Wasalaam wana jamvi,leo nimeamua tumuangalie kocha wa Yanga SC,Mkongomani Mwinyi Zahera(Papaa)
Huyu Mwalimu mwanzoni alionekana ni mtu anayejielewa na mwenye uwezo mkubwa wa kuunganisha timu yaani muwe wamoja kwa hilo nampa kongole sana amejitahidi kuleta umoja miongoni mwa wachezaji lakini pia hata kwa mashabiki wa Yanga Sc
Lakini Mwalimu huyu pale mambo yanapomuendea kombo amekuwa mjanja sana kwa kujivua lawama machoni kwa wana Yanga na wadau wa soka hapa nchini
Nakumbuka kuna mechi mambo yanapokwenda kombo hulalamikia wachezaji wake hadharani,Michango ya mashabiki,Viongozi,Ratiba,Viwanja na bodi ya ligi tena kama hii sababu ya mwisho hata jana wakati anahojiwa kuhusu kajiandaaje na mchezo ghafla akaanza kulaumu bodi ya ligi kama vile nj Yanga pekee ndio waliokuwa wanacheza saa 8 mchana.Azam media walipoona mzee wa gubu kaanza kubwabwaja tu wakamkatisha wakarudi studio
Ushauri wangu ni sina shaka na uwezo wa Mwinyi lakini lazima akubali kwa sasa Yanga haipo kwenye mzani mmoja na Simba siamini kama anatakiwa kulia sana ili watu tumuelewe kwamba hausiki na matokeo mabaya ya Yanga.Watanzania hatuwezi muhukumu kwa wakati huu.
Karibuni wana jamvi