Kafanyaje?
📌Kwa wachezaji wa kibongo wote wazuri wakiwa na hizi timu za mid table kushuka chini kwa sababu wanacheza kila siku. Ni wachache sana wanao weza kumaintain kiwango chao wanapokwenda Simba au Yanga. Wakifika kwenye hizi timu kubwa muda wa kucheza ni mdogo changanya na "pressure" za mashabiki. Akipata nafasi mara moja na ikitokea akakosea akazomewa au akakutana na mjadala unaomponda mitandaoni au kwenye zile redio zetu pendwa ndio basi kashapotea huyo.
Kibaya unakuta hawajaandaliwa watu wa saikolojia kuwapa somo. Mameneja wao mimi nawaita madalali tu wakishapokea chao basi mchezaji anaachwa ajipambanie mwenyewe. Hili tatizo lipo miaka yote na watu huwa hawalioni kabisa. Ndio maana kila mwaka Simba na Yanga zinasajili hawa vijana wa kitanzania wengi lakini utakuta ni mmoja au wawili wanaowika wanaobaki wote wanatolewa kwa mkopo au kuachwa kabisa.
Na cha kusikitisha zaidi wengi wao wakishaachwa Simba au Yanga na kiwango ndio kinaporomoka zaidi hata kurudi kwenye kiwango walichokuwa nacho kabla ya kusajiliwa Simba au Yanga kinakuwa mtihani.
Ombi langu kwenu wapenda soka hawa vijana badala ya kuwalaumu na luwazodoa tuwape moyo kwani wengi wao ahawajapita kwenye mifumoi sahihi ya soka hivyo tukiwapa changamoto na sisi tunakuwa ni sehemu ya kuwamaliza. Na hao mameneja toeni hela kidiogo kwa watu wa saikolojia ili angalau wajiandae kwa changamoto wanazoenda kukumbana nazo kwenye vilabu vikubwa.
Umemaliza Kila kitu Mkuu.Lakini tunapowalaumu mameneja, watangazaji wa michezo wa hizi fm redio mimi napenda kuwaita wapiga kelele wakati mwingine nao wachezaji vijana ni wa kalaumiwa. Mchezaji kijana anatakiwa awe na malengo asiwe na papara na awe na maamamuzi binafsi ya maisha yake ya soka ya baadae. Kwa nini wanashindwa kumuiga Kelvin John aliyezikataa Simba na Yanga.
Mfano mmoja mdogo tu ni kwa Chasambi kuwakilisha wachezaji vijana wa Tanzania. Alisajiliwa Simba akapata nafasi akaonyesha kiwango kikubwa sana baada ya kuaminiwa na Mgunda. Baadae wamekuja makocha wengine wameua kipaji chake. Kwangu mimi nilitegemea kabisa baada ya kutokea nafasi ya yeye kuondoka Simba; angechagua hata kwa mshahara mdogo amfuate Mgunda ili akafufue kiwango chake maana kati yao wanajuana vizuri. Lakini sijui ni utoto akachagua kwenda kujimaliza tena Singida kwa kuangalia zaidi pesa ndefu. Nina hakika angeenda kwa Mgunda angepata muda mwingi wa kucheza na kiwango chake kingepanda upya na kumpa nafasi ndani ya miaka miwli ijayo achague pa kwenda akiwa tayari mchezaji mkubwa.
Mnawatetea sana ndo maana wanakua wajinga miaka yoteKwa wachezaji wa kibongo wote wazuri wakiwa na hizi timu za mid table kushuka chini kwa sababu wanacheza kila siku. Ni wachache sana wanao weza kumaintain kiwango chao wanapokwenda Simba au Yanga. Wakifika kwenye hizi timu kubwa muda wa kucheza ni mdogo changanya na "pressure" za mashabiki. Akipata nafasi mara moja na ikitokea akakosea akazomewa au akakutana na mjadala unaomponda mitandaoni au kwenye zile redio zetu pendwa ndio basi kashapotea huyo.
Kibaya unakuta hawajaandaliwa watu wa saikolojia kuwapa somo. Mameneja wao mimi nawaita madalali tu wakishapokea chao basi mchezaji anaachwa ajipambanie mwenyewe. Hili tatizo lipo miaka yote na watu huwa hawalioni kabisa. Ndio maana kila mwaka Simba na Yanga zinasajili hawa vijana wa kitanzania wengi lakini utakuta ni mmoja au wawili wanaowika wanaobaki wote wanatolewa kwa mkopo au kuachwa kabisa.
Na cha kusikitisha zaidi wengi wao wakishaachwa Simba au Yanga na kiwango ndio kinaporomoka zaidi hata kurudi kwenye kiwango walichokuwa nacho kabla ya kusajiliwa Simba au Yanga kinakuwa mtihani.
Ombi langu kwenu wapenda soka hawa vijana badala ya kuwalaumu na luwazodoa tuwape moyo kwani wengi wao ahawajapita kwenye mifumoi sahihi ya soka hivyo tukiwapa changamoto na sisi tunakuwa ni sehemu ya kuwamaliza. Na hao mameneja toeni hela kidiogo kwa watu wa saikolojia ili angalau wajiandae kwa changamoto wanazoenda kukumbana nazo kwenye vilabu vikubwa.
Tusipowatetea sisi awatetee nani wakati hata viongozi wa hizi timu kubwa nao wanaona vijana wanakandamizwa na hawawasaidii. Badala yake wamegeuza ndio miradi yao. Kila mwaka wanawasajili na msimu unaofuata wanawaacha. Mfano mzuri ni Chasamabi na Chikola wana vipaji vikubwa na wamedhihirisha hilo lakini leo hii wapo wapi.Mnawatetea sana ndo maana wanakua wajinga miaka yote
Mpira ni kaz na inahitaj juhud sio ushaur nasaha kama wagonjwa wa ukimwi
Intrinsic motivation karibia asilimia 98.9 ya waafrika wote hatuna
Bado kijana, kipaji anacho apewe muda. Tunapenda kuwakatia tamaa hawa vijana sababu ya kuwalinganisha na akina Kangwanda. Huyu mtoto boli lipoUsajili wa ovyo. Huyu Chuga Boy hata Namungo hana nafasi ya kuanza