa Waarabu au watu wote waliolinganiwa na Mitume hao na kuwafuata walikuwa Waarabu? Bila shaka jibu litakuwa "hapana". Bali tunajifunza katika Qur-an yenyewe kuwa Allah (s.w) amewajaalia walimwengu kuzungumza lugha mbali mbali na ni katika ishara ya Uungu wake na utukufu wake.

"Na katika Ishara zake (zinazoonyesha uwezo wake) ni kuumba mbingu na ardhi, na kuhitilafiana lugha zetu na rangi zenu. Kwa yakini katika haya zimo ishara kwa wenye ujuzi." (3 0:22)

Kwa nini Qur-an imeshushwa kwa lugha ya Kiarabu? Jibu lake linapatikana ndani ya Qur-an yenyewe:

"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia. Kisha, Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye (kwa kuwa hataki kufuata ujumbe uliomfikia wazi wazi) na humuongoza amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Hekima." (14:4)


Aya hii inatufahamisha kuwa kila Mtume alishushiwa Wahyi kwa lugha ya watu wake ili yeye mwenyewe apate kuwabainishia vizuri na wao wapate kumuelewa vizuri. Kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu wa kabila la Kiquraishi na kwa kuwa Maquraish na Waarabu kwa ujumla ndio watu wake wa mwanzo kuwalingania Uislamu ili wamsaidie kuufikisha ulimwengu mzima. Qur-an ilibidi ishushwe kwa lugha ya Kiarabu cha Kiquraish kilichokuwa fasaha kuliko vilugha vyote vya Kiarabu. Watu wake wasingemuelewa kabisa kama Mtume (s.a.w) angewalignania kwa lugha isiyokuwa ya Kiarabu:

"Na lau kama tungaliifanya Qur-an lugha isiyo ya Kiarabu wangelisema: Kwa nini aya zake hazikupambanuliwa? Lo! Lugha isiyokuwa ya Kiarabu na (Mtume) Mwarabu! (Mambo gani hayo)? " (41:44).

"Na lau tungaliiteremsha juu ya mmoja wa wasiokuwa Waarabu, na akawasomea (kwa ufasaha) wasingalikuwa wenye kuamini." (26:198-199)

Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:
(i)Ni desturi ya Allah (s.w) kumtuma mjumbe wake kwa lugha ya watu wake anaowafikishia.
(ii)Qur-an imeteremshwa kwa lugha ya Kiarabu kwa kuwa Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa Mwarabu na wale aliowalingania mara ya kwanza walikuwa ni Waarabu.
(iii)Waarabu wa mwanzo kulinganiwa Uislamu na Mtume (s.a.w) wasingeliukubali ujumbe kama Mtume asingelikuwa Mwarabu na kama angelingania kwa lugha nyingine isiyokuwa ya Kiarabu.
(iv)Kama Mtume (s.a.w) angelingania kwa lugha nyingine isiyokuwa Kiarabu, ujumbe wake usingelifahamika na watu wake wasingelazimika kuufuata kwa kuwa hawauelewi.
"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia. Kisha, Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye (kwa kuwa hataki kufuata ujumbe uliomfikia wazi wazi) na humuongoza amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Hekima." (14:4)"

👆👆Ok wewe muafrika ukasahaulika kushushiwa mtume wa kabila lako,,wewe huko nalinjilingi ukaona zile zile ibada za wazee wako hazifai ila hizi za kiarabu ndio sahihi kwako kuzifuata
 
Mtu kama FaizaFoxy ni mwenyeji wa pwani mkuranga huko lakini anajinasibisha na uarabu,mtu kama huyo ukimwambia dini ya kiislamu ni mila za waarabu anakubishia,kisa kwenye quruan kuna maandiko yamewaambia haya maneno yameshuka kutoka juu kwa mwenyezi Mungu

Hawajui ya kuwa wanatumika na uislam kuendeleza tamaduni, mila na desturi za kiarabu. Mudi kawakataza kutumia lugha na majina yao ya asili isipokuwa kiarabu, halafu bado wanasema kuna utofauti.
 
Mtakuja na kila hoja ya kupinga na kuutetea uislam,lakin utabaki kuwa uislam ni mila za kiarabu,ni mtu mjinga pekee asietumia akili yake ndio ataamini uislamu si uarabu

Bro umemaliza. Wee watu gani hata wakionana wanaanza kusalimiana asalam aleykum. Utafikiri wako Oman 🇴🇲 kumbe ni kina FaizaFoxy wa kimanzi chana

😛
 
uwe una swali kwa kutumia lugha ya mila yako basi kama quruan si kiarabu,na Mkiwa mnafunga zile ndoa zenu muache kufunga misuli na kuweka majambia huko viunoni na muache kupika mabirani na kuweka kaswida, sababu hivyo vyote ni tamaduni za waarabu

Bro umemaliza kila kitu. Watabisha sana. Lakini ukweli wanaujua.
 
"Na hatukumpeleka Mtume yeyote isipokuwa kwa lugha ya watu wake ili apate kuwabainishia. Kisha, Mwenyezi Mungu anamuacha kupotea amtakaye (kwa kuwa hataki kufuata ujumbe uliomfikia wazi wazi) na humuongoza amtakaye. Naye ni Mwenye nguvu na Mwenye Hekima." (14:4)"

👆👆Ok wewe muafrika ukasahaulika kushushiwa mtume wa kabila lako,,wewe huko nalinjilingi ukaona zile zile ibada za wazee wako hazifai ila hizi za kiarabu ndio sahihi kwako kuzifuata

Bro wewe kweli ni muislam halisi kiufahamu, sina uhakika kiimani. Maana unaleta aya iliyonyooka kuleta ushahidi.
Kina Bwana Utam FaizaFoxy Kosugi wanaongea ongea tu bila authority.
 
Uislam upi na wakati mnasema kuruwan ilishushwa wakati wake
Yaan wanajichanganya hao,kutetea imani ambayo sio yako kazi sana,halafu mbaya zaidi ndani ya hivyo vitabu wamekatazwa matumizi ya akili,yaan wewe hutakiwi kuhoji kila utakachokisoma huko kubaliana nacho,ndio maana unaweza kuona mtu ana uelewa mpana wa mambo ya ulimwengu lakin anaposoma hicho kitabu akili zake anaziweka pembeni kwasababu akihoji tuu amemkufuru allah
 
Mfumo wa uongozi mmoja ulikwisha zamani sana kiongozi wa mwisho alkuwa Alli bin Abitwalib....kwahiyo uislam ni tofauti na ukiristo

Sema ni tofauti na Roman Catholic wenyewe ndiyo bado wako authoritative.
 
kuna siku shehe mmoja hv ana asili ya kiarabu alikuwa kwenye kipindi cha televisheni cha hapa bongo

watu wakawa wanauliza maswali mbalimbali kuhusiana na imani yao

mmoja wa watazamaji alitaka kujua namna ya kusali sala fulani hivi

jamaa akamjibu namna ya kusali lakini akasisitiza ili Allah amsikie inambidi asali hiyo sala kwa kiarabu
🤣🤣🤣

Hapo ndipo tatizo linapoanzia. Usipojua kiarabu huna chako katika pepo ya kiislam.
 
Yaani wewe ni kizazi mbatata,kinachosababisha uislam uwe uarabu si lugha au?

Huyu Bwana Utam hajui tamaduni, mila na desturi za jamii yoyote ile hutambulishwa kwanza kabisa na lugha. Halafu mambo mengine yanafuatia. Sasa nyie 99% ya ibada yenu inasadifiwa na lugha ya kiarabu. Halafu unakaza fuvu eti uislam haujafungwa ndani ya uarabu.
 
Wewe siyo mstaarabu?
Leo hoja imekuzidi 😂 umeshindwa kuwatetea ndugu zako katika imani,Ni suala la muda tuu ila uwongo wa hizi imani mbili zitajulikana kwa waafrika,watu watataka kujua ilikuaje zikafika Africa,muda walitumia hawa wakoloni kueneza propaganda zao ndio muda huo huo Afrika itatumia kurudi kwenye asili yake
Wewe siyo mstaarabu?
 

Attachments

  • FB_IMG_1731619891334.jpg
    FB_IMG_1731619891334.jpg
    57.1 KB · Views: 3
Mtakuja na kila hoja ya kupinga na kuutetea uislam,lakin ukweli utabaki kuwa uislam ni mila za kiarabu,ni mtu mjinga pekee asietumia akili yake ndio ataamini uislamu si uarabu
Sio kweli unajua kama waarabu walimpinga mtume s a w wakati anawahubiria qur an na uislam mpaka wakawa wanampa kejeli na kumwambia kama qur an uzushi kutunga nk au hujasoma hili
 
Back
Top Bottom