DOKEZO Huyu Afisa anaichafua LATRA-Morogoro, anachukua fedha za stika na faini za Madereva Bajaji na kuanza kuwatisha

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kuna Afisa mmoja wa LATRA Morogoro anafahamika kwa jina la Fadhili, huyu mtu ni hatari sana kwa Vijana wanaoendesha Bajaji, anatutesa sana sisi Vijana na kinachouma zaidi ni kuwa inavyoonekana Wakubwa wake wa kazi wanajua michezo yake lakini nao wapo kimya.

Afisa huyu ana mtindo wa kulazimisha vijana wampe hela za kulipia Stika ya LATRA, anatuambia tumpe yeye ndiye atalipia.

Ikitokea amekwambia umpe hela ya stika au ya faini akakulipie kwenye mfumo ukakataa na kutaka Control Number ili ulipe mwenyewe, utazungushwa kwa kuambiwa Mtandao au sababu nyingine yoyote.

Kwakuwa tunamjua ni mtumishi wa ofisi hiyo tulikuwa tukimuamini na kumpa hela za kulipia faini na stika zinazotakiwa ili kupunguza usumbufu.

Fadhili (katikati)
Sasa tulivyoanza kumshtukia kuwa anatupiga ni baada ya kuwa kila aliyempa hela kwaajili ya kulipiwa alikuja kubaini kuwa kama ni deni lipo palepale.

Alituzungusha kwa muda wa miezi mitatu tulipobaini kuwa fedha ambazo tulimpa akatulipie hazijalipwa, kwa kuwa tulipokutana na maafisa wengine Barabarani walitukamata kututaka tulipe.

Kuna tukio moja lilitokea Machi 28, 2023, bosi mmoja wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) aliongoza zoezi la kukamata Bajaji ambazo hazina Stika za LATRA, waliokamatwa walikuwemo wale ambao walimpa Fadhili fedha ili akawalipie, pikipiki na bajaji zao zikaenda kufungiwa Manispaa.

Wale wenzetu ambao walimpa fedha Fadhili ikabidi wamfuate, alipoona msala umekuwa mkubwa akawarudishia baadhi fedha walizompa na kuwaambia “wapambane kujitetea wenyewe”. Mwisho watu wakaamuliwa kulipa deni na faini ya sh. 50000 juu kwa kuchelewa kulipa deni na huku hela walimpa Fadhili ambaye alikiwa kakaa nazo miezi 3.

Wengine ambao Pikipiki na bajaji zao ziliendelea kushikiliwa wakataka kuanza kuhoji kwa sauti, akawaambia “pigeni hizo kelele tuone zitawasaidia nini, maana hamna cha kunifanya”.

Kuna mengi ambayo yanaendelea kuhusu Afisa huyu, naomba LATRA Makao Makuu wajibu au waje wachunguze, huyo Fadhili ni nani hapo LATRA Morogoro? Kwa nini anakiburi kiasi hicho?

Kwa nini anachukua fedha za madereva Bajaji na kuchikichia nazo kisha anawatia matatizoni au anatumwa na wanaomsimamia?

Uchunguzi ufanyike na ili akibainika na matumizi mabaya ya madarka, hatua zichukuliwe haraka ili iwe fundisho kwa wengine.

Majibu ya LATRA ~ LATRA: Anayetuhumiwa kuchukua hela za Madereva Bajaj si Mtumishi wa LATRA ni Afisa wa Halmashauri ya Morogoro

Ufafanuzi wa tuhuma za rushwa katika utoaji leseni za LATRA kwa pikipiki (bajaji) Mkoa wa Morogoro
 
kuna watu watakuja hapa kukuponda kuwa unamsagia kunguni ndugu fadhili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…