Huyu kanichosha

Huyu kanichosha

Pole sana mkuu,ila itoshe kusema ukiona kwa mkeo leo ni matokeo ya ulichokitengeneza wewe mwenyewe mwanzo wa mahusiano yenu,kwa hakika yawezekana ulifanya kwa kujua au kutokujua ,ila ukweli ni kuwa pengine ulianza kwa kumdekeza kwa kumpa kila apendacho ikiwemo pesa,na yawezekana ulinyimwa unyumba na ukaishia kumbembeleza japo hukuwa na kosa na hivyo yeye akageuza fimbo ya kukuadhibu kwa kukunyima tendo kila atakapohisi umemkwaza,ulianza kwa kumuwekea wasaidizi wawili sasa kwa nini asishinde fb?
Hivyo nakushauri usimuache bali onesha misimamo kama mwanaume,maana ungekuwa na misimamo thabiti asingechukua pesa na kwenda kununua zawadi ya rafiki yake,jitathimini mkuu na uchukue hatua
 
Nikifikiria talaka huwa nafiriia watoto wangu wataishi maisha ya vipi bila Mimi nakuwa napata jibu LA msamaha!
 
Pole sana mkuu,ila itoshe kusema ukiona kwa mkeo leo ni matokeo ya ulichokitengeneza wewe mwenyewe mwanzo wa mahusiano yenu,kwa hakika yawezekana ulifanya kwa kujua au kutokujua ,ila ukweli ni kuwa pengine ulianza kwa kumdekeza kwa kumpa kila apendacho ikiwemo pesa,na yawezekana ulinyimwa unyumba na ukaishia kumbembeleza japo hukuwa na kosa na hivyo yeye akageuza fimbo ya kukuadhibu kwa kukunyima tendo kila atakapohisi umemkwaza,ulianza kwa kumuwekea wasaidizi wawili sasa kwa nini asishinde fb?
Hivyo nakushauri usimuache bali onesha misimamo kama mwanaume,maana ungekuwa na misimamo thabiti asingechukua pesa na kwenda kununua zawadi ya rafiki yake,jitathimini mkuu na uchukue hatua
Wanaishi kizungu yeye na mke wake.
Leo ndio nmeelewa kwa nini baadhi ya wanaume imefikia wanapotaka kutoa pesa kwenye mfuko wa suruali wanawaambia wake zao wasogee pembeni ili wasione kinachotoka.
 
Ningekuwa mimi wala ushauri wa mtu nisingetaka. Vile sipendagi ujinga, Ee Mungu nisaidie mja wako.
 
Brother pole Ila case yako inahitaji msaada wakiroho,Mpe likizo kidogo akajifunze kwao,
 
blaza, nilipofika kusoma sehemu uloandika kachukua hela kaenda kununua jokofu, roho imeniuma sana. dah, pole blaza.
jitenge na huyo binti atakuingiza kwenye umaskini.
mimi nipo napambana na wangu hapa ananunanuna hovyo habadiliki hata umuelekezeje anajisahau sana.
nashkuru Mungu sijamuoa na dalili za kuoa naona zinaanza kupotea, ni jipu huyu, kisirani mno, sometimes nasema labda kwasababu bado mdogo akikua ataacha ila kuna roho inanambia ntachomwa na jua sana huko mbeleni.

fukuza huyo mwanamke hata akiomba msamaha puuzia usiwe na huruma kama mimi huruma inatukosti sana kaka.
Mkuu,nadhani ukizaa namwanamke anakua kama kakuroga dizaini flani,hata mm binafsi hyo Hali yakhurumia mwanamke wakati unajua fika huyu nijipu,nakwamba Hana dalili zakubadilika zipo mwanamke wapwani huko Lindi,mkigombana ndani kesi unasuluhishwa namtaa , makelele ndani hayaishi ,kushika simu mara ugomvi wakuamliwa namajirani nawananchi yaan loh,Ila ukifikiria juu yamtoto unaamua kuyamaliza Ila,huruma zetu wanaume zinatuponza Sana kuendelea kulea Majipu
 
Ila mkuu si umeamua mwenyewe kumwekea wafanyakazi wawili wa ndani sasa kinachokuliza ni nini ndugu yangu?.

Nikwambie kitu sipendi uweachishe kazi hao mabinti ila kwa masilahi mapana ya ndoa na familia yako embu fanya kuwapa mitaji hao maninti kiroho safi uwaambie samahanini naomba mkataba wetu wa ajira uishie hapa.

Naona watakusikiliza alafu sasa huyo mkeo umuache afanye hayo yote mwenyewe ataacha ujinga wake na uvivu.

Wala usimpe talaka sababu bado utaumia mkuu, huyo bado mdogo sana miaka 28 anaweza mkagawana mali alafu akaenda olewa na kajamaa kaboya boya ukashangaa kabadilika hapo utaanza sema mkeo alikuwa anakucheat na huyo mume wake mpya kumbe walaa ni kwamba kajifunzia nje ya kwako.

Natumai umenielewa Bro!. Pole sana
Nice advice big up,
 
Duuh, huyu wangu sitakaa nimuache ng'oooo! Nimegundua wa kwangu ni mke mwema saaaaana,.. Nikisoma maisha ya ndoa ya watu na visanga vyao... Namshukuru Mungu kwa mke alonipa... Hakika nimepata mke haswaaaa... Pole yako.
Mkuu tupe vionjo unavyopewa ili nasisi tuone niladha zipi niadimu unapata
 
Naitwa Mr. Brian (Sio jina langu halisi). Umri wangu ni miaka 35 kwa sasa. Nilioa miaka mitano iliyopita na mke wangu hivi sasa anayo miaka 28.

Kusema kweli naipenda familia yangu na kama mwanaune najitahidi sana kuihudumia. Nyumbani kwangu tunao mabinti wawili wa kazi. Mmoja kwa ajili ya kusaidia kazi za ndani na mwingine kusaidia kulea watoto wetu mapacha wenye umri wa miaka miwili hivi sasa.

Pamoja na yote nayojitahidi kumtimizia mke wangu, yeye amekuwa mtu ambaye hatimizi majukumu yake kama mke.

Amekuwa na ile aina ya maisha ya mitandaoni, kwanza ni mtu wa kushinda sana Instagram, facebook, Watsapp, Snapchat na Jamii Forums

Katika Page zote za Umbea umbea, page za maeneo ya starehe, hoteli za hadhi hakosekani. Hana muda kabisa wa kunipikia chakula, kunifulia nguo na kazi nyingine zote wanafanya wadada wa kazi.

Nilimtafutia kazi katika kampuni fulani, alifanya kazi miezi miwili tu na kuacha maelezo yake eti mshahara ni mdogo mno ukilinganisha na elimu yake. Kumbe aliniongepea kwani ukweli ni kwamba alifukuzwa kutokana na uzembe kazini.

Sikuona tabu, nikamfungulia duka la bidhaa za nyumbani (mini-shop), lakini biashara hata ikawa haistawi, nilivyofanya uchunguzi nikaja kugundua kuwa sababu ni lugha yake mbovu kwa wateja kiasi ya kwamba ilikuwa haipiti siku bila kugombana na wateja kadhaa jambo lililofanya wateja kukimbia.

Nimechukua maamuzi mara kadhaa ya kumrudisha kwao lakini amekuwa akilia na kudai nimsamehe atajirekebisha lakini wapi, hubadilika muda mfupi na kurudi kwenye ujinga wake.

Jambo kubwa ambalo limefanya mpaka uvumilivu unishinde ni hili; Juzi kati kuna fedha Milioni mbili na nusu niliipata baada ya kuuza mazao yangu, kwa kuwa ile fedha nilipewa cash na ilikuwa siku ya Jumamosi usiku nikaazimia Jumapili baada ya kutoka Kanisani nakaiweke benki kupitia Wakala wa Fahari Huduma.

Kumbe mwenzangu aliziona, akachukua na kwenda kununua furniture, Oven, Friji na vikolombwezo vingine kwa ajili ya kumpa rafiki yake ambaye alikuwa anafanyiwa kitchen party Wiki iliyokua inafuata. Nilipomuuliza akawa akinipa stori za alufu ulela ulela. Hazina miguu wala mikono.

Nafikiri sasa nimechoka rasmi, hapo sijazungumzia masuala ya kunyimwa unyumba. Nafikiria Kutalakiana nae. Maana nahisi muda wowote naweza nikafa kwa pressure nikaacha wanangu bado wadogo.

Je , niko sahihi kwa maamuzi ya kumpa talaka nilee tu watoto mwenyewe maana sioni msaada wowote!View attachment 1094860
Hali pa kuchukua Hela yako na kwenda kufanyia Manunuzi ya zawadi za Kitchen Party ilikuwa ndio Tiketi yake ya Kuondokea Mkuu!
Ninashaa bado yupo na Unakuja humu kutaka Ushauri!
 
Hali pa kuchukua Hela yako na kwenda kufanyia Manunuzi ya zawadi za Kitchen Party ilikuwa ndio Tiketi yake ya Kuondokea Mkuu!
Ninashaa bado yupo na Unakuja humu kutaka Ushauri!
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] umri hufanya maamuzi ya busara kidogo sio hasira na haraka
 
Back
Top Bottom