Huyu kiumbe mwanamke!

Huyu kiumbe mwanamke!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,421
Mila na desturi zetu zinatufundisha au kutuelekeza kwamba jinsia zetu zinasema pia kuhusu thamani zetu. Tumeambiwa na kwa kiasi kikubwa tunaamini kwamba wanawake ni dhaifu kwa wanaume.

Neno kuoa au kuolewa kwa asili yake lina maana ya kuchukua au kuchukuliwa. Hii ina maana kuwa kwa mila na desturi zetu, mwanamke huchukuliwa na mwanaume. Mwanamke baada ya kuolewa au kuchukuliwa huanza kuwa mali ya mumewe.

Kwa sehemu kubwa mila na desturi zetu zimepachika ndani mwetu imani kwamba mke huolewa kwa lengo la kumpa mumewe starehe na kumzalia watoto. Kumbuka kwamba imani hizo ziko kwa wanaume na wanawake pia. Ndio maana sio ajabu kukuta mwanamke akisema, ‘nimemzalia mume wangu watoto wawili .' Anachojua ni kwamba, yeye ni mashine ya kuzalisha bidhaa (watoto) inayohitajiwa na mume.

Mume kwa mkabala huo huamini kwamba anazo haki zote kwa mwili wa mkewe na mkewe hana haki hizo. Mke naye huamini kwamba, msemaji wa mwisho juu ya mwili wake ni mume.

Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba, kauli kama vile, ‘mke ni pambo la nyumba,' hazijitokezi tu kwenye jamii.

Kwa kuwa mwili wa mke ni mali ya mume kwa kila hali na jamii imetufundisha kwamba, jukumu la mke ni kumstarehesha mume na kumzaliwa watoto, na hii starehe pamoja na watoto vimejifunga kwenye tendo la ndoa. Mwenye haki ya tendo la ndoa kionevu na kifedhuli huwa ni mume.
 
Leo niseme tu kua Mtambuzi... wanawake wamekutawala katika kila aspect of your interest... Dah!

Naomba tuletee na topic zinazo husu wanaume... hata sie wanawake tunataka taarifa za kaka/baba zetu.
 
Leo niseme tu kua Mtambuzi... wanawake wamekutawala katika kila aspect of your interest... Dah!

Naomba tuletee na topic zinazo husu wanaume... hata sie wanawake tunataka taarifa za kaka/baba zetu.

Bado kitambo kidogo nitakujibu dada......naandika kwa kufuata utaratibu nmiliojipangia au?
 
kuna concept umeigusia nahisi nimeipenda kuhusu maana halisi ya kuoa au kuolewa,,, vipi na maana ya kuoana?
 
Kwa hiyo mwanamke ni chombo cha starehe tu kwa mwanamke? au sijaelewa?
 
Lakini huo ni mfumo dume au?Maana siku hizi kila jambo mfumo dume!
 
Mume kwa mkabala huo huamini kwamba anazo haki zote kwa mwili wa mkewe na mkewe hana haki hizo. Mke naye huamini kwamba, msemaji wa mwisho juu ya mwili wake ni mume.

Bila shaka utakubaliana na mimi kwamba, kauli kama vile, ‘mke ni pambo la nyumba,’ hazijitokezi tu kwenye jamii.

Kwa kuwa mwili wa mke ni mali ya mume kwa kila hali na jamii imetufundisha kwamba, jukumu la mke ni kumstarehesha mume na kumzaliwa watoto, na hii starehe pamoja na watoto vimejifunga kwenye tendo la ndoa. Mwenye haki ya tendo la ndoa kionevu na kifedhuli huwa ni mume.

labda wataka kushindana na Muumba ambaye amesema ya kuwa Mke hatakuwa na sauti juu ya mwili wake ila mumewe na mume hatakuwa na sauti juu ya mwili wake ila mkewe...........1 Corinthians 7:3-5..................."Let the husband render to his wife the affection due her, and likewise also the wife to her husband......................The wife does not have the authority over her own body, but the husband does. And likewise the husband does not have authority over his own body, but the wife does...........................................Do not deprive one another except with consent for a time, that you may give yourself to fasting and prayer; and come together again so that Satan does not tempt you because of your lack of self-control..........."
 
Back
Top Bottom