POTOSHI Huyu aliyefua na kuanika nguo, je hapa ni daraja la Kijazi Ubungo?

POTOSHI Huyu aliyefua na kuanika nguo, je hapa ni daraja la Kijazi Ubungo?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
1779540780096.png
uy
 
Tunachokijua
Madai

Kumekuwapo na picha inayosambazwa mtandaoni ikionesha nguo zilizoanikwa sehemu yenye uwazi juu darajani na kuelezwa kuwa imepigwa daraja la Kijazi Ubungo.


Je, ni upi uhalisia?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejiridhisha kuwa tukio hilo katika picha ya daraja si halisi bali picha imehaririwa kwa Akili Unde. Mathalani kupitia Google Reverse Image Search inabainisha moja ya video ya tukio hilo ambayo imetengenezwa kwa AI.

Aidha muundo wa daraja hilo haufanani na Muundo wa daraja la Kijazi Ubungo ambalo umbo la nguzo zake ni duara tofauti na picha hiyo yenye umbo tofauti.

Uchambuzi wa picha unaonesha viashiria vya wazi kwamba imefanyiwa uhariri wa kidijitali:

Uchambuzi wa kidijitali unabainisha kuwa sehemu za picha hii zimehaririwa au kuzalishwa kwa kutumia zana za AI za Google.

Kutokuwiana kwa Muonekano: Kamba ya kutundikia nguo, televisheni, na baadhi ya vitu vya nyumbani vilivyowekwa kwenye uwazi wa zege chini ya daraja vinaonekana kuunganishwa isivyo kawaida na mazingira yanayovizunguka. Mwanga na vivuli vya vitu hivyo haviendani kwa uhalisia na vivuli vizito vinavyotokana na mihimili mikubwa ya zege juu yake.

Ingawa wakati mwingine watu hujisitiri katika maeneo yasiyo ya kawaida mijini, uwepo wa televisheni na kamba ya nguo iliyonyooka kikamilifu katika nafasi ya juu ndani ya muundo wa daraja linalotumika ni jambo lisilo la kawaida. Hii ni sifa inayojitokeza mara nyingi katika picha zilizotengenezwa kwa AI au picha zilizochanganywa kwa lengo la kuunda maudhui ya kushtua au kusambaa mtandaoni.​

screenshot-2026-05-25-111220-png.3594685
Back
Top Bottom