Sharobaro la jf
JF-Expert Member
- Apr 23, 2020
- 237
- 325
Habari zenu wakuu poleni kwa miangaiko ya hapa na pale katika kutafuta chochote riziki ili kujikwamua kiuchumi
Nije kwenye mada, mimi nipo eneo x sasa ninapoishi nyumba yetu imepakana na nyumba fulani yaani pua na mdomo. Hapo kuna msichana mmoja tulisoma wote shule ya msingi ila baada ya hapo kila mtu akaachana na mwenzie maana mimi nilienda kusoma mkoani ila yeye sekondari alieendea pale pale hadi alipomaliza form4.
Sasa mazoea yameanza mwezi huu toka mda wote hatukuwa na mazoea zaidi tu ya salamu tu kama majirani, mimi nipo zangu mda huu elimu ya juu sana kuliko yeye ambae hakufanikiwa kuendelea na advance. Sasa toka nipo chuo kila nikirudi naona ananichangamkia ile mbaya kiasi cha kuanza kubadilishana namba na tukawa tunachati kama majirani
Wiki iliyopita akaniuliza upo home nikamjibu yeah, akasema nakuja nikwambie karibu, mda sio mda mtoto huyo, basi tukapiga stori mbili tatu, akasema eti simu yake inasumbua camera, sio kesi ikabidi niingie playstore nikamchukulia kamera kali ya sweet camera kiasi aliifurahia hiyo camera akaondoka, jioni akanitext ahsante sna nikamjibu usijari
Juzi tena akaniambia nakuja home hapo unitengenezee simu yangu nashindwa kuingia fb inagoma, nikamwambia haina shida, mara mtoto kaja kweli akaa ameakaa kwenye kochi alinikuta napika, nilikuwa naangalia muvi ya prison break mara mtoto anaanza kujiongelesha daah una muvi nzuri nimeipenda naomba niwe nakuja kuangalia muvi, nikamwambia usijali jirani jisikie upo nyumbani sisi ni majirani, akatabasamu basi baada ya kumtengenezea fb yake akaniaga huku akiniangalia kwa jicho la huba akaandoka
Jana mchana nipo nasikiliza nyimbo kwenye buffer ilikuwa ni nyimbo ya nandy one day, akanitext akaniambia naipenda hiyo nyimbo naomba irudie rudie, nikamjibu poa, kufupisha stori demu inaonekana kuna kitu anakificha sasa kwa mabaharia kama sisi tushajua kipi anakitaka ila tatizo ni moja
Mimi toka nigombane na demu wangu, tuna wiki ya pili nimejikuta sina mood ya kuwa na demu tena naweza kusema hata huyu ninaweza nikawa nae ila nikamuumiza bure na sitaki kitu kama hicho
Swali langu naombeni mbinu itakayokatisha mazoea na huyu jirani ili nimuokoe?