Huyu bibi enzi za usichana wake nadhani alikuwa kama tractor

matunduizi

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2018
Posts
7,968
Reaction score
19,368
Ni bibi Mzee
Kapinda mgongo na dental formula imebaki nusu.
Mvi kichwa Kizima.

Leo nimemfuatilia nimeshangaa

1: anafuga Kuku na kuwahudumia mwenyewe. Sio Kuku tu Bali hata mzinga na kanga. Anatotesha na kuvilea vifaranga mwenyewe bila msaada.

2: Anaamka asubuhi anafagia Nyumba nzima. Anafuta vumbi na kudeki.

3: Jioni anakimbia kanisani mazoezi ya kwaya kwa wakati na hachelewi.

4: Anajaza Maji kwenye matank na kuhakikisha choo na bafu ni visafi.

5: Anapata Muda wa kusoma kutanua ubongo. Vitabu mbalimbali.

6: Saambili anapata muda wa kuangalia Habari ili asiachwe nyuma.

7: Anapata Muda wa kupigia Simu watoto wake na wadau mbalimbali kusocialize.

8: Anaamka mapema SAA kumi na moja kuanzia siku.

9: Analimisha Mashamba na Bustani za mbogamboga.



Wako wapi mabinti wenye Viwango angalau vya bibi
 
Wacha mabinti, hata vidume hawajui hata kufuga kuku wapate kipato.
Sababu hapo watakwambia hawana ardhi.
 
Kuna tofauti kubwa sana kati ya kusoma na kuwa na akili nyingi. Kuna watu waliishia darasa la saba (7) tu kwa sababu ya umasikini
 
Bila picha ya bibi mkuu ni stori ya kufikirikaπŸ˜€πŸ˜€
Mkuu Picha nikiweka mtanidukua
. kuna wengi wanamfahamu na nawajua wamo jf humu.

Ila ni kweli na Leo nilikuwa naye, yule bibi ni mshkaji wangu.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
 
Mkuu Picha nikiweka mtanidukua
. kuna wengi wanamfahamu na nawajua wamo jf humu.

Ila ni kweli na Leo nilikuwa naye, yule bibi ni mshkaji wangu.
πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€
Basi wewe nimeshakujua tayari kumbe ndio matunduizi.
 
Basi wewe nimeshakujua tayari kumbe ndio matunduizi.
Hahahaha
Matunduizi ni jina nililojitungia Mimi hakuna anayeniita popote.

Watu wacjukue ujumbe waachane na mambo ya clip. Hii sio siasa
 
Bila picha hatukubali
 
Sio lazima kila mtu afuge kuku shekhe, kila mtu afanye kitu kutokana na Hobie yake
'Hobby' ya wanaolalamika hawana kazi , maisha yanawapiga ni nini? Kufuga kuku nimetolea mfano, kuliko kuaibika huna hela ya kula 'hobby' ya kufuga kuku au kulima mchicha haiwezi kusaidia?
Kama 'hobby' zingekuwa zinaingiza kipato,, dunia ingekuwa peponi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…