Huyu kijana nitamsaidiaje apate ajira?

Huyu kijana nitamsaidiaje apate ajira?

Kiingereza ni janga la taifa, kama kazi yenyewe itahusisha kiingereza hiyo barua tu mushkeli, achilia mbali hivyo vyeti.

Na hapa linaweza likawa suala kubwa zaidi ya Kiingereza.

Maana inaonekana ama hajui kama Kiingereza chake cha kuunga unga, ama anajua lakini kakosa hata akili ya kutafuta mtu (au hata computer) kufanya spellchecking and grammar correction, au anajua lakini ni mlipuaji.

Lakini labda ni kitu cha kawaida bongo mpaka kinazoeleka.Hata wewe mwenyewe mkuu umetaja vyeti tu hujataja hili kama issue (unless kuonyesha barua ilivyoandikwa ndo una solicit input).

Alikuja jioni kisomo mwingine earlier today anatafuta scholarship ya masters degree in Education na madubwana kochokocho.

Nikamwambia kwa kiingereza hiki bora tafuta scholarship ya English course kwanza.

Kiranga,

Huyu kijana kama asingeleta hiyo barua angekuwa na ma vyeti yake mimi ningeona ni kawaida tu ningemsongesha front. Nashukuru ameandika hiyo barua nimepata kufahamu zaidi.
 
huyo anafafanana sana na zinduna binti aliyehojiwa na clouds tv anaulizwa kama umemaliza form 4 ulifanyia mtihani masomo mangapi? eti anajibu manne na alazimisha kabisa.mkuu huyo mtu atavuruga heshima yako

Aisee hapo umenena...
 
Duh!! Luck is when opportunity meets quality and qualification. Granted, the young man is lucky to have you as a referee. But I just cant imagine a University graduate writing such a nauseating English!!!

Mkuu,

Nadhani kuna haja ya kuangalia upya tuamue kama ni kiswahili ama kingereza. Inawezekana yakawa kama yale ya haki elimu labda ningemwambia aandike barua hii hii kwa kiswahili ningekutana na kiswahili maridhawa kabisa. Lakini sitashangaa kama huyu kijana ame graduate kweli , sasa swali linakuja hao walimu wake vp?
 
Mkuu wangu Maundumula,
Be careful na huyo mtu......am convinced kwamba huyo mtu anafahamu anachokifanya; ole wako ama ole wenu mzani huyo jamaa ni kilaza! Si ajabu hata hapa anafuatilia thread hii!

Let's be honest...kwa mtu mwenye kiingereza kibovu kama hicho anatarajiwa awe hata form IV hajafika. Jiulize, ameitoa wapi confidence ya kujifanya ana degree ya Business Administration! I repeat, anafahamu anachokifanya! Kama huyo jamaa angejinadi kwamba ni Engineer, nisingeshangaa! Let's say alisema ni Mechanical Engineer...so hata kama hana degree ya hiyo fani basi ningehisi labda anajivuna yupo fit practically! c unajua mafundi wetu wa gereji bubu? Unakuta mtu hata FTC hana, lakini yupo fit mbaya! Lakini jamaa anasema ana BA!!! Ujasiri huo ameutoa wapi? Look here, Certificate hana; sawa! Ndo hata transcript?! Be careful broda, msije mkadondokewa na jumba bovu; jamaa yupo kazini huyo!

NasDaz,

Huyu nadhani hata JF haingii maana angekuwa mtu wa dizaini hiyo ingemsaidia kidogo kukuza kiwango.
 
wonders shall never end.. kama kuna uwezekano wakumsaidia msaidie.
 
Mkuu,

Nadhani kuna haja ya kuangalia upya tuamue kama ni kiswahili ama kingereza. Inawezekana yakawa kama yale ya haki elimu labda ningemwambia aandike barua hii hii kwa kiswahili ningekutana na kiswahili maridhawa kabisa. Lakini sitashangaa kama huyu kijana ame graduate kweli , sasa swali linakuja hao walimu wake vp?

Mkuu wangu Maundumula,
There's no way kwamba a university graduate anaweza kuwa na kiingereza kibovu kama hicho.....i repeat; there's no way!! Count on my word; huyo mtu anajua anachofanya; kuweni makini hapo....isije ikawa ametumwa huyo!! Wengi wetu tuna Viingereza vibovu; lakini si vya staili hiyo especially kwa graduate hata kama alikuwa ni full madesa a.k.a Symb kama tulivyokuwa tunaita SUA!! Hivi ni graduate wa aina gani katika karne hii ambae hata kufahamu hafahamu kwamba ukiingia net anapata a well structured job application letter?! hivi ni graduate gani huyo asiyefahamu hata kuandika kwa usahihi jina la shahada yake? Come on chuck, Open up ur eyes! Kiingereza hicho ni ama cha primary school leaver or completely form four failure tena wa shule za kata za vijijini!!! Jambo la kujiuliza, ni kwamba ni wapi huyo mtu ametoa ujasiri wa kujifanya ni graduate; tena katika taaluma isiyohitaji nguvu bali weledi?! Hebu angalia hizo sentensi zake mbili za mwisho [Please Sir I beg you to accept my application. Im confident I will perform well if my application will be considered]Hivi huoni kuna tofauti kubwa sana hapo kati ya hizo sentensi zilizo kwenye mabano na sehemu iliyobaki ya barua yenyewe?! Mtu ambae anavunja kiingereza kiasi hicho asingeweza kuandika sentensi hizo mbili za mwisho kwa staili hiyo! Ukiniuliza abt the last two sentences, i can simply tell u kwamba hapo alishajisahau kwamba alitakiwa kuonesha kwamba ana kiingereza kibovu kupita kiasi!
 
Jamari Mbona Mimi hzi chance sizipati.?ama Kweli Kwenye miti hakuna wajenzi
Mimi nakushauri acha nae Kabisa kwa sababu Kama Kweli ni graduate hajui kuandika barua basi utandawazi angegoogle akili ya kawaida tu haihitaji elimu
 
NasDaz,

Mimi nilifikiri hizo sentensi mbili za mwisho labda ndio aliomba msaada mtu amuandikie? au pengine aliona barua mahali imeandikwa imemaliza kwa staili hiyo aka copy paste.
 
Kuna kijana mmoja alitokea hapa kwenye kibarua changu akanielezea anahitaji ajira. Akaacha wasifu wake CV nikapitia nikaona ana degree Bachelor of Business Administration kwa mujibu wa CV. Sasa nikazungumza na mkuu wangu wa kuajiri akasema poa mlete tutamfanyia "interview", sasa nimewasiliana na huyu kijana anipe vyeti vyake alivyomalizia chuo na shule zote zlizopita. Bahati mbaya hana cheti cha chuo, yeye ameniambia hajapewa.

Nikaomba anipe japo yale majibu ya mwisho "Transcript" na yenyewe hana. Nikamwambia anipe vyeti vyoote alivyokuwa navyo nione tutafanyaje, sasa hapa akaniletea cheti Form Six ambacho amefaulu vizuri kunishinda hata mimi enzi zangu, pamoja na barua ambayo imeandikwa kama nilivyonukuu hapo chini. Je ungekuwa wewe ungefanyaje? Mind you kwamba nikimpeleka kule mwisho wa siku mimi nakuwa kama referee wake na ninampigia chapuo kama mtu ninayemjua ingawa hata simjui kabisa. Na kwa kifupi anaonesha anaitaka sana kazi.Na sijui alimaliza hicho chuo au aliishia kati. Hapa chini ni kama alivyoandika yeye sijaongeza sijapunguza hakuweka hata nukta moja au mkato na hakusaini.

I (His name) i am pursued batcher of business administrationat univesty of ........... here it is the letter to request to your that I will submit my universty results which is not found in my certificaties and I fail to submit it dut to the problems which I was faced after complete my final examination because my father was die so I was fail to wait for such cerificaties. Please Sir I beg you to accept my application. Im confident I will perform well if my application will be considered.

Yours

.....................

kuna ishu nmekupm ndugu km vp icheki kwanza.
 
Piga chini, stick to the point kwamba wanataka degree zake la sivyo sorry! Kuna chuo kikuu kweli hapo!
 
Back
Top Bottom