DOKEZO Huyu anayejiita "Russia wa Bongo" anafanya udhalilishaji kupitia mtandaoni. Mamlaka mchukulie hatua

DOKEZO Huyu anayejiita "Russia wa Bongo" anafanya udhalilishaji kupitia mtandaoni. Mamlaka mchukulie hatua

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mafyangula

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2025
Posts
557
Reaction score
1,039
Katika siku za hivi karibuni, kumekuwa na ongezeko la baadhi ya vijana wanaojiita watengeneza maudhui ya mtandaoni, lakini njia wanazotumia si sahihi na zinakiuka maadili ya kijamii.

Mmoja wa mifano ni kijana anayezunguka mitaani akiwa amevaa miwani yenye kamera ya siri, kisha huwasimamisha watu bila ridhaa yao na kuanza kuwauliza maswali yanayogusa maisha yao binafsi. Kitendo hiki si tu kinakiuka faragha, bali pia kinaweza kuleta madhara makubwa kwa wahusika.

Katika tukio moja, kijana huyo alimdanganya msichana kwa kumshawishi kuwa kuna fursa ya kazi. Baada ya kuamini, msichana alimpeleka hadi nyumbani kwake, akampokea kwa ukarimu na hata kumpa chakula. Wakati msichana alipokwenda kuoga, kijana huyo alitoka nje na kuanza kusimulia tukio hilo kwa marafiki zake, jambo linaloonyesha wazi nia ya kudhalilisha na si kutengeneza maudhui yenye maana.

Link za huyo maudhui :

View: https://www.instagram.com/p/DV3CG20jGHJ/

View: https://www.instagram.com/p/DVsyESejAm-/

Vitendo vya aina hii vinaweza kuharibu maisha ya mtu. Fikiria kama mhusika ana familia, mume, au wazazi—athari zake zinaweza kuwa kubwa kijamii na kisaikolojia. Hii si burudani, bali ni unyanyasaji na uvunjaji wa haki za msingi za faragha.

Ni muhimu kwa mamlaka husika kuchukua hatua za haraka dhidi ya watu wanaotumia majukwaa ya mtandaoni vibaya.
 
Mimi sijambo, hofu na mashaka kwako uliye mbaaali sana rafiki 👋
Tunaomba ulifanyie kazi Waziri wetu mpendwa, lakini pia Muheshimiwa naomba uongeze nguvu kwenye haya maswala ya vibao Kata zilizojaa ushoga wa kila aina mitandaoni Taifa letu linaangamia vibaya sanaa.
Utakua sehemu ya kumbukumbu katika kuokoa kizazi chetu Muheshimiwa.🙏🙏
 
Sasa mbona na wewe unazidi kumtangaza? Tena mpaka umeweka na hizo clip za udhalilishaji!

Mfano mimi ndio kwanza namjua kwa kupitia huu uzi wako!

😅😅😅
Umempa neno
Mimi pia na nimeenda kuangalia na mengine kama alivyotaka iwe kwetu wadau wa humu tuende

Angeanza kwa kuandika kasaidia kwanza kwa ripoti hizo maana sio yote anaweka ni ya haya anadai..
 
Sasa mbona na wewe unazidi kumtangaza? Tena mpaka umeweka na hizo clip za udhalilishaji!

Mfano mimi ndio kwanza namjua kwa kupitia huu uzi wako!
Wana Jf wangesema Uzi huu ni upuuzi bila ushahidi wa picha na kaClip
 
Wana Jf wangesema Uzi huu ni upuuzi bila ushahidi wa picha na kaClip
Huwezi kuwaridhisha watu wote kwa kila jambo,alichokikemea mleta mada ndicho hicho hicho na yeye amehusika kukitangaza,

Si ajabu lengo la huu uzi wake wala halikua kukemea bali ni kupromote jambo hilo.
 
Nipo nipo, hata leo nimesalimiana na @mongi2026
Safi sana mh waziri hiv ndivyo inavyotakiwa unakuwa active kwa kila kero

Kuna mawazir wenzako walikuwa active humu kabla ya teuz baada ya teuZi hawataki kusikiliza kero humu wanatuona kama wapiga kelele na wenye husda na vyeo vyao
 
Back
Top Bottom