Huyu Brigedia Warioba aliyeteuliwa na Rais Kenyatta ana uhusiano gani na Jaji Warioba?

Huyu Brigedia Warioba aliyeteuliwa na Rais Kenyatta ana uhusiano gani na Jaji Warioba?

tang'ana

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2015
Posts
11,931
Reaction score
15,849
Raisi Kenyatta wa Kenya amemteua mtu anaeitwa Bridgedia General John Kibaso Warioba kuwa mkuu wa jeshi la Magereza la kenya.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya huyo Bridgedia Warioba na jaji warioba wa Tanzania?

Screenshot_20211117-172037_Instagram.jpg
 
Mwingiliano wa majina tu kama utakavyomkuta lymo wa kenya na wa Tz!
 
Raisi Kenyatta wa Kenya amemteua mtu anaeitwa Bridgedia General John Kibaso Warioba kuwa mkuu wa jeshi la Magereza la kenya.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya huyo Bridgedia Warioba na jaji warioba wa Tanzania?

View attachment 2014217
Ukiwa mkoani Mara utajua kuwa wakurya walioko mkoani Mara kama vile Tarime, Bunda na Serengeti na walio Esebania wote ni wakurya. Ni sawa na wamasai walio Tanzania na wamasai walio Kenya wote ni wamasai.

Ukisikia jina Wariaoba kwa kabila la jamii ya wakurya ni sawa na jina Makame kwa Zanzibar, Mombasa au Kenya.

Ukisiakia jina Warioba ni sawa na Masanja, Mabula, Maganga, Mayala, Kabula, Soko, Nyanjige usukumani; sio akina Warioba wote ni wanatoka ukoo mmoja, ni majina tu.

Hata Tanzania tuna Naibu (W) anaitwa Waitara, kule Tarime wako akina Waiatara wengi sana akiwamo Gen. Waitara na hawana vinasaba vya ukoo kabisa.
 
Raisi Kenyatta wa Kenya amemteua mtu anaeitwa Bridgedia General John Kibaso Warioba kuwa mkuu wa jeshi la Magereza la kenya.

Je, kuna uhusiano wowote kati ya huyo Bridgedia Warioba na jaji warioba wa Tanzania?

View attachment 2014217
Hawana uhusiano wowote kwa sababu huyu brigadier General John Warioba ni wa kabila la mkuria wa nchini Kenya na Josef Warioba ni wa kabila la kiikizu linalopatikana Mara Tanzania.
 
Warioba ni majina ya wabantu na sio wajaluo. Ila unaweza kukuta mjalio analo hilo jina usishangae ni kwa sababu ya muingiliano wa jamii kama kuoana na nk.

Mfano, mama ni mkurya ama mzanani ama muikizu baba mjaluo, mama anaeitwa Prisca Warioba anaweza kuzaa na mjaluo anaeitwa Ondieki Onditi halafu wakapata mtoto wa kiume/ kike kwa sababu jamii ya wakurya wanaweza kuita jina la kiume kwa mtoto wa kike na kinyume chake pia. Huyo mtoto akaitwa Warioba, baba wa mwanamke.

So utakuta damu ya kijaluo ila jina la kikurya ama jamii ya wakurya hao wazanani, waikizu, nk wanaoishi mkoa wa mara na ndugu zao walioko upande wa Kenya.

Ila jina warioba perse ni la hizo jamii maana warioba ni mtu aliezaliwa wakati jua limewaka, rioba ni jua, hivyo warioba-mtu wa jua, mtu aliezaliwa wakati jua limewaka sana.
 
Hongera sana kwake....majina yako pande zote tu ....
 
Back
Top Bottom