Uchaguzi 2020 Huwezi kuwatishia wananchi ambao hawana cha kupoteza

Shule yenye wanafunzi zaidi ya mia tano unapeleka ruzuku ya shilingi laki moja kwa mwezi,zinaweza kufanyia nini?Shule hazina vyumba vya madarasa,nyumba za waalimu,vyoo vya wanafunzi/staff,madawati hakuna,vitabu na vifaa vya kufundishia nk.Hiyo ndiyo elimu bure tunayohubiriwa.Je,hayo ndiyo tuliyoahidiwa kuhusu elimu?Ndiyo tuliyostahili?
 
Safi, watu wanataka kusikia jinsi kipato chao kitaongezeka. Mfano unawaambia walima alizete bei itakuwaje na uwezekano wa kuuzika. Sasa ukiwwambia ndege na hata wengine hawajui hata ndani kukoje hawatakielewa.
Pambio la reli, barabara, flai ova nk. Limeshiba masikioni.

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Kama mtu hana chakupoteza maana yake ni kuwa hatishiki na hivyo haina maana kuongelea vitisho kwa watu ambao hawatishiki. Halafu hivyo vitisho unavyoongelea, ni tafsiri yako tuu
 
Watu wengi wanasubiri kufa just wamekosa hela ya kujitibu. Sikiliza njia pamda Redio Free Afrika Jumapili usikilize shida za watu. Sasa lissu akisema bima ya afya kwa kila mtu hawa walioko njia panda si watasema siku zikimbie wapige kura? Sasa ukimwambie ndege labda useme itatumika kuwapeleka mbinguni siku wakifa.ujue baba mtakatifu anaogopa kufa!

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Uzi bomba kabsa...
 
Wanaomzunguka wana matatizo makubwa zaidi

Sent from my Nokia 6.1 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu misamiati ya wanasiasa inahitaji utulivu kuielewa
Mfano anaposema yeye ni Rais wa wanyonge unaelewa vipi?
Elimu Bure unaelewa vipi?
1.wanyonge ni jamii ya watu masikini na mafukara kupindukia ki hali na mali
2,mnyonge ni mtu anaishi kwa hofu na uwoga na kujihisi ni mwenye hatia
3,mnyonge ni mtu ambae hata akikanyagwa bahati mbaya hawezi kusema kwa sababu ya khofu iliomjaa

Kwa maana hii je Mr Pombe amefanikiwa kiasi gani kutufanya tuwe wanyonge katika nchi yetu?
Tundu Lissu amekataa unyonge huu amekua shujaa nani alidhani kwa Tanzanian ilivyofikia tungeweza kumpata mtu wa kuzungumza hivi?
Tukija kwenye elimu ya Bure
Kila siku Bure ni ghali kuipata na haina thamani ukiwa nayo
Ukisikia mtu anasema kitu fulani ni Bure kabisa maana yake ni kitu cha hovyo
Na elimu ya Tanzania kwa Sasa ni Bure kabisa
Natarajia umenielewa
 
Lissu ni rais ajae wa Tanzania tumechoka na ccm tupo huvi tulivo kwa sababu yao hawana cha kutudanganya tuliwapa miaka zaidi ya 55 watuongoze lakin wameshindwa wapishe wengine tar 28 mwezi ujao nao tuone watatufikisha wapi.

Tunahitaji kujikomboa ki fikra, tuwe na mifumo bora na imara, Katiba bora na sio kutegemea hisani za mtawala yaani mtu mmoja ndo anakuwa mwamzi wa kila kitu kwa nchi yenye zaidi ya watu million 60, anatumia kodi zetu kufanya mambo mengine hayana ulazima wala umhimu kwa nchi

.Lissu ndio kiongozi sahihi kutuongoza kwa uhuru kamili wa fikra kwa taifa letu. Eti hivi sasa huduma miradi maendeleo afya,maji barabara ni hisani ya Mtawala ili hali raia wanapaswa kuhoji na kudai kadiri pato la taifa,michango nchi rafiki na jumuia za Kimataifa..

Haya mambo ya muteuana hatuyataki tunataka kuwa tunawachagua sisi wenyewe wenyenchi ndio yanaleta kubebana ,kuiba na kufichiana maovu .miaka zaidi ya 55 wameshindwa ni zamu ya wengine ccm watuache kidogo Watanzania tuna jambo letu tar 28 wa 10
 
Hivi Kuna kitu mmegundua humu mitandaoni?
Sioni tena wale watetezi wa chama Cha mbogamboga kwa wingi ulee uliokuwa mwanzo naona hata hao wamerudi kwenye uhalisia kwa kiasi Fulani

Hakuna hoja ambayo wanaweza kutoa ikawa na mashiko zaidi ya kuonekana tu wapambe
Tanzania tunaenda kuzungumza lugha moja Sasa
 
Kuna mgombea ni mzuri sana kwenye claiming na sio kwenye reasoning. Anaweza haidi atawanunulia ndege watu wa kijijini ambao hata wachange wote kijiji kizima hazitoshi nauli ya kupanda ndege
Hii nimeielewa. Asante.
 
Ameshindwa kujua changamoto za watu wa eneo hilo . labda anadhani watu wa eneo hilo wanahitaji ndege na ndio kipaumbele chao.
 
Mimi mwenyewe nimebaki kuwa ccm nafasi tu ,lakini moyoni nampenda Lissu na sio chadema
 
JPM ananadi sera wakati Lissu analalamika kapigwa risasi 16.sasa kupigwa kwake risasi 16 zinamuhusu nini mwananchi wa kijijini?
Sera gani za kununua ndege, unaenda kijjijini unanadi Sera za kununua ndege , wakati zahanati hakuna madawa, hiyo akili matope
 
Naona wanyonge wameanza kujua kwamba wanaibiwa. Nampenda mchungaji wangu, aliniambia hakuna unyonge kwa yesu. Unyonge ni sifa ya shetani. Unyonge ni ile hali ya kusumbuliwa na dhambi
 
Pana mgombea anapitapita anawatishia wapiga kura wasipowachagua asiowataka atawashughulikia atowaletea maendeleo japo Kodi zao anachukua hapa tume wamekaa kimya hawaoni
 
Huyu mzee kwake maendeleo ni ndege
 
sasa kweli sisi wa vijijini tumekosa uhuru lini mpaka ulete na Lissu maana hata gongo tunakunywa na kulewa hadharani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…