Huyu jamaa Bwana, yuko happy kama kawa

Bilioni walizoiba wakina Tibaijuika ni za walipa kodi sasa kawaida iko wapi hapo? Sasa kwa mfano hela zote za ESCROW na mikataba feki ni vipi itawafanya watu wafurahie Tanzania?

Wewe kweli nanga, nani kakwambia zile zilikuwa pesa za Umma? Tajiri wa kihaya alilipwa chake, na si pesa ya serikali. Kosa pale ni kuwa kwa nini watumishi wa umma walipokea pesa ambazo zilikuwa zina-undermine performance yao. Ni kosa la kimaadili tu, na sio criminal offence.

Kuhusu mikataba nani umeona ameshitakiwa mpaka sasa hivi?

Jitambue na elimika ili uweze kuwa na uwezo wa kutamka lenye ukweli na uhakika.
 
Wabongo bhana!
Siamini Kama Ni hapa hapa huyo mzee wa watu mlimsema vibaya hadi akatamani kumaliza muda wake wa uongozi mapema, Leo hii nyie nyie mliosema hafai mnatamani jamaa bado awe madarakani!!
Ila sishangai sana maana inafanana Na ile ya Lowasa Ni Fisadi lakini baada ya muda mkasema sio Fisadi!
 
huyu jamaa alikuwa anapata wapi pesa?


swissme
Mkuu usiulize alikuwa anapata wapi pesa...uliza alikuwa anatumiaje pesa?

Tanzania ina pesa sana tatizo zinafichwa Benki kuu wakati wanafunzi hawana mikopo, waliothirika na majanga hawajasaidika ipasavyo, madawa hospitalini.....dah!
 
Nimejikuta napata swali Mkuu....
Kwani huyu wa sasa ndie mwenye sifa zinazo shabihiana na hizo?
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hilo sijalisema mkuu, mimi nimeongelea sifa ambazo J.M Kikwete hana.
 
Awamu hii mtasema yote heeheehee huyu mkwere si ndio mlimsema dhaifu?? Sasa hivi mnaisoma namba wallah laadhim! Piga kazi Ngosha mpaka wahame nchi , heshima itarudi taraaatiibu.
 
Awamu hii mtasema yote heeheehee huyu mkwere si ndio mlimsema dhaifu?? Sasa hivi mnaisoma namba wallah laadhim! Piga kazi Ngosha mpaka wahame nchi , heshima itarudi taraaatiibu.
Heshima gani sasa wakati tunaelekea kuwa majini maana tushapitiliza ushetani,mm sikufichi mm na familia yangu wote tulimchagua ngosha na kumpigia kampeni kwa matumaini tele mpaka tuligombana na watu,,ila kwa muda huu mfupi sina hamu naye,,ukiniambia hata uchaguzi huu hapa bora kura nimpe rungwe,mm na familia yangu, tena ninaposema familia uelewe ni familia CCM haswa,kindakindaki ila kwa hili picha ,mwache amalize mwenyewe tu!
 
Sasa tatizo ni nini ?? Hapa ngosha ana mwaka 1 tu, wewe na familia yako mpeni hata miaka 3 kwanza ainyooshe nchi... There's light at the end of the tunnel.. akifikisha 10 years nchi itakua kama ughaibuni mtu unaishi kwa discipline ya maisha.mpe muda kidogo.
 
Nikiangalia kilichotokea Zanzibar, namuangalia mara mbilimbili sana huyu jamaa.
Kazi kwa kazi JPM ndo mpango mzima
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…