Huyu JK vipi???

Moja kati ya udhaifu mkubwa sana kwa kiongozi ni kutotekeleza anayoyasema, hii inaonyesha dharau kwa wale anaowaeleza maneno hayo.

Mbaya zaidi yeye mwenyewe anafahamu kuwa amesema mambo mengi na kuwaahidi watanzania lakini hakuna chochote anachofanya,
Dawa yake ni ndogo sana, 2010, pale tutakapo mwuliza maswali, yeye na wenzake wagombea ubunge 'mbona maneno yenu mengi mliyosema yamebaki kuwa hadidhi' hapo ndipo tutasikia kigugumizi na kazi ni moja tu piga wote Chini akina sisiemu.
 
Mi naona bora hata mzee wa ruksa kuliko huyu "HANDSOME BOY" Sijui hata anatupeleka wapi? Kesi ya mpambe wake ndo ilisaisha hivyo, uliona wapi muuaji tena kwa makusudi yuko nje kwa dhamana tena anapeta tu Dar-Tabora, anasafirisha zake asali bila hata wasiwasi.

Ila mi bado nayasubiri hayo maisha bora kwa kila Mtanzania, maybe 2009,manake kampeni zitakuwa zimekaribia.
 

Asante mzee mimi nilikuwa nimempa credit JK kwa kumaliza majambazi. Kumbe nayeye sasa anaanza kuzalisha majambazi. basi hana cha kujivunia.
 

Mzee nashukuru kwa updates. Basi nafikiri kuna haja za makusudi za kupiga kampeni za waziwazi kuhakikisha MR. JK anashindwa kwa kishindo kama alivyoshinda kwa kishindo.

Ikidhihirika kuwa hakufanya kitu na kuendelea kujichanganya kwa kutojua wananchi walikuwa wanategemea nini kwake, nafikiri itabidi tupige ndogondogo hata ndani ya CCM asipite katika mchujo wa kutafuta mgombea.

Lakini pia nafikiri kuna haja ya kuainisha failure zake balabala hili ziweze kutumika wakati wa uchaguzi mwaka 2010, hili hata yeye asije akalalamika pale misaafu itakapochomolewa.

Hizi kauli zake ikiwapo pia ya nguvu mpya kasi mpya itunzwe vizuri hili tuweze kupima kama kweli ameweza kufanikisha objective yake.
 
 

Ebana vipi mbona umenijia juu hivyo? Unataka kuanzisha shari na mimi au nimekuelewa vibaya? Hebu fafanua zaidi....
 

i wish huyu mkuu wetu wa idara ya utalii na bnez kwa mabiashara Tz angekua member wa JF naye ajadili nasi ili tujue hasa yuko pale kwenye jumba jeupe kwa minajili gan?as waTz hatuelewi
 
Mmh! yaani Chadema kina Dr. Slaa & Co. ni wakali na trend setters, yaani mpaka Raisi wa jamuhuri anawaiga staili yao ya kuwashitaki wabadhirifu kwa wananchi?
 
Rais Jakaya Kikwete amewataka Watanzania kutambua kuwa njia pekee itakayowakwamua kiuchumi na kuwaletea maisha bora ni kujishughulisha na shughuli mbalimbali za maendeleo na si kukaa tu vijiweni na kulalamika.

Kauli hiyo aliitoa jana wakati akijibu malalamiko ya wananchi wa kijiji cha Nyumba ya Mungu, kilichopo katika kata ya Lang`ata, tarafa Msitu wa Tembo, wilayani Simanjiro, ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara yake ya kikazi mkoani Manyara.
 
Mkuu nimekuelwa vizuri ila wewe kufikia uamuzi kwamba ni JF hapo you went out of line!Ina maana you mean JF ni Kijiwe?Hapa hatulalamiki kama JK anavyodai but we are providing solutions to some of the most pressing issues in our country ambazo zinahitaji solutions and pointing out the weaknesses of the govt and other people as well as how to bring them back on track!
 
Umejuaje amekusudia Jamii Forums ?

Sasa mwenye macho haambiwi tazama ,si unajua JF tupo mstari wa mbele kuzidumba kauli za Muungwana na maisha bora kwa kila Mtanzania ,hivi nani aliahidi kuwa atahakikisha kila Mtz anapata na kuishi katika maisha ya wastani.

Sasa kama yeye aliahidi inakuwaje leo arudi atuambie tusikae na kulalamikia ahadi zake ambazo hajazitekeleza,hivi ni nani aliahidi kupambana na rushwa,ni nani aliahidi maisha bora kwa kila Mtanzania ,ni nani aliahidi kutengeneza ajira au nafasi za kazi kwa mamilioni ,hivi huelewi kama Mheshimiwa anakengeuka ahadi zake ?

Hivi Muungwana hajui kama waTz wanasubiri hizo ajira ili waanze kuchapa kazi ? Sasa kusema tusikae vijiweni kupiga makelele kudai ziko wapi sera zake za kuwania Uchaguzi ndio imekuwa nongwa ?
JF ni kijiwe ambacho waTz wenye maoni mbali mbali hukutana na kupeana uwono kwa kina ,sasa ukisikia kijiwe sijui kwa akili yako inakufananishia na nini ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…