Huwezi pata watendaji wazuri ikiwa utaongoza kwa umungu mtu!

Huwezi pata watendaji wazuri ikiwa utaongoza kwa umungu mtu!

mr pipa

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2021
Posts
3,074
Reaction score
6,472
Hiyi nchi sio kwamba viongozi walio chini ya uongozi mkuu hawawezi wajibika hapana isipokuwa mamlaka aliyopewa Raisi ni makubwa kuliko uhalisia au uwezo halisi.

Mimi naamini tuna viongozi bora sana na wenye nia ya kujituma ila kwakuwa mkuu ndio mwenye mamlaka ya kila kitu kitachofuata utafanya kazi kwa kujipendekeza kwa mkuu ili ulinde cheo.

Ndio maana kwenye nchi hii polisi kujipendekeza kwenye mamlaka husika wabunge, mawaziri, nk na sio kwamba wanapenda. Mtawalaumu bure shida ipo alietunga sheria ya kumpa Rais mamlaka zote, huyo huyo mkuu wa majeshi, huyo huyo mkuu wa nchi, huyo huyo mwenyekiti wa chama halafu mtake matokeo mazuri, never!

Kumbuken Rais ni binadam na asili ya binadam anapopewa mamlaka kama hizi kuna kiroho fulani hivi kakuamini wewe ndio mwisho, hata wewe msomaji ukipewa Urais kazi ni hii hii mnayoiona kwa huyu, hakutokuwa na badiliko lolote.

Alaumiwe alietunga sheria ya kumpa Rais mamlaka zote hizo, hawa polisi, mawazi,wabunge, nk mtawaonea bure hawana na hawawezi kufanya lolote mbele ya mamlaka ya Urais wa namna hii. Kilichobaki kila mtu atetee tumbo lake.

Ila mkitaka hii nchi iende mnavyotaka mvueni baadhi ya vyeo Rais, hapo ndipo mtaona matokeo ya utendaji wa vyombo vyote vilivyo chini ya Urais.

Je, ni nani ataweza kuvua hivyo vyeo ikiwa Rais ndie mshika steling mbinu zipo mbili? Moja, wananchi wenyewe muamue kwa pamoja kwenye mbinu hiyi lazima mkubali kuumia kuna vitu ving vitatokea vifo, majeruhi nk mbinu ya pili jeshi liamue kwaajili ya wananchi, kwenye hili mtasubiri sana.

NB: Hakuna mpinzani, au nchi itayokuja kukutetea mwananchi ikiwa wemwenyewe umekaa kama bendera ya chuma kiufupi wacha wale kwanza.
 
Hiyi nchi sio kwamba viongozi walio chini ya uongozi mkuu hawawezi wajibika hapana isipokuwa mamlaka aliyopewa raisi ni makubwa kuliko uhalisia au uwezo halisi mimi naamini tunaviongozi bora sana na wenye nia ya kujituma ila kwakuwa mkuu ndio mwenye mamlaka ya kila kitu kitachofuata utafanya kazi kwa kujipendekeza kwa mkuu ili ulinde cheo ndio maana kwenye nchi hiyi polisi kujipendekeza kwenye mamlaka husika wabunge, mawaziri, nk na sio kwamba wanapenda mtawalaumu bure shida ipo alietunga sheria ya kumpa raisi mamlaka zote, huyo huyo mkuu wa majeshi huyo huyo mkuu wa nchi huyo huyo mwenyekiti wa chama alafu mtake matokeo mazuri never kumbuken rais ni binadam na asili ya binadam anapopewa mamlaka kama hizi kuna kiroho fulani hivi kakuamin wewe ndio mwisho hata wewe msomaji ukipewa uraisi kazi ni hiyi hiyi mnayoiona kwa huyu hakutokuwa na badiliko lolote alaumiwe alietunga sheria ya kumpa raisi mamlaka zote hizo hawa polisi, mawazi,wabunge, nk mtawaonea bure hawana na hawawez kufanya lolote mbele ya mamlaka ya uraisi wa namna hiyi kilichobaki kila mtu atetee tumbo lake ila mkitaka hiyi nchi iende mnavyotaka mvuen baadhi ya vyeo raisi hapo ndipo mtaona matokeo ya utendaji wa vyombo vyote vilivyo chini ya uraisi je ni nani ataweza kuvua hivyo vyeo ikiwa raisi ndie mshika steling mbinu zipo mbili, moja wananchi wenyewe muamua, kwa pamoja kwenye mbinu hiyi lazima mkubali kuumia kuna vitu ving vitatokea vifo majeruhi nk mbinu ya pili jeshi liamue kwaajili ya wananchi kwenye hili mtasubiri sanaa NB hakuna mpinzani, au nchi itayokuja kukutetea mwananchi ikiwa wemwenyewe umekaa kama bendera ya chuma kiufupi wacha wale kwanza
Kama tumefeli leadership, ziko nchi zilizopiga hatua kubwa, tujifunze kwao. Ila hofu yangu, je tuna dhamira, nia na malengo ? Sababu ya mtu kuutaka uongozi ni kutajirika, au kutumika ? Ziko nchi Kiongozi wa nchi anatafutwa kwa vetting hatari, sio uchama, au kadi ya chama. Sifa ya Kiongozi ukiiona imesimama, imeshiba, imenyooka, imetukuka. Hapa kwetu Africa bado. Tunaendekeza HISTORIA. Mtoto/mjukuu wa waziri, Rais, mkurugenzi nk bila kuzingatia uwezo, umakini, uzalendo na Karama ya uongozi .
 
Back
Top Bottom