Jannatul Firdaus
JF-Expert Member
- Aug 4, 2026
- 446
- 1,113
Wazia dunia ambayo huna haja ya kununua LUKU, kuweka bando la umeme, wala kuvuta mawaya ya hatari juu ya paa la nyumba yako. Dunia ambayo unachomeka kifaa chako chochote hewani na kinapata umeme bila kulipia hata shilingi moja!
Hili halikuwa wazo la kusadikika au sinema ya Hollywood. Lilikuwa ni wazo la Nikola Tesla—mwanasayansi na mvumbuzi aliyebadilisha sura ya dunia.
Kabla ya wazo lake hili kubwa, Nikola Tesla tayari alikuwa ametengeneza vitu vilivyoshangaza ulimwengu:
Ndiye aliyegundua mfumo wa Umeme wa AC (Alternating Current) unaosafiri umbali mrefu na unaotumika kwenye nyumba na viwanda vyote duniani leo.
Aligundua misingi ya teknolojia ya Radio, Remote Control, Motors za Umeme, na hata taa za Neon.
Tesla alikuwa na uwezo wa kubuni na kufanyia majaribio mashine zote ndani ya kichwa chake kabla hata hajazichora kwenye karatasi. Lakini uvumbuzi wake mkubwa zaidi na wa hatari kwa matajiri ulikuwa unakuja.
Tesla aligundua kuwa angahewa na ardhi vina nishati kubwa mno inayoweza kubeba mawimbi ya umeme. Wazo lake lilikuwa jepesi lakini la kimapinduzi: Kurusha umeme kupitia hewani na ardhini bila kutumia waya wowote.
Mwaka 1901, katikati ya eneo la Long Island, New York, Tesla alianza utekelezaji wa mradi huu wa kihistoria. Alianza kujenga mnara mkubwa wa chuma wenye urefu wa ghorofa 18 uliokwenda kwa jina la Wardenclyffe Tower.
Plan yake ilikuwa:
Mnara huo urushe mawimbi ya nishati ya umeme angani na ardhini.
Mtu yeyote duniani—awe yuko kijijini Afrika, mjini Ulaya, au katikati ya bahari—ategee tu antena ndogo juu ya nyumba yake na kuanza kutumia umeme wa bure bila kikomo!
Ili kujenga mnara huo, Tesla alihitaji mtaji mkubwa. Alipata ufadhili kutoka kwa tajiri mkubwa zaidi wa benki nchini Marekani wakati huo, J.P. Morgan, aliyeweka zaidi ya Dola 150,000 (sawa na mabilioni ya leo).
Siku moja, J.P. Morgan alimhoji Tesla vizuri kuhusu jinsi mfumo huo utakavyoingiza faida. Tesla alipomweleza kwa furaha kuwa umeme huo utakuwa bure hewani na utawasaidia watu wote maskini duniani, J.P. Morgan alishtuka na kuuliza swali moja lililoua mradi huo papo hapo:
"Kama umeme unaruka hewani na kila mtu anaweza kuuchukua bure, sisi tutaweka wapi mita ya kumpima na kumtoza pesa mteja?"
Mara baada ya kugundua kuwa mradi wa Tesla ungeua biashara za mafuta, maliasili, na mawaya ya umeme za matajiri wenzake, J.P. Morgan:
Alisitisha kutoa fedha zote mara moja.
Alitumia ushawishi wake kuwashawishi wawekezaji wengine wote wasimpe Tesla hata shilingi moja.
Alimchonganisha Tesla kwenye vyombo vya habari na kuanza kumtangaza kama mwanasayansi aliyerukwa na akili.
Akiwa hana fedha za kumalizia mradi, mnara wa Wardenclyffe Tower ulitelekezwa. Wakati wa Vita vya Kwanza vya Dunia, serikali iliuamuru mnara huo ubomolewe na kuuzwa kama chuma chakavu ili kulipa madeni ya Tesla.
Tesla aliingia kwenye msongo mkubwa wa mawaso na umaskini wa kutisha. Alimaliza maisha yake akiwa peke yake kwenye chumba kidogo cha hoteli, akilishwa biskuti na maziwa na wasamaria wema, huku ndoto yake ya kuipa dunia umeme wa bure ikizikwa pamoja naye.