Mtambuzi
Platinum Member
- Oct 29, 2008
- 8,809
- 15,421
Mila na desturi zetu zinatufundisha au kutuelekeza kwamba jinsia zetu zinasema pia kuhusu thamani zetu. Tumeambiwa na kwa kiasi kikubwa tunaamini kwamba wanawake ni dhaifu kwa wanaume.
Neno kuoa au kuolewa kwa asili yake lina maana ya kuchukua au kuchukuliwa. Hii ina maana kuwa kwa mila na desturi zetu, mwanamke huchukuliwa na mwanaume. Mwanamke baada ya kuolewa au kuchukuliwa huanza kuwa mali ya mumewe.
Kwa sehemu kubwa mila na desturi zetu zimepachika ndani mwetu imani kwamba mke huolewa kwa lengo la kumpa mumewe starehe na kumzalia watoto. Kumbuka kwamba imani hizo ziko kwa wanaume na wanawake pia. Ndio maana sio ajabu kukuta mwanamke akisema, ‘nimemzalia mume wangu watoto wawili .' Anachojua ni kwamba, yeye ni mashine ya kuzalisha bidhaa (watoto) inayohitajiwa na mume.
Mume kwa mkabala huo huamini kwamba anazo haki zote kwa mwili wa mkewe na mkewe hana haki hizo. Mke naye huamini kwamba, msemaji wa mwisho juu ya mwili wake ni mume.
Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba, kauli kama vile, ‘mke ni pambo la nyumba,' hazijitokezi tu kwenye jamii.
Kwa kuwa mwili wa mke ni mali ya mume kwa kila hali na jamii imetufundisha kwamba, jukumu la mke ni kumstarehesha mume na kumzaliwa watoto, na hii starehe pamoja na watoto vimejifunga kwenye tendo la ndoa. Mwenye haki ya tendo la ndoa kionevu na kifedhuli huwa ni mume.