Warioba ni majina ya wabantu na sio wajaluo. Ila unaweza kukuta mjalio analo hilo jina usishangae ni kwa sababu ya muingiliano wa jamii kama kuoana na nk.
Mfano, mama ni mkurya ama mzanani ama muikizu baba mjaluo, mama anaeitwa Prisca Warioba anaweza kuzaa na mjaluo anaeitwa Ondieki Onditi halafu wakapata mtoto wa kiume/ kike kwa sababu jamii ya wakurya wanaweza kuita jina la kiume kwa mtoto wa kike na kinyume chake pia. Huyo mtoto akaitwa Warioba, baba wa mwanamke.
So utakuta damu ya kijaluo ila jina la kikurya ama jamii ya wakurya hao wazanani, waikizu, nk wanaoishi mkoa wa mara na ndugu zao walioko upande wa Kenya.
Ila jina warioba perse ni la hizo jamii maana warioba ni mtu aliezaliwa wakati jua limewaka, rioba ni jua, hivyo warioba-mtu wa jua, mtu aliezaliwa wakati jua limewaka sana.