Huyu kocha anajitahidi sana kujivua lawama wadau wa michezo tushamsoma

McDonath

Senior Member
Joined
Jan 2, 2018
Posts
110
Reaction score
105
Wasalaam wana jamvi,leo nimeamua tumuangalie kocha wa Yanga SC,Mkongomani Mwinyi Zahera(Papaa)

Huyu Mwalimu mwanzoni alionekana ni mtu anayejielewa na mwenye uwezo mkubwa wa kuunganisha timu yaani muwe wamoja kwa hilo nampa kongole sana amejitahidi kuleta umoja miongoni mwa wachezaji lakini pia hata kwa mashabiki wa Yanga Sc

Lakini Mwalimu huyu pale mambo yanapomuendea kombo amekuwa mjanja sana kwa kujivua lawama machoni kwa wana Yanga na wadau wa soka hapa nchini

Nakumbuka kuna mechi mambo yanapokwenda kombo hulalamikia wachezaji wake hadharani,Michango ya mashabiki,Viongozi,Ratiba,Viwanja na bodi ya ligi tena kama hii sababu ya mwisho hata jana wakati anahojiwa kuhusu kajiandaaje na mchezo ghafla akaanza kulaumu bodi ya ligi kama vile nj Yanga pekee ndio waliokuwa wanacheza saa 8 mchana.Azam media walipoona mzee wa gubu kaanza kubwabwaja tu wakamkatisha wakarudi studio

Ushauri wangu ni sina shaka na uwezo wa Mwinyi lakini lazima akubali kwa sasa Yanga haipo kwenye mzani mmoja na Simba siamini kama anatakiwa kulia sana ili watu tumuelewe kwamba hausiki na matokeo mabaya ya Yanga.Watanzania hatuwezi muhukumu kwa wakati huu.

Karibuni wana jamvi
 
zahera anasema kweli tff wanaibeba sana simba. kwanza marefa wanaochezesha mechi za simba wanaonyesha upendeleo wa wazi kabisa huku yanga wakiminywa ili wasipate ushindi huu ni uonevu
 
haiwezekani simba kila mechi wanashinda magoli ya ajabu ajabu mara offside mara penati mradi ni kubebwa tu
 
Simba mwaka huu ni wao ila kwa hali iliyoko Yanga ndo ingekuwa iko Simba basi Simba wangeshuka daraja!
Pesa ipo Simba wachezaji wazuri na muwekezaji mkubwa sana tu lakini bado ushindi kwa mbinde!!
 
Siku aliposema kuna timu zinapewa hela na Simba ili ziikazie Yanga,nikajua huyu ni wenge
Alipobaki Dar wakati timu yake ina game Lipuli nikajua njaa za wanayanga ndo zinamfanya aote pembe ila ingekua Yanga yenye stability kama ile ya Manji,Yanga wasingemuacha
 
zahera anasema kweli tff wanaibeba sana simba. kwanza marefa wanaochezesha mechi za simba wanaonyesha upendeleo wa wazi kabisa huku yanga wakiminywa ili wasipate ushindi huu ni uonevu
Huyo ni ZAHERA... wewe je unasemaje?
 
Simba mwaka huu ni wao ila kwa hali iliyoko Yanga ndo ingekuwa iko Simba basi Simba wangeshuka daraja!
Pesa ipo Simba wachezaji wazuri na muwekezaji mkubwa sana tu lakini bado ushindi kwa mbinde!!
Simba wamekaa kipndi kirefu wakiwa na migogoro iliyoambatana na njaa na ndiyo siri ya wachezaji wengi hapa kati kutoka Simba kwenda Yanga......haya mambo yanayoitokea Yanga sio mageni kwenye soka letu si kwa Simba,Yanga wala Ndanda
 
Simba mwaka huu ni wao ila kwa hali iliyoko Yanga ndo ingekuwa iko Simba basi Simba wangeshuka daraja!
Pesa ipo Simba wachezaji wazuri na muwekezaji mkubwa sana tu lakini bado ushindi kwa mbinde!!
Mo amewekeza Simba mwaka wa ngapi huu??
Kabla ya Mo Simba imewahi kushuka daraja??
Toka Manji amwage Pesa zake Yanga timu imewahi kugusa ROBO au Makundi CCL??
JIBU HAYA TWENDE SAWA.
 
Tumetia migoli, makambo anajua kuwasumbua mabeki na Yanga itachukua ubingwa mwaka huu''
Maneno hayo huyatamka km akiokotea kigoli chake kimoja
Hii TFF inaipenda sana simba limechi limechezwa vibaya referee anaipenda sana simba hata ule mgoli wa kagere aliumufunga kwa mukono na alikuwa offside.' '
Maneno haya ukiyasikia basi kuna mambo tyr yashamsibu
Kaoshwa bukta yake au kanyang'anywa tonge mkononi na kasugulishwa chini.
Huyu ndio POPOO MWANYA ZA HIRA
 
Tena jana licha ya kufungwa walizuiliwa hotelini Morogoro walipe deni la hoteli.
TASAF FC.
Wamekuja na wimbo mpya anayeongoza wimbo ni Poyoyo Zahera.
 
Simba mwaka huu ni wao ila kwa hali iliyoko Yanga ndo ingekuwa iko Simba basi Simba wangeshuka daraja!
Pesa ipo Simba wachezaji wazuri na muwekezaji mkubwa sana tu lakini bado ushindi kwa mbinde!!
Itakua umeanza kupenda Mpira Mwaka huu....Simba tumepitia kipindi kigumu Sana,Rudi nyuma manji kaanza kuidhamini yanga lini na Simba tukiwa tunaunga unga Hadi mnachukua ubingwa wa dhuruma Mwaka juzi kwa maamuzi ya ajabu ajabu,Simba tukaanza kupandisha wachezaji toka Timu B ambao wengi wametapakaa katika Timu mbalimbalu TPL na bado tulikua tunapambana,kwa Tanzania Simba ndio Kila kitu ukiangalia hata wachezaji wa Timu nyingi zinazoshiriki TPL wamecheza Simba angalia hata yanga yako.
 
Anaongea sana kwa kweli. Halafu akumbushwe hawezi kuwadanganya watu wote, wakati wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…