dada pole sana, ni kawaida yetu wanaume, huwa vigumu kumwacha mtu live sabu ya kukuzoea sana afu pia tunahofia ung'ang'anizi wenu kuuliza kwanini unaachwa na kulia lia kwenu wakati mwingine kulazimisha uambiwe sababu au usamehewe makosa usiachwe. Mambo mengine hayaelezeki. Kwa mfano mademu wengine mvaa vibaya na hamtaki kubadilika eti mmesoma mnaenda na wakati, pia wengine wavivu anakutembelea geto anataka kitandani tu hataki hata kufua au kuosha vyombo vya jamaa geto anaona noma. Jamaa anapima huyu vipi? majibu ya haraka ni kwamba tukioana utanifanya house boy au utataka housegeli atupikie na kutufulia. Wa nini wakati hatuna mtoto?
Sababu nyingine ni mademu wenyewe kujifanya modern wa western kuliko wazungu wenyewe kwenda kijijini kwetu Karatu au Kigoma hataki wala kujenga kijijini hamtaki mwataka mjini. sasa tukishawajua hivyo nasisi tunawaza huyu kwetu hatakubali kwenda mana kitanda chetu kijijini ni changa na mkeka, au nyumba yenyewe mbavu za mbwa na bati za kulaza maarufu 'slops' nyie mwaona ushamba nitakupeleka wapi na nyumba ya kupanga hadi lini?
Afu zaidi wengine hamjihangaishi kabisa na ujasiriamali, mkipata muda wa kupumzika ni saluni kuongeza kucha unarudi geto nikichelewa kurudi unaanza kutext honey vipi mboma wachelwe? mna kera nyie! hamjui tu.
Ushauri kwako kama hujatambua jamaa kishakumwaga kwa sababu nilizoeleza hapo juu.
1. Mtafute toka naye mahali tulivu kusiwe na kitanda, muulizane vipi mwenzangu mbona waniweka njia panda? umepata mwingine, mbembeleze akueleze kama bado ujue kuna jambo limemkera kwako hata sema kati ya hayo hapo juu.
2. Mwambie katika maisha yake alitarajia mke wake awe na sifa zipi. Akufafanulie kila sifa anayotaka nawe utafakari hizo unazo au wambabaisha tu mjini.
3. katika kumuliza ujue mazingira ya kwao yakoje na angetaka wewe uwe vipi.
4. kama bado anakupenda, nenda naye kwa wataalamu wa saikolojia kama mimi japo hutonipata, awashauri mapenzi yenu yana kosa nini na nini mfanye muyaboreshe.
5. Kuwa mbinifu katika uhusiano si kitandai tu mpaka hata namna ya kumpokea kila siku, namna ya kumshauri, punguza maswali wakati mtu kachoka, au wakati kula. anapokuwa na mawazo ona kama nawe wahusika mshauri.
6. mweleze mataraji yako kwake, kama mume ungetaka yeye aweje. kama haelekei usipoteze muda, wanaume huwa hatusema wazi kumbe tushamaliza penzi tunaogopa kukuumiza kusema wazi kuwa hunifai.
NOTE. mnapoelezana usionyeshe kupewa huruma wala usiwe mkali, jaribu kuwa wa kawaida, wala usijutie kumpoteza lakini mweleze madhara ya kuwa na wapenzi wengi atakuambukiza au utamwambukiza kwasababu hamjakuta muda hivyo kila mtu anahisia zake huo mda ni mrefu mno kama hajazoea kukaa zaidi ya mwezi bila wewe lazima kuna mahali kishenda kupooza nawe pia hivyo hivyo. kuweni wa wazi.
Asante dada na pole sana, Heri ya mwaka mpya.