Huyu binti ana nini? Hebu nisaidieni jamani

Huyu binti ana nini? Hebu nisaidieni jamani

1. Mpeleke hosp kitendo cha Afya ya Njia ya mkojo watamtibu vzr na atakua ok.

2. Mjengee saikolojia ya kujiamini. Angalia michezo anayocheza kila siku, anatumia vinywaji/vyakula gani hasa na rafiki zake, muhoji huota nini.

3. Hakikisha analala mapema akiwa amekojoa, then usiku aamshwe akakojoe.

4. Asinywe maji wala kimiminika kingine usiku. Mpen dry food (japo yaezapelekea constipation japo inasaidia).

5. Msimchape na mnapomkaripia mtumie lugha isiyoudhi.

She gonna be ok, ni stage tu!
Hayo yote akienda ugenini hakuna atakaye yafanya hivyo ataishia kudharirika tu.

Suluhisho la kudumu aende maduka ya dawa za asili wakampe dawa.
 
Nina mwanangu wa kike mwenye umri kama wa miaka 12 hivi. Ana matatizo mawili ambayo nimeshindwa kupata ufumbuzi wake ndio maana nikaamua kuleta huu uzi hapa ili muweze kunishauri.

Tatizo la kwanza ni kwamba binti huyo anakojoa sana kitandani kwa hivi sasa licha ya umri huo alionao. Mwanzoni wakati alipokuwa mdogo hakuwa hivyo ila kadri anavyozidi kukua tatizo linaongezeka. Huu unaweza kuwa ni ugonjwa? Na kama ni ugonjwa tiba yake ni nini?

Tatizo la pili ni kwamba kwa kuwa binti ni kikojozi, basi amekuwa akiamshwa mara kwa mara usiku ili ajisaidie ingawa hiyo haijasaidia. Hata hivyo anapoamshwa, anakuwa kama mtu mlevi au aliyepoteza kumbukumbu.

Anaweza akazunguka nyumba nzima na kufungua milango yote akitafuta choo kilipo. Akishindwa anatoka hadi nje na ikishindikana kabisa atazunguka hadi anajikojolea.

Anakuwa kama yuko ndotoni hivi. Hii pia inaweza kuwa nini? Naombeni msaada wenu.
Tuwasiliane mkuu mimi ni expert wa hao watoto wenye matatizo hayo.
 
Back
Top Bottom