Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Kaka Pekee

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2018
Posts
336
Reaction score
564
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
 
... huyu jamaa sijui ana tatizo gani. Mbona Jenerali Mabeyo tunapishana naye mitaa ya Segerea kila siku kikawaida kabisa bila wananchi kuwekwa pembeni au kugandishwa kwenye foleni. Anasahau kila mtu anawahi kwenye mihangaiko yake na sio yeye tu.
 
Cheo chake ni Chief of Staff, ni cheo cha pili kutoka brigedia general...kama ukifuatilia zaidi unaweza kulipata jina lake mahali fulani naamini
Kijeshi ni Luteni Jenerali (Lieutenant Geneal; 3-star General) just nyuma ya Mkuu wa Majeshi (Jenerali - 4-star General). Chief of Staff ni cheo cha utendaji ambacho anaweza akapewa kamanda mwingine yeyote mwenye cheo sawa cha kijeshi.
 
Mkuu mimi ni mzoefu Wa hiyo barabara tangu enzi za mkwere kila asubuhi na jioni lazima kunakuwa na ving'ora vya hawa wajomba na tulishazoea huo utaratibu, mkuu all in all heshimu mamlaka husika hasa hawa mabaka mabaka ukileta ujuaji mwingi hawakawii kukufundisha adabu mpaka uhame mji na kuwachukia milele, mbona misafara ya rais mnapigishwa foleni mpaka Masaa mawili hulalamiki?
 
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Hii ndio tatizo LA viongozi wengi wa Africa,hao walinzi wake huwa kama majambazi,kufokea watu,kama vile walichokibeba,ni kitu nyeeeti sana,
Mimi huwa najiuliza,kama wao ni wanajeshi waliobobea kwenye medani za kivita,kwanini wanakuwa na papara wanapokuwa wanamsindikiza kiongozi wao?kwanini wasikae kwenye foleni,kimya kimya,bila mbwembwe,wamlinde boss wao vzr,bila papala,maana wanachokifanya,huwa ni "Ku atract attention" kiasi kwamba kama kuna watu wabaya wanaweza kumdhuru boss wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom