Wazee walimuingilia na bango la kuoa, yalikuwa maswali lini itafika siku yako, jibu ni kuwa bado, sasa wazee nao wamechoka wamejiachia. Ikabidi sisi madada tumuulize wifi lini utatuonesha jibu ni vile vile nasi tukajiachia kuuliza direct question. Lakini sasa utata ni kuwa hana histori ya kuwa na mwanamke au hata being accompanied a woman except those close to him.
Yeye hata akiona dada mzuri au wa aina yeyote ni nutral, hakuna reaction, tukasema labda ni gay hata hao wa design hizo hatumwoni nao. Kuwa ni mlokole si wa hivyo kama ni mtu wa kila saa na neno la mungu, nikajaribu kumintroduce kwa huyo dada japokuwa mawasiliano yanaendelea lakini nothing more nothing less mazungumzo ni ya kawaida ya hali ya hewa, chadema na sensa no flirting au yale ya kiujanja janja wa kiume.
Nimekuja kuona aibu mimi mwenyewe kwa huyu mdada maana mpaka sasa yule kaka hailekei, Ok hana ulazima na huyu mtu wangu lakini atleast tujue yuko category gani maana hizi mbili za kuwa straight or gay hayuko, nikafikiri kuwa kutakuwa na namna ya tatu ambayo siifahamu.