Ndio nimekaa zaidi ya miezi na ni majirani zangu! Kuhusu uwazi na uwajibikaji na Uhuru wa kujieleza Kenya wako vizuri katika Hilo ni uwongo usiopingika! Unless unaamua kubisha!Wangekuwa wanafuata haki mamia ya Gen Z wasingeuliwa kama kuku kwenye maandamano miezi michache iliyopita... kimsingi umeandika mambo ya kusadikika ambayo wakenya wenyewe hawaishi humo. Kama Kenya ni kipimo cha uadilifu kwa Tanzania basi dunia imefikia mwisho wake. Wewe ulishawahi hata kukaa Nairobi kwa siku 4 tu ukajionea maisha ya kule?
Maisha ya Kenya ni magumu yaliyojaa chuki ndani yake. Sio maisha ya kuiga kabisa. Uhuru mnaousemea nyie ni uhuru wa kutukana kitu ambacho kamwe ndani ya Tanzania hakitakubalika.Ndio nimekaa zaidi ya miezi na ni majirani zangu! Kuhusu uwazi na uwajibikaji na Uhuru wa kujieleza Kenya wako vizuri katika Hilo ni uwongo usiopingika! Unless unaamua kubisha!
Imekaa vizuri sana hiyoTarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.
Katika habari picha mojawapo, Rais alinukuliwa akisema: "Tusitoe nafasi kwa wanaharakati wa nje kuingilia masuala ya Tanzania"! Kama kauli hiyo ni ya Rais Samia Saluhu Hassan, nchi yetu itakuwa imefikia hatua mbaya sana kwani hata Rais amejua kuwa tumefikia mahali ambapo tunahitaji watu au wanaharakati wa nje kutetea wananchi wa Tanzania.
Huko nyuma kuanzia mwaka 1961 hadi 1990, wanaharakati, wanasiasa na viongozi kutoka Tanganyika na baadaye Tanzania ndio ambao walikuwa wakiingilia masuala ya nchi jirani au nchi za nje. Wanaharakati, wanasiasa, watetezi na viongozi hao waliokuwa wakiingilia mambo ya nchi nyingine waliongozwa na Rais Julius Nyerere mwenyewe.
Wakati Rais wa Malawi, Dkt. Hastings Kamuzu Banda anatesa na hata kuua watu wake, nchi ya Tanzania sio tu kuwa iliingilia masuala ya nchi ya Malawi, bali pia iliwapa hifadhi watu na wakimbizi kutoka Malawi akiwemo mwandishi nguli aliyekuwa akiandikia gazeti la Daily News.
Wakati Idi Amini Dada alipoipindua serikali ya Uganda na kumuondosha madarakani Rais Milton Obote, Rais Nyerere aliingilia masuala ya Uganda, akaenda mbali zaidi akawa hifadhi Milton Obote, Yoweri Kaguta Museveni, nk.
Wakati Afrika Kusini ilipokuwa chini ya mfumo wa utawala wa ubaguzi wa rangi, Tanzania ya Rais Julius Nyerere iliingilia masuala ya Afrika Kusini kwa kuhamasisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya nchi hiyo ikatoa ardhi kwa wapiganaji wa Afrika Kusini.
Nchi nyingine ambazo ziliingiliwa wanasiasa, wanaharakati na wapiganaji wa Tanganyika na baadaye Tanzania ni pamoja na Rhodesia (sasa Zimbabwe), Msumbiji, Angola, Namibia, Algeria, nk.
Lakini pia hakuna asiyejua ya kuwa wakati wa utawala wa Mobutu Seseko wa Zaire (sasa DR Congo), Tanzania iliingilia masuala ya Zaire kwa kuwahifadhi Desire Kabila (Baba Ntwale) na mwanaye hadi wakafanikisha kumuondoa madarakani Rais Mobutu. Mifano haiishi kwani sio watu wengi wanajua kuwa wanajeshi wetu walikwenda katika Visiwa vya Commoro. Lakini kama walikwenda kutembea au walikwenda kula pikiniki, ajuaye ni Rais Kikwete na Jenerali wake Davis Mwamunyange.
Kama asilimia kubwa ya Watanzania wanajua ya kuwa upinzani unanyanyaswa nchini huku viongozi wao kama Ali Kibao wameuawa na wengine kama Soka, Kipanya, Chaula, Mlay, Mbise na Mdude wametekwa na hawajulikani waliko, hautarajiwi kuwa wanaharakati wa nchi za jirani wasijue kuwa kuna ufinyaji wa haki za msingi nchi ikiwemo haki ya kuishi.
Lissu alipigwa risasi 16 mchana kweupe akiwa katika majengo ya serikali yanayolindwa pia na serikali lakini hadi sasa hakuna mtu ye yote aliyekamatwa na wala hakuna uchunguzi wo wote uliofanywa hadi sasa. Lissu amekamatwa na kupewa makosa mazito kabisa duniani ya uhaini ambayo hatima yake ni kunyongwa hadi kufa. Katika mazingira kama hayo, haitarajii ya kuwa wanaharakati kutoka nje za nje watakaa kimya wasiingilie mambo ya Tanzania. Kama Tanzania ilitia sahihi mikataba ya kimataifa juu ya haki za binadamu, ni lazima itaingiliwa na wanaharakati kutoka nchi za nje.
Kama wao Rais Samia, CCM pamoja na serikali yake wanataka Tanzania isiingiliwe na watu au wanaharakati kutoka nchi za nje, basi wafanye mambo mawili. Mosi, waandike katiba mpya au wabadili katiba iliyopo ili wanyofoe kifungu kile kinacholinda haki za binadamu. Pili, wafanye haraka sana juhudi kuiondosha Tanzania katika mikataba yote ya kimataifa. Baada ya kufanya hivyo, waiondoe Tanzania kutoka katika Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Madola, Jumuiya ya Afrika Mashariki, COMESA, SADC, nk.
Wakimaliza kufanya yote hayo, ndipo Tanzania ivunje uhusiano wa Kibalozi katika nchi zote duniani na iwaite Mabalozi wake wote walioko katika nchi hizo, mwisho iwafukuze Mabalozi wote wa nchi za kigeni walioko Tanzania. Hapo ndipo itoe kauli ya kutokuingiliwa na wanasiasa na wanaharakati kutoka nchi za nje kwani sasa Tanzania itakuwa tayari ni Kisiwa cha Mbudya!
Je, nini kimekushangaza? Je, nini maoni yako?
Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!
Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula
Itunge, Dar es Salaam, 20 Mei 2025; saa 3:45 asubuhi.
NO REFORMS, NO ELECTION.Tarehe 19 Mei 2025 ni siku iliyokuwa imebana sana kwangu. Sikuweza kufanikiwa kufuatilia hotuba yeyote iliyotolewa na Mheshimiwa Rais Samia Saluhu Hassan. Hata hivyo, usiku niliona habari picha kadhaa zikiwa na maneno ambayo yanaelezwa kuwa yalitolewa na Rais Samia.