Mkuu Mwanakijiji.
Nakushukuru kwa hili chapisho, kuna kitu naamini ingawaje sina hakika kama wengine wanaliona hili.
MDAHALO WA WAGOMBEA URAISI. naamini kuwa mdahalo ukifanyika watanzania watapata nafasi nzuri sana ya kuwajua wagombea kwa undani zaidi na hasa uelewa wao juu ya matatizo ya taifa letu.
Kwa sasa CCM wameogopa tayari, Je nyie mlioko huko majuu hamwezi kutusaidia ukafanyika hata kama mgombea wa CCM hatakuwepo?
Naamini hii itakuwa karata nzuri sana kwa upinzani na hasa chadema kwa sababu ya uwezo wa Dk Slaa kuongea kwa kutumia takwimu. naamini uwezo wake wa kusoma na kupitia kila nyaraka inayohusu taifa letu utajidhihirisha kwa watanzania.
Tusaidieni.