<br /><b>mwanaume kujua fungu la nyanya sokoni ni sh ngapi na vitunguu vya mia ni vingapi ni haki? kila mtu akae kwa heshima zake bwana yaani mume wangu kabisa atwange tangawizi na kukuna nazi sipati photo</b>
Mhhhh mkuu usitake tufike huko
Tuishie kwetu bara huku huku ambako tunajua wapi na lipi la kufanya
hahahaah..
kalikuwa kamfano tu mkuu..lol!
Na ishu ya kuacha matumizi ya nyumbani mbona hujaiongelea??
Kila mtu ana roles zake kwenye familia mkuu!
mbona siku hizi tunasaidiana katika kutoa matumizi, kusomesha watoto, kujenga na mengineyo? Mbona basi tusisaidiane katika majukumu mengine ya nyumbani? Mie naona ni kuendekeza mfumo dume na kutotaka kukubali mabadiliko. Utakuta asubuhi mnadamka nyote kwenda kaznini, lakini mwanaume anataka aandaliwe chai, apigiwe pasi nguo zake awekewe maji ya kuoga, abrushiwe viatu, na briefcase yake aletewe.
Mh....!
Salaam wadau,
Nimejaribu kuangalia kwa kina maisha ya ndoa hasa hizi za kiafrika, kipekee za kitanzania na nimegundua kuwa wengi wa wanaume huwafanya wanawake kuwa ni "watumwa" wao.
Yaani wanaume huwatumikisha wake zao kupita kiasi. Kuanzia kufua, kupika, kuosha vyombo na mikazi mingine kibao....bado mume akiwa ameketi atataka apakuliwe chakula, atengewe, hadi mikono eti anawishwe...Hivi ni kweli wewe mwanaume unashindwa hata kupakua chakula kutoka kwenye hotpot hadi upakuliwe..?
Mara atataka anyooshewe nguo, viatu ang'arishiwe....dah too much jamani!
Hivi huyo ni mkeo au mtumishi wako..!?
Modern men need to change bwanaaa!
Swala la wanawake kuwahudumia waume zao lilianzia mbali sana, tangu enzi hizo, kuwa majukumu ya kazi za nyumbani ni za mama na baba kazi yake ilikuwa ni kutafuta mahitaji ya nyumbani na kuitunza familia.... sisi tumezaliwa tumekuta hivyo, sio rahisi leo hii umwambie kijana aliyelelewa na kukuta kwamba kazi zote za nyumbani kwao alikuwa anazifanya mama yake na baba yake alikuwa akishinda kwenye Bao au kwenye baraza la Kahawa, leo umwambaie amsaidie mkewe kwa kuwa huo ni mgawanyo wa kazi, atakuona unamtusi. mimi binafsi niliwahi kushuhudia kaka akimfokea dada yake kisa eti kamuacha mumewe awapikie, alidai kuwa hayo ni matusi kwao, lakini kumbe mume aliamua kumsaidia mkewe kupika, kwao lilikuwa ni jambo la kawaida lakini kwa kaka mtu ilikuwa ni matusi.
Muingiliano wa tamaduni hasa kutoka Magharibi umeleta mabadiliko makubwa katika baadhi ya ndoa za vijana, wanasaidiana kazi kama ulivyobainisha, lakini hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, siku hizi wanandoa wote wanatakiwa kuchangia pato la familia, kwa hiyo wote wanawajibika, lakini kwa kuwa bado baba anaonekana kuwa ni kichwa cha familia, hawezi kushiriki hizo kazi za nyumbani, ndio maana nafasi hiyo ikachukuliwa na mtumishi wa nyumbani tunaita House girl. ni kwa nini? Ni kwa sababu bado kuna wanaume ambao hawako tayari kubadilika kwa sababu jamii imewaambia kuwa hizo ni kazi za wanawake.
Lakini pia kuna malalamiko kuwa wanawake nao, wakisaidiwa, hujisahau na wakati mwingine huwavunjia waume zao heshima, pale ambapo kuna wageni mke anaweza kumuinua mume, tena bila haya na kumwambia 'leo ni zamu yako kupika' kuna wanaume wengine huchuklulia jambo hilo kama kudhalilishwa.....
Mabadiliko yapi unaongelea??
Mbona bailojia hazijabadilika??
Mbona umesoma kama vile una kengeza? Umeona hicho kipande tu, bila kukihusianisha na vipande vingine? Soma post ya mtambuzi hapo chini imenisaidia sana kujibu hoja yako. Asante
Swala la wanawake kuwahudumia waume zao lilianzia mbali sana, tangu enzi hizo, kuwa majukumu ya kazi za nyumbani ni za mama na baba kazi yake ilikuwa ni kutafuta mahitaji ya nyumbani na kuitunza familia.... sisi tumezaliwa tumekuta hivyo, sio rahisi leo hii umwambie kijana aliyelelewa na kukuta kwamba kazi zote za nyumbani kwao alikuwa anazifanya mama yake na baba yake alikuwa akishinda kwenye Bao au kwenye baraza la Kahawa.
Leo umwambaie amsaidie mkewe kwa kuwa huo ni mgawanyo wa kazi, atakuona unamtusi. mimi binafsi niliwahi kushuhudia kaka akimfokea dada yake kisa eti kamuacha mumewe awapikie, alidai kuwa hayo ni matusi kwao, lakini kumbe mume aliamua kumsaidia mkewe kupika, kwao lilikuwa ni jambo la kawaida lakini kwa kaka mtu ilikuwa ni matusi.
Muingiliano wa tamaduni hasa kutoka Magharibi umeleta mabadiliko makubwa katika baadhi ya ndoa za vijana, wanasaidiana kazi kama ulivyobainisha, lakini hiyo ni kutokana na mabadiliko ya kiuchumi, siku hizi wanandoa wote wanatakiwa kuchangia pato la familia, kwa hiyo wote wanawajibika, lakini kwa kuwa bado baba anaonekana kuwa ni kichwa cha familia, hawezi kushiriki hizo kazi za nyumbani, ndio maana nafasi hiyo ikachukuliwa na mtumishi wa nyumbani tunaita House girl. ni kwa nini? Ni kwa sababu bado kuna wanaume ambao hawako tayari kubadilika kwa sababu jamii imewaambia kuwa hizo ni kazi za wanawake.
Lakini pia kuna malalamiko kuwa wanawake nao, wakisaidiwa, hujisahau na wakati mwingine huwavunjia waume zao heshima, pale ambapo kuna wageni mke anaweza kumuinua mume, tena bila haya na kumwambia 'leo ni zamu yako kupika' kuna wanaume wengine huchuklulia jambo hilo kama kudhalilishwa.....
Najua kwamba mfumo ndo umetutengeneza hivyo. Sasa kwa kutumia kigezo hicho hicho cha mfumo, ili tusionekane tumebadilika kwa kasi kwani kwa kufanya hivyo inakuwa ngumu kueleweka na jamii; basi si vibaya kufanya baadhi ya kazi hasa zile zinazotuhusu moja kwa moja kama mume, mfano kama nilivyoainisha awali: kunyoosha nguo zako, kung'arisha viatu...n.k. Kwani tukifanya kazi za aina hiyo nini kinaharibika hapo? Au hata wakikukuta watu unafanya kazi kama hizo ni aibu gani utapata hapo...bado sijaona ubaya! Si lazima tupike na kuosha vyombo.
Kusaidiana kupo lakini sio kanuni,kazi za ndani zote zinamuhusu wife,ikimsaidia mara moja moja poa.Lakini kuto kumsaidia sio tatizo..na mwanamke mwenye kujitambua hilo sio tatizo kwake.We leta uzungu hapo kwako,kama unaosha vyombo kila mara ni majukumu yako tayari,na usipofanya mkeo atakuhoji.Kuwa makini na hilo,huduma hizo ndo zina thamani kubwa kwa mwanamume kufanyiwa na mkewe na zinamfanya mwanamume ampende mkewe zaidi.
swala ni whom you get married to,olewa na mzungu hizo kazi za nyumbani mtazigawanya 50/50...olewa na mbongo utafua hadi sox zake.....msitutusakame mnapoona tunakimbilia kuolewa na wazungu hata kama ni vibabu......at least hawatakutreat kama mtumwa!..

Kwani nyumbani kwako anazifanya nani?
Kwangu zinafanywa na wasichana wa kazi....Kwa hiyo hata hoja ya kumsaidia wife siioni kwani keshasaidiwa long time!!