Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Huyu Kamanda wa Jeshi anatukera sana wakazi wa Mbezi

Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Huyu afande kwanza anachelewa kazini, anapitaga tangi bovu around saa 1. Askari wale mbwembwe nyingi. Mara nyingi wanakuwa wrong lane na wanasababisha foleni upande ule unnecessarily

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cheo chake ni Chief of Staff, ni cheo cha pili kutoka brigedia general...kama ukifuatilia zaidi unaweza kulipata jina lake mahali fulani naamini
Sasa chief of staff ambaye hajali wenzake barabarani sijui anawajali vipi staff wake huko jeshini, alitakiwa awe mfano wa kuigwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani amekuambia kuzoea kwako kwa muda mrefu ndiyo sheria?
Mkuu mimi ni mzoefu Wa hiyo barabara tangu enzi za mkwere kila asubuhi na jioni lazima kunakuwa na ving'ora vya hawa wajomba na tulishazoea huo utaratibu, mkuu all in all heshimu mamlaka husika hasa hawa mabaka mabaka ukileta ujuaji mwingi hawakawii kukufundisha adabu mpaka uhame mji na kuwachukia milele, mbona misafara ya rais mnapigishwa foleni mpaka Masaa mawili hulalamiki?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu afande kwanza anachelewa kazini, anapitaga tangi bovu around saa 1. Askari wale mbwembwe nyingi. Mara nyingi wanakuwa wrong lane na wanasababisha foleni upande ule unnecessarily

Sent using Jamii Forums mobile app
Afadhali wewe unanielewa vyema ninachozungumzia Ndugu Yodoki!...nimeshuhudia wakimkalipia mama wa watu aliyekuwa kapigwa na bumbuwazi kuona wanatokea ghafla mbele yake wakimuelekea toka upande anapokwenda na Ki mtoto wa gari chake hadi nikamuonea huruma
 
Habari wana jamvi,

Kwa wale wakazi wenzangu wa Mbezi Beach, Kunduchi, Goba na watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kwa ujumla
bila shaka Mtakuwa mmekutana na huyu Kamanda wa Jeshi (Chief of Staff) ambaye kuanzia majira ya kila siku Asubuhi 12:30- 1:00 hutugandisha kwenye foleni kwa muda mrefu kila siku akisubiriwa kupita yeye na ma MPs wake wanaoning'inia kwenye milango bila sababu ya Msingi na wakati mwingine waki ning'inia na Bunduki na mavazi kama tuko Afghanistan...wakifokea watu barabarani kukaa pembeni tena wakiwa kwenye wrong Lane!

Binafsi ananikera sana, kama anahitajika kufika ofisini mapema si atoke mapema kama wengine...😡 au ndio Madaraka ya Kulevya?
Kuna siku niliwahi kuongozana na gari ya Waziri wa Ulinzi toka Uwanja wa ndege wa Dsm hadi hadi nilipofika Mwenge nao wakiwa kwenye foleni bila hamaki wala papara.

Hebu mfikishieni salamu huyu Kamanda, awaambie walinzi wake kuwa wastaarabu na kutotukera wananchi.
Mawaziri hawana mbwembwe siku hizi..namuana mara kibao Kingwangwala yupo kwelye foleni anatweet tu hana mbwembwe wala nini
 
Nchi ya viwonder

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Akashusha vioo kabisa na kukupungia.

Huu uongo first class.

Sent using Jamii Forums mobile app
sio uongo
mimi binafsi wakati nasoma Tambaza high school 2003 tulikuwa tunamuona CDF General george waitara na gari yake 4 star akiingia ngome kila siku hakuwa ma vingora wala mbwembe kama za siku hizi, tuliwahi kumpungia mkono na yeye akarudisha salamu.
mwaka huu nilikutanana chief of staff YH Mohamed dodoma anamsafara kama wa magari 5 na MP wa kutosha,tena barabarani kila kona ya dodoma Millitary police wanafanya kazi za trafiki polisi, nilibaki na duwaa ni kajisemea zama zimebadilika
 
Back
Top Bottom