Huyu fundi gari leo ilikuwa nifungwe kwa kuua kwa kukusudia

Huyu fundi gari leo ilikuwa nifungwe kwa kuua kwa kukusudia

Mafundi wengi wa Magari Bongo ni wababaishaji PERIOD!
 
🤣🤣🤣🤣🤣 hayo ni majibu ya kutiana wazimu halafu mwishowe watu muonane wabaya..... Kitu kinapita kelele anasema hakijazoea....😂😂😂 Hapo fundi anakujibu kirahisi kabisa hata mashaka.

Shule n nzur sana aisee,Kuna vijana hawana shule n mafundi ukimuulza ktu anakujbu ksenge yaan mpaka unawaza huyu mjinga ana akil kwel,mfano unaweza muulza Fundi kuwa hik ktu ulichofunga mbona knapga kelele,yeye anaweza kukujbu kuwa hakjazoea kkizoea ktatulia na uktafakar kwa akil ya kawaida unaona sio kwel
 
Nipo mkoa fulani gari yangu ilipata ajali nmeleta kwa fundi. Hapa niliambiwa ndio mtaalamu wa hizi gari ni Toyota Hilux D4 zenye speed 200. Ilipata rabsha kidogo ikabidi nilete kwa fundi akague kila kitu.

Gari imerekebishwa upande wa body mbele kidogo na chassis ilipinda hivyo ilibidi kushushwa engine inyooshwe. Imenyooshwa leo wanarudisha engine. Mimi nipo nafuatilia kwa ukaribu.

Fundi amefunga kila kitu namwona kwenye kopo kuna Bolts kama 8-10 hivi. Namuuliza umemaliza kila kitu kurudishia. Ananambia ndiyo. Basi nikainuka nikachukua lile kopo lenye bolts na kumuuliza "hizi bolts kwa nini zimebaki?"

Ananijibu "Hizo zilizidi Boss" hapa pembeni yangu kuna spana sijui nani alinishikisha mkononi nikakuta nmemrushia na yeye sijui nani alimkwepesha akaepa na kukimbia akipiga kelele.

Hapo akaja fundi mkuu nikamweleza situation ilivyo akaniomba radhi sana. Sasa ameamua engine ishushwe aipandishe aifunge yeye mwenyewe upya. Hataki tena kuwaachia madogo wake. Sasa nami nipo nao bega kwa bega maana huwa nikija garage nakuja nmevaa overall kabisa.

Nimewaza huyu fundi bwana mdogo ana akili kweli? Yaani bolts zote zilikuwa zimefungwa. Leo karudisha engine anasema zilikuwa zimezidi, bolts zimezidije, alizikuta pembeni ya engine?

Sasa imagine haupo. Unakuja unakabidhiwa gari bolts 8 hazijafungwa. Huu si wendawazimu, wehu, ukichaa, ubaradhuli, ubazazi, ufala, usengie wa mafundi? Wallah ile spana ingempata ningekuwa kwenye hard time sana.
Ajali nyingi za barabarani husababishwa na uzembe kama huo. Mtu unaamini umetoka kutatua tatizo, kumbe umeongeza tatizo. Pole sana mkuu kwa yaliyokukuta.
 
Ushakosa kazi ya mgambo kijana....unamkosaje kumlenga shabaha kizembe hivo
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]aiseee
 
Mie huwa sitoki hapo hadi gari ipone ka yupo bize namwambia akiwa free anicheki niende ili shuhuli iishe siku hyo hyo huwa hawanipendi hao jamaa
Mimi magonjwa ya kawaida au ku replace parts fundi wangu ameshazoea namuita home anakuja na kijana wake na mimi nakuwa nao mwanzo mwisho.
 
Back
Top Bottom