Huyu dada, hawezi kunipa limbwata kweli?

Mkuu, umenitisha sana. Kuna siku alikuwa anapiga safari kwenda field, kabla ya kwenda huko akaenda kwa mtaalamu wake kwa tiba. Aliporudi jioni, akanitafuta tukawa tunapiga bia, katika mazungumzo akaniambia hatonipa penzi mpaka siku tatu zipite, kwa sababu mtaalamu alimzuia, ili tiba ifanye kazi. Kwa hiyo kuna uwezekano walishanipiga chapo...Nami nataka nimkimbie kabla haijawa jioni
Kama bado unajitambua hujalimwa mzee baba
 
Kifupi nakupa tu pole maana kazi ya limbwata ni kumfanya mtu amtii mwenzake,sasa wewe tayari una hofu na hujui ufanye nini,hapo kaa kwa kutulia dawa iingie vizuri.
Angekuwa hajakupiga limbwata wewe mwenyewe baada ya kuona humuelewi na hayo mambo yake ungefanya maamuzi ila kwa sasa huna jeuri ya kufanya maamuzi yoyote juu ya mahusiano yenu.
 
Wakuu habari?

Mnavyojua tena, wanaume tumeumbwa kutamani na kupenda; hivi karibuni niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja anafanya biashara ya kununua madini mkoa mmojawapo huko kanda ya ziwa.

Huyo dada nilimpenda kutokana na uchangamfu wake, na uhusiano wetu ulianzia club moja, nilipoenda kupumzisha akili. Ndipo nilipomuona, na kumpatia namba yangu ili aweze kunitafuta. Na kweli alinitafuta, na mahusiano yakawa moto moto.

Mnavyojua tena, mimi huwa napenda kujifunza vitu kupitia watu mbalimbali; nikajaribu kumdadisi namna anavyofanya hiyo biashara, ili ikiwezekana na mimi huko mbeleni niweze kuifanya.

Katika majadiliano, ikaonekana huwa anajihusisha mara kwa mara na mambo ya uganga katika kujikinga na maadui mbalimbali katika hiyo biashara. Yaani yeye kwenda kwa mganga, ni sawa na muumini aliyeshika dini yake anavyoenda kusali siku ya jumapili au ijumaa.

Akiona mdudu yeyote, lazima awasiliane na mtaalamu wake ili kujua kama kuna usalama ama vipi.

Kinachonipa wasi wasi zaidi, jana tulikesha naye maeneo fulani ya mapumziko, akaniambia ana safari leo ya kwenda sehemu, lakini hiyo sehemu anayotaka kwenda inautata, na hawi muazi kuniambia anaenda kufanya nini.

Mbaya zaidi, alikuwa safari ya kama mwezi hivi, ambapo mawasiliano mimi naye yalikuwa yanasua sua hasa kwa upande wangu, nilikuwa simtafuti mara kwa mara.

Kutokumtafuta ikawa ni sehemu ya ajenda; kwa nini nilikuwa nafanya hivyo, au kuna mchepuko mwingine? Nikajaribu kujitetea hapa na pale, lakini likawa limeisha kwa shingo upande.

Hofu yangu; hii safari ambayo ameenda leo, inawezekana anaenda kushughulikia biashara zake, lakini na wasi wasi pia, anaweza kunipiga limbwata nikawa sina jeuri kwake.

Wakuu, nifanyeje ili nikimbie hichi kifungo kinachokuja mbele yangu?
Mtego wa panya hunasa wanaohusika na wasiohusika.
All the best katika maisha yako mapya ya kuwa kwenye limbwata
 
Mtu anaye kwenda kwa waganga ni mchawi mchawi!

Kwa hiyo unategemea nini kutoka kwa mchawi? Ukiamua kuingia kwenye mahusiano na mchawi jiandae kwa kila kitu ni lazima utarogwa tuu!

Ukitaka kujiokoa wewe ni kuvunja hayo mahusiano kabisa kinyume na hapo swala la kupewa limbwata au kufanywa zezete litegemee kabisa na watakao sumbuka ni ndugu zako.
 
Watanzania bwana ajiombee vp wakati ana zini na mtu asiye mkewe, ni mungu yupi atamlinda na uchafu anaofanya. Sema akajikinge kwa waganga alilogwe[emoji3][emoji3][emoji3]
Ahahah atubu aachane na mambo ya dunia amrudie muumba wake,kwenda kwa waganga simshauri kabisaaaaaa.

Dawa ni moja tu maombi.
 
Wafanyabiashara ya madini lazima ujizindike otherwise hutapata kitu so hao ndo walivyo kuwa na aman hawez kukuroga

Sisi wakurya hatuoi mwanamke anayetokea
Migodoni
Majini(sehem zenye uvuvi)

Kwa sababu watu wanaotoka hizo sehem waganga kwao ni kama kwenda kanisan tu
 
Wakuu habari?

Mnavyojua tena, wanaume tumeumbwa kutamani na kupenda; hivi karibuni niliingia kwenye mahusiano na dada mmoja anafanya biashara ya kununua madini mkoa mmojawapo huko kanda ya ziwa.

Huyo dada nilimpenda kutokana na uchangamfu wake, na uhusiano wetu ulianzia club moja, nilipoenda kupumzisha akili. Ndipo nilipomuona, na kumpatia namba yangu ili aweze kunitafuta. Na kweli alinitafuta, na mahusiano yakawa moto moto.

Mnavyojua tena, mimi huwa napenda kujifunza vitu kupitia watu mbalimbali; nikajaribu kumdadisi namna anavyofanya hiyo biashara, ili ikiwezekana na mimi huko mbeleni niweze kuifanya.

Katika majadiliano, ikaonekana huwa anajihusisha mara kwa mara na mambo ya uganga katika kujikinga na maadui mbalimbali katika hiyo biashara. Yaani yeye kwenda kwa mganga, ni sawa na muumini aliyeshika dini yake anavyoenda kusali siku ya jumapili au ijumaa.

Akiona mdudu yeyote, lazima awasiliane na mtaalamu wake ili kujua kama kuna usalama ama vipi.

Kinachonipa wasi wasi zaidi, jana tulikesha naye maeneo fulani ya mapumziko, akaniambia ana safari leo ya kwenda sehemu, lakini hiyo sehemu anayotaka kwenda inautata, na hawi muazi kuniambia anaenda kufanya nini.

Mbaya zaidi, alikuwa safari ya kama mwezi hivi, ambapo mawasiliano mimi naye yalikuwa yanasua sua hasa kwa upande wangu, nilikuwa simtafuti mara kwa mara.

Kutokumtafuta ikawa ni sehemu ya ajenda; kwa nini nilikuwa nafanya hivyo, au kuna mchepuko mwingine? Nikajaribu kujitetea hapa na pale, lakini likawa limeisha kwa shingo upande.

Hofu yangu; hii safari ambayo ameenda leo, inawezekana anaenda kushughulikia biashara zake, lakini na wasi wasi pia, anaweza kunipiga limbwata nikawa sina jeuri kwake.

Wakuu, nifanyeje ili nikimbie hichi kifungo kinachokuja mbele yangu?
Rudi kwenu haraka ila ukiendelea kubaki hapo hutoboi huyo anakupiga limbwata sio la kitoto na akija kukuchoka tu anakugeuza msukule
 
Mkuu asikushuulishe huyo ww piga Vizuri tu ila huyo kuwa mke hafai nasema hafai anaweza kutoa kafara watoto huyo ohoooo usiseme sjakwambia Ila hayo mengine unajitisha hakikisha hakupikii kitu, kinywaji fungua mwenyewe , asije kukuomba nguo au kucha, au hata nywele Zako.

Wazee wapwani tunasema uchawi unataka link naww ndo ukudhuru haswa wamapenzi apate nguo, nywele, kucha, akuwekee kitu kwenye kinywaji, chakula au kwenye kitu ukipendacho[emoji3][emoji3][emoji1787] hapo SASA ndo kwenye issue Ila we piga tuu.
 
Back
Top Bottom