Econometrician
JF-Expert Member
- Oct 25, 2013
- 17,929
- 33,764
Ni nchi gani hapa duniani iliwahi kufanikiwa katika nyanja zote bila machafuko??Kwa hiyo mwanasiasa mwenye historia chafu kama Martha naye aruhusiwe kuingilia mambo ya nchi? Kuweni serious
Mnatumia nguvu kubwa kujaribu kukosoa maamuzi ya Rais kwa kuja na hoja za wakati wa kupigania uhuru.Tarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.
Katika habari picha mojawapo, Rais alinukuliwa akisema: "Tusitoe nafasi kwa wanaharakati wa nje kuingilia masuala ya Tanzania"! Kama kauli hiyo ni ya Rais Samia Saluhu Hassan, nchi yetu itakuwa imefikia hatua mbaya sana kwani hata Rais amejua kuwa tumefikia mahali ambapo tunahitaji watu au wanaharakati wa nje kutetea wananchi wa Tanzania.
Huko nyuma kuanzia mwaka 1961 hadi 1990, wanaharakati, wanasiasa na viongozi kutoka Tanganyika na baadaye Tanzania ndio ambao walikuwa wakiingilia masuala ya nchi jirani au nchi za nje. Wanaharakati, wanasiasa, watetezi na viongozi hao waliokuwa wakiingilia mambo ya nchi nyingine waliongozwa na Rais Julius Nyerere mwenyewe.
Wakati Rais wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda anatesa na hata kuua watu wake, nchi ya Tanzania sio tu kuwa iliingilia masuala ya nchi ya Malawi, bali pia iliwapa hifadhi watu na wakimbizi kutoka Malawi akiwemo mwandishi nguli aliyekuwa akiandikia gazeti la Daily News.
Wakati Idi Amini Dada alipoipindua serikali ya Uganda na kumuondosha madarakani Rais Milton Obote, Rais Nyerere aliingilia masuala ya Uganda, akaenda mbali zaidi akawa hifadhi Milton Obote, Yoweri Kaguta Museveni, nk.
Wakati Afrika Kusini ilipokuwa chini ya mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, Tanzania ya Rais Julius Nyerere iliingilia masuala ya Afrika Kusini kwa kuhamasisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo ikatoa ardhi kwa wapiganaji wa Afrika Kusini.
Nchi nyingine ambazo ziliingiliwa wanasiasa, wanaharakati na wapiganaji wa Tanganyika na baadaye Tanzania ni pamoja na Rhodesia (sasa Zimbabwe), Msumbiji, Angola, Namibia, Algeria, nk.
Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.
Kama asilimia kubwa ya Watanzania wanajua ya kuwa upinzani unanyanyaswa nchini huku viongozi wao kama Ali Kibao wameuawa na wengine kama Soka, Kipanya, Chaula, Mlay, Mbise na Mdude wametekwa na hawajulikani waliko, hautarajiwi kuwa wanaharakati wa nchi za jirani wasijue kuwa kuna ufinyaji wa haki za msingi nchi ikiwemo haki ya kuishi.
Lissu alipigwa risasi 16 mchana kweupe akiwa katika majengo ya serikali yanayolindwa pia na serikali lakini hadi sasa hakuna mtu ye yote aliyekamatwa na wala hakuna uchunguzi wo wote uliofanywa hadi sasa. Lissu amekamatwa na kupewa makosa mazito kabisa duniani ya uhaini ambayo hatima yake ni kunyongwa hadi kufa. Katika mazingira kama hayo, haitarajii ya kuwa wanaharakati kutoka nje za nje watakaa kimya wasiingilie mambo ya Tanzania. Kama Tanzania ilitia sahihi mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu, ni lazima itaingiliwa na wanaharakati kutoka nchi za nje.
Kama wao Rais Samia, CCM pamoja na serikali yake wanataka Tanzania isiingiliwe na watu au wanaharakati kutoka nchi za nje, basi wafanye mambo mawili. Mosi, waandike katiba mpya au wabadili katiba iliyopo ili wanyofoe kifungu kile kinacholinda haki za binadamu. Pili, wafanye haraka sana juhudi kuiondosha Tanzania katika mikataba yote ya kimataifa. Baada ya kufanya hivyo, waiondoe Tanzania kutoka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA, SADC, nk.
Wakimaliza kufanya yote hayo, ndipo Tanzania ivunje uhusiano wa Kibalozi katika nchi zote duniani na iwaite Mabalozi wake wote walioko katika nchi hizo, mwisho iwafukuze Mabalozi wote wa nchi za kigeni walioko Tanzania. Hapo ndipo itoe kauli ya kutokuingiliwa na wanasiasa na wanaharakati kutoka nchi za nje kwani sasa Tanzania itakuwa tayari ni Kisiwa cha Mbudya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam, 20 Mei 2025; saa 3:45 asubuhi.
Mnatumia nguvu kubwa kujaribu kukosoa maamuzi ya Rais kwa kuja na hoja za wakati wa kupigania uhuru.
Lissu aliyeongea uchonganisha huwezi kumlinganisha na kina Samora Machel waliopambana na makaburu mpaka wakafa kwa ndege kutunguliwa ikiwa angani.
Kina Mandela waliolala jela miaka 27 huwezi kuwalinganisha na hawa wanasiasa wanaofanya shughuli ya usaliti kwa mataifa yaliyowasomesha na kuwalea tangu wakiwa watoto wasioelewa nini kinaendelea duniani.
Siasa ya vyama vingi imekuja huku afrika ikiwa ni sehemu ya matakwa ya mataifa yetu kuweza kukidhi vigezo vya kupatiwa misaada, hatuna asili ya mfumo huu. Kwa bahati mbaya kwa kusema hivyo maana yake mzungu anaendelea kututawala kwa kutumia siasa aliyoileta.
Tanzania yenye kudumu kwa miaka 64 ya utulivu haiwezi kuwafurahisha wazungu, hawawezi kutupenda kwa namna yoyote ile mfano ni namna DRC wanavyouana halafu kiulaini mzigo wa madini unakwenda huko huko Ulaya kuwatajirisha wazungu.
Kaulize UNNi nchi gani hapa duniani iliwahi kufanikiwa katika nyanja zote bila machafuko??
Inasikitisha sanaHuyu Martha ni kibibi cha miaka 67,badala ya kulea wajukuu,anazurura.hii ndio inasababisha Kenya kuwa na chokoraa wengi,na wavuta gundi,kutokana na vibibi wa kuwalea,wanazurura, nao wamekuwa chokoraa.
uko sahihi mno comrade,Ni kwa nia njema ya kuwajulisha wasiomjua Martha Karua hasa upande wake wa uovu. Mwaka 2007 hadi mwanzoni mwa 2008 kulitokea machafuko ya baada ya uchaguzi yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1500, ubakaji wa zaidi ya wanawake 3000 huku watu zaidi ya 300,000 wakipoteza makazi yao. Ulikuwa ni unyama mkubwa mno zilizosababishwa na siasa za kijinga na genge lake.
Ikumbukwe Martha Karua alikuwa mshauri wa karibu wa hayati Rais Mwai Kibaki kama waziri wa sheria na katiba. Hivyo hawezi kuepuka lawama alizokuwa anatupiwa Rais Kibaki kuhusu machafuko hayo. Wakati wa maongezi ya amani kati ya upande wa Raila na Kibaki, Martha alikuwa kiongozi wa kambi ya Kibaki kwenye hayo mazungumzo.
Vyombo vya dola kumzuia mhusika wa machafuko nchini kwake kutoingia nchini ni kitu cha kupongezwa na wazalendo wote. Walifanya vyema sana.
Nampongeza zaidi Rais Samia Suluhu kwa ushupavu wake kama Amiri jeshi mkuu kukemea Martha Karua na wanaharakati wengine toka nchi jirani wanaotamani kuleta machafuko kama ya 2007 nchini Kenya.
Swali zuri sanaWaliohusika na machafuko walipelekwa ICC mmojawapo ni Ruto. Martha alituhumiwa wapi?
RUTO akija TZ mnampokea huku mkiwa mnabinua makalio kwa kunengua
Hiyo katiba mpya iliyofanya waandamane kisa hawana unga wa kupikia ugali?Hakuna kizuri kinakuja bila gharama,hata wangefariki watu milioni 10 but at the end wamepata Katiba mpya na nzuri,na wananufaika na matunda uchumi wao.
Sasa sisi hapa Tanzania ambapo hatuna katiba nzuri na hakuna kifo tumenufaika na nini??
Kwa hiyo mwanasiasa mwenye historia chafu kama Martha naye aruhusiwe kuingilia mambo ya nchi? Kuweni serious
Kundi la wajinga wa Ccm kazini.Ni kwa nia njema ya kuwajulisha wasiomjua Martha Karua hasa upande wake wa uovu. Mwaka 2007 hadi mwanzoni mwa 2008 kulitokea machafuko ya baada ya uchaguzi yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1500, ubakaji wa zaidi ya wanawake 3000 huku watu zaidi ya 300,000 wakipoteza makazi yao. Ulikuwa ni unyama mkubwa mno zilizosababishwa na siasa za kijinga na genge lake.
Ikumbukwe Martha Karua alikuwa mshauri wa karibu wa hayati Rais Mwai Kibaki kama waziri wa sheria na katiba. Hivyo hawezi kuepuka lawama alizokuwa anatupiwa Rais Kibaki kuhusu machafuko hayo. Wakati wa maongezi ya amani kati ya upande wa Raila na Kibaki, Martha alikuwa kiongozi wa kambi ya Kibaki kwenye hayo mazungumzo.
Vyombo vya dola kumzuia mhusika wa machafuko nchini kwake kutoingia nchini ni kitu cha kupongezwa na wazalendo wote. Walifanya vyema sana.
Nampongeza zaidi Rais Samia Suluhu kwa ushupavu wake kama Amiri jeshi mkuu kukemea Martha Karua na wanaharakati wengine toka nchi jirani wanaotamani kuleta machafuko kama ya 2007 nchini Kenya.
Hii ni tofauti na ya kwenu ambayo Rais ni Mungu..Hiyo katiba mpya iliyofanya waandamane kisa hawana unga wa kupikia ugali?
Uchaguzi huru ni siasa zetu za ndani, Samia kapinga huyo Mama na mashoga zake kutoka Kenya kuja kutuletea vurugu humu TZ.Nyie ndiyo mnatumia nguvu nyingi na mali nyingi kuhalalisha dhuluma. Hivi kwako uchaguzi huru na haki ni tatizo?
Hizi nadharia haziwazuii kina Ruto kupiga mabilioni kwa mabilioni ya mapesa.Hii ni tofauti na ya kwenu ambayo Rais ni Mungu..
Haya ni manufaa matano ya Katiba mpya ya Kenya ya mwaka 2010:
1. Ugatuzi wa madaraka
Katiba mpya ilianzisha mfumo wa ugatuzi (devolution), ambapo serikali za kaunti 47 zilianzishwa. Hii imeleta huduma karibu na wananchi, kukuza maendeleo ya maeneo ya mashinani na kupunguza msongamano wa maendeleo katika miji mikuu pekee.
2. Ulinzi wa haki za binadamu
Katiba mpya ina sura nzima (Sura ya 4 – Bill of Rights) inayolinda haki za binadamu kama vile haki ya kuishi, elimu, afya, uhuru wa kujieleza, na usawa mbele ya sheria.
3. Utawala bora na uwajibikaji
Katiba ilianzisha taasisi huru kama Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), Tume ya Huduma za Polisi, na Tume ya Uchaguzi (IEBC), ambazo huchochea uwazi, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.
4. Ushirikishwaji wa umma
Katiba inatambua na kutekeleza ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya serikali kupitia vikao vya hadhara, maoni ya umma na mchakato wa bajeti. Wananchi sasa wana sauti katika masuala ya maendeleo ya maeneo yao.
5. Uongozi wa kikatiba ulio wazi
Katiba mpya imeweka masharti wazi kuhusu uongozi bora kupitia kipengele cha Leadership and Integrity (Sura ya 6), ambacho kinatathmini tabia, maadili na uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Wangekuwa wanafuata haki mamia ya Gen Z wasingeuliwa kama kuku kwenye maandamano miezi michache iliyopita... kimsingi umeandika mambo ya kusadikika ambayo wakenya wenyewe hawaishi humo. Kama Kenya ni kipimo cha uadilifu kwa Tanzania basi dunia imefikia mwisho wake. Wewe ulishawahi hata kukaa Nairobi kwa siku 4 tu ukajionea maisha ya kule?Hii ni tofauti na ya kwenu ambayo Rais ni Mungu..
Haya ni manufaa matano ya Katiba mpya ya Kenya ya mwaka 2010:
1. Ugatuzi wa madaraka
Katiba mpya ilianzisha mfumo wa ugatuzi (devolution), ambapo serikali za kaunti 47 zilianzishwa. Hii imeleta huduma karibu na wananchi, kukuza maendeleo ya maeneo ya mashinani na kupunguza msongamano wa maendeleo katika miji mikuu pekee.
2. Ulinzi wa haki za binadamu
Katiba mpya ina sura nzima (Sura ya 4 – Bill of Rights) inayolinda haki za binadamu kama vile haki ya kuishi, elimu, afya, uhuru wa kujieleza, na usawa mbele ya sheria.
3. Utawala bora na uwajibikaji
Katiba ilianzisha taasisi huru kama Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC), Tume ya Huduma za Polisi, na Tume ya Uchaguzi (IEBC), ambazo huchochea uwazi, uwajibikaji na mapambano dhidi ya rushwa.
4. Ushirikishwaji wa umma
Katiba inatambua na kutekeleza ushiriki wa wananchi katika maamuzi ya serikali kupitia vikao vya hadhara, maoni ya umma na mchakato wa bajeti. Wananchi sasa wana sauti katika masuala ya maendeleo ya maeneo yao.
5. Uongozi wa kikatiba ulio wazi
Katiba mpya imeweka masharti wazi kuhusu uongozi bora kupitia kipengele cha Leadership and Integrity (Sura ya 6), ambacho kinatathmini tabia, maadili na uwajibikaji wa viongozi wa umma.
Sema huyu maza hazeeki...