Naona umejaribu kutetea lakini cha ajabu kila mafanikio ulioyataja unakuwa mwepesi kukubali kwamba lakini.... kwa kiingereza 'but's na 'if's kibao!
Suala la majambazi inabidi nikatae! Hivi unasoma magzeti kweli? Hujasoma wikiendi hii majambazi walivyokuwa na field day! And FYI masuala ya ujambazi yalikithiri JK alipoingia madarakani siyo wakati wa BWM! Hata ishu ya akina Zombe ilikuwa enzi zake, so let's put the record straight! This was a power struggle among the police, nadhani kuna wachambuzi wenye information zaidi.
Suala la elimu - university, primary na secondary - enzi za danganya toto Bongo imekwisha! Wanalazimisha wananchi wajenge mashule na wanakomba misaada alafu tunasoma kila leo pesa za MMES na MMEM zimetafunwa, alafu watoto wanaenda shule na kujikuta na mwalimu moja. Then what happens? Panic! "Basi tuchukue ma-failure wa form four waende kufundisha watoto wetu" - ludicrous! Mungwana hana strategy katika elimu! Kaikuta imebaki from BWM era anaiendeleza it is not his initiatve, hili nalijua maana nliona mpango wa kuendeleza elimu. Walianza na MMES under BWM na next stage ilikuwa ni sekondari then baadaye vyuo. Siyo mafanikio yake JK!
Lakini thread hii haiko hapa kuchambua mafanikio ya JK, bali tunachojaribu kuelewa ni kwamba ana matatizo gani rais wetu? Maana it is without doubt kwamba mambo hayaendi kabisa Bongo. Sasa tunajaribu kuchambua psyche yake.
Look sisi kama raia wa Tanzania, in fact wapiga kura, tunampa mtu kura kuwa rais ili atende vitu fulani, sasa kusema anajitahidi and that he is training on the job for 2 years is WRONG!
Inaonyesha kwamba a) he is slow to understand maana miaka 2 bado tu! b) he understands but is incapable of action
Naomba: mwaka 2010 iwe mwaka wa mabadiliko jamani we cannot take more of the same!