Sielewi msukumo uliokufanya kuleta mada kama hii hapa wakati huu; wakati tukiwa na janga kubwa kabisa linalotuzonga.
Hii ni mada nzito sana ambayo ni wazi uzito wake huna uwezo nayo. Nayasema haya kutokana na hayo machache uliyoweka hapo.
"Class Consciousness"? Unataka tuwe na hizo class consciousness waTanzania ili zitusaidie kitu gani; hasa ukichanganya na haya tuliyo nayo sasa!
Haya matabaka, wewe huyaoni ndiyo anayopigania Samia, au mpaka yaweje ndiyo uyatambue?
Kwa taarifa yako kama ulikuwa hujui: hayo matelevisheni yooote uliyoyataja hapo ni vyombo vya propaganda. Sisemi TBC inanafuu zaidi ya hao' TBC na wenzake wote hata hawajui kazi wanayoifanya.
Unachoshindwa kuelewa wewe ni kuwa hizo "Class Consciousness" ndani ya jamii hazijengwi kwenye matelevisheni, ni mchakato unaoanzia mwanzo kabisa wa uhai wa raia ndani ya jamii husika.
Kinachotafutwa, na pengine nawe ndicho ulicholenga ni kumfanya mhusika/mlengwa awe ameandaliwa kuwa na ufahamu wa kutambua anacholishwa na hayo matelevisheni; ili ajijengee uamzi wake juu ya hicho anacholishwa.
Nirudie tena. Sijui ni nini hasa kimekupa msukumo wa kuleta mada kama hii hapa leo.
Ni mada muhimu sana na ni ngumu, hasa kwa uelewa tulionao sasa hivi miongoni mwa jamii yetu
Sitegemei kamwe kwamba lengo la CHADEMA litakuwa ni kujenga hizo unazoziita wewe "Class Consciousness". That will be a terrible thing to do for that party.
N.B.: Nilitaka kudai unipe mrejesho wa hoja yangu, lakini naogopa nitakachopata.