Wasalam,
Imebidi niingie kwanza Restraurant moja niagize Sharubati moja baridi na Maridhawa kupooza koo huku nikicharaza keybord za simu yangu kwa ajili ya huu uzi
kutokana na Mchomo wa jua ukiongeza tukio lililonikumba punde kutoka kwa Huyu Bidada umri 23-27
Nmejitazama kwenye kioo mara tatu tatu hapa Katika choo cha restra lakini , sijajitanabahi kama niko katika muonekano wowote wa kutilia shaka, wasiwasi au chenye kufanana na hicho.
Nilikuwa town juu ya leo ni weekend nikijaribu kutafuta , vijimalighafi kadhaa vya kuweka ghetto maana katikati ya week ni bize na kazi.
Wakati nakatiza viunga flani hapa tow, mbele yangu alikuwa bidada mmoja ,alivalia juu t-shirt nyeupe na suruali ya Bluu iliyomkaa vyemaa kutokana na umbo lake.
Lakini binafsi sikuwa na wazo lolote kumhusu yeye, huku macho yangu yakiwa bize kubarizi katika maduka tofauti tofauti kutazama bidhaa ambayo ingenivutia ili niweze kuisogea nayo ghetto.
Wakati huu bidada yule alikuwa akielekea katika muelekeo ambao hata mimi nlikuwa nikijongea kwayo.
Baada ya kama mwendo wa dakika 2 au au 3. Pasi na kuzidi hapo.
Hapo yeye akageuka nyuma macho yakagongana pengine alishageuka mara tele lakini kutokana na ubize wa macho yangu sikulitambua hilo mpaka mara hii ambapo macho yaligongana, akatembea kidogo na kugeuka tena tukatazamana tena.
Hamaad ghafla mwenzangu akaushika mkoba wake vyemaa tena kwa mkazo , na kuanza kuchakata mwendo kwa haraka zaidi. Huku akiwa na wajihi wa wasiwasi dhidi yangu. Akaharakisha kutokomea mbele akionesha kila dalili ya kunikwepa.
Nlijihisi isivyopendeza, nikajitazama mara mbilimbili pengine nina muonekano wa kiharamia lakini ubongo wangu haukubahatika kugundua hilo, hatua zangu si za pupa wala si za kukata, sijavalia kihuni. Hata mpangilio wa nywele na sharafa zangu kinyozi aliutendea haki, sionekani kama kibaka au mwenye kufanana kama wao.
Nlitamani nimsimamishe na kumwambia mimi ni kijana mstaarabu ninyefanya kazi tena yenye vijisenti kadhaa mwisho wa mwezi ambavyo havileti tamaa hata ya kuiba visivyo vyangu, lakini hilo nalo halikubahatika kutokea.
Kibaya zaidi mchana kweupe na watu wakiwam katika mtaa.
Huyu dada kanichukulia vipi
Nmeingia hapa restra nikipata sharubati huku nikijitafakari[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]