Huyu dogo kanishangaza sana, hata mimi nilikuwa hivi ila yeye kazidi

Huyu dogo kanishangaza sana, hata mimi nilikuwa hivi ila yeye kazidi

Naamini inawezekana. Kutokana na yeye kukaa nao kwa muda mrefu Basi amezoea sifa ya kila ng'ombe kuanzia rangi yake mpaka tabia zake. Maana hata hayo majina yao lazima tu yanaakisi sifa/tabia zao. Nikiwa nasoma nilikuwa na uwezo wa kufahamu wanafunzi shule yote kwa majina yao. Hii pia imenifanya nikumbuke nikiwa O-level mkuu wangu wa shule alikuwa ni mhindi, amefika hapo shuleni hata hajamaliza wiki, unaokutana naye njiani anakusalimia kwa kutaja jina lako pasipo hata wewe kumtajia jina lako.
Kuona kitu na kukitambua jina lake ni rahisi sana.
Huyo mwalimu wenu alikuwa akiona mwanafunzi ndio anakumbuka jina lake lakini pengine mkiwa darasani unaweza ukawa haupo na asigundue kwamba haupo kama wewe sio msumbufu darasani, au unakaaga siti ya mbele, unajibugi maswali, au unakaaga nyuma au sifa nyingine yoyote inayokutofautisha na wengine na yupo interested kukufuatilia kuliko wanafunzi wengine.

Okay tufanye hivi. Yawezekana wewe unajua wasanii /waimbaji wengi sana kwa majina na sura.
Lakini leo hii nikikuambia andika majina yao kwenye karatasi unaweza usifikishe hata kumi. Lakini nikimsimamisha mbele yako ndio unakumbuka oooh huyu ni Alikiba. Kwahiyo mkuu kuona kitu na kujua jina lake ni tofauti kabisa na kukumbuka kitu fulani sijakiona leo kama hicho kitu hakina sifa za ziada.
 
Mapema wiki hii nilikuja kijijini kuwaona wazee huku Bariadi, sasa siku ya Jana asubuhi nilitoka na mzee tukaenda mjini,tulirudi mida ya jioni saa kumi na mbili,ule muda mifugo inarejeshwa nyumbani toka machungani.

Aisee tumekaa pale tumetulia ng'ombe wakiwa wanaingia zizini kuna dogo ana umri wa miaka kumi na mbili (mtoto wa dada) anakaa pale home, wakati ng'ombe wanaingia zizini yeye anawacheki kwa makini sana,mwishoni kabisa akaja pale tulipokuwa tumekaa akasema uncle kuna ng'ombe watatu hawapo kwenye kundi lote hili,akawataja kwa majina wale ng'ombe waliomiss,kweli walipohakiki hawakuwepo,na walipoenda kutafutwa porini walipatikana.

Kilichonishangaza ni kwamba huyu dogo anawafahamu ng'ombe 860 kwa majina (kuna ng'ombe wengine wana majina ya viongozi),nilitaka anifundishe majina ya ng'ombe wote,alianza kunionesha na kuwataja majina alipofikisha ng'ombe mia nikamwambia inatosha,nilielezwa kuwa yule dogo katika kundi lote la ng'ombe wa babu yake ndiyo pekee anaweza kunotice kwa haraka sana kama kuna ng'ombe hata mmoja atamiss,nilishangaa sana ule uwezo wake,nikawaza huyu atakuja kuwa Kiduku LILO
KAMA HII SIO CHAI....Mzee auze Ng'ombe hata 10 tu, dogo apelekwe GRAIYAKI-Mara.
 
KAMA HII SIO CHAI....Mzee auze Ng'ombe hata 10 tu, dogo apelekwe GRAIYAKI-Mara.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mkuu katafute vitafunwaaa tuu[emoji119][emoji119][emoji119] Sukari imekolea vizuri ng'ombe 800 sio mchezooo
 
Mapema wiki hii nilikuja kijijini kuwaona wazee huku Bariadi, sasa siku ya Jana asubuhi nilitoka na mzee tukaenda mjini,tulirudi mida ya jioni saa kumi na mbili,ule muda mifugo inarejeshwa nyumbani toka machungani.

Aisee tumekaa pale tumetulia ng'ombe wakiwa wanaingia zizini kuna dogo ana umri wa miaka kumi na mbili (mtoto wa dada) anakaa pale home, wakati ng'ombe wanaingia zizini yeye anawacheki kwa makini sana,mwishoni kabisa akaja pale tulipokuwa tumekaa akasema uncle kuna ng'ombe watatu hawapo kwenye kundi lote hili,akawataja kwa majina wale ng'ombe waliomiss,kweli walipohakiki hawakuwepo,na walipoenda kutafutwa porini walipatikana.

Kilichonishangaza ni kwamba huyu dogo anawafahamu ng'ombe 860 kwa majina (kuna ng'ombe wengine wana majina ya viongozi),nilitaka anifundishe majina ya ng'ombe wote,alianza kunionesha na kuwataja majina alipofikisha ng'ombe mia nikamwambia inatosha,nilielezwa kuwa yule dogo katika kundi lote la ng'ombe wa babu yake ndiyo pekee anaweza kunotice kwa haraka sana kama kuna ng'ombe hata mmoja atamiss,nilishangaa sana ule uwezo wake,nikawaza huyu atakuja kuwa Kiduku LILO
usirudie tena kumfananisha huyu dogo na wapuuzi flani wa humu.
 
Sio kawaida kichwa chake kina uwezo mkubwa wa kuprocess na kuhifadhi data zaidi yenu..ila kwakua amezaliwa bara la giza imebidi atumie kipaji chake kukariri ng'ombe wakati kwa wenzetu NASA na CIA wangepiga hodi mapema kujichukulia Asset yao
exactly,I was amazed na huyu dogo ana asili ya upole,unaweza ukakaa nae kama hujamsemesha akakaa kimya hata masaa matano,Mara kibao tu huwaga wanampiga wakidhani ana kiburi,,,,darasani hafanyi vizuri sana ila kwa mambo anayofanya kwa kujisimamia hata ukimpa kazi yuko safi
 
Sio kawaida kichwa chake kina uwezo mkubwa wa kuprocess na kuhifadhi data zaidi yenu..ila kwakua amezaliwa bara la giza imebidi atumie kipaji chake kukariri ng'ombe wakati kwa wenzetu NASA na CIA wangepiga hodi mapema kujichukulia Asset yao
Hamna mkuu NASA na CIA sio rahisi ila kuna organization yao inaitwa MENSA wangeshambeba huwa wanasomeshwas elimu yao binafsi na ni siri mno.
 
Hua siamini katika namba tatu.

Yaani mfano mtu aseme 'Basi akampiga ngumi ya kwanza, ya pili, ya tatu chali' au 'Nilivyomchunia nikakaa siku ya kwanza, ya pili, ya tatu mwenyewe akapiga'

Na hapo mifugo iliyokosekana mitatu au siyo? Hii stori ina chembechembe za uongo.
Utakuwa GENIUS MKUU au la!! Una OCD
Screenshot_2019-11-07-20-04-21.jpeg
 
"Ngombe wengine wana majina ya viongozi" We jamaa viongozi wa kijiji chenu hicho ni hawa wakulu wetuuu , sauti iko chini bado
 
Back
Top Bottom