Huyu Mayele ni bonge la mshambuliaji

Huyu Mayele ni bonge la mshambuliaji

Mayele huyu mwenye goli 12? Kagere alipokuwa moto alikuwa anafunga 20+
 
Kimataifa..yes , kupitia kwa msemaji wao msomi mwenye degree mbili za south africa na china bwana Hajj manara Yanga sc walitangaza kwamba mwaka huu watachukua ubingwa wa Afrika na wataanzia round ya kwanza siyo ya awali, inarajiwa Fiston mayele ataibuka top scorer wa CAf champions league
sijawai kuona semaji bovu kama lile[emoji2][emoji23][emoji28]
 
Ni kweli ni hatari ila kusema kuwa ni hatari bila kulinganisha takwimu za michezo aliyocheza na idadi aliyofunga na kisha kulingamisha na takwimu za waliopita ndani ya miaka hiyo uliyotaja nadhani umekosea sana. Nakushauri hoja yako ijikite sana kwenye takwimu zaidi
 
Katika miaka kumi iliyopita toka hapa tulipo, tathimini yangu inanionesha hajawahi tokea mshambuliaji hatari kama Fiston Mayele.

Donald Ngoma na Okwi angalau kidogo.

Angalia mechi ya Jana Kigoma, japo hajafunga lakini mambo aliyokuwa anafanya pale mbele ni makubwa sana.

Anatumia hesabu ktk kupiga mipira golini, mikimbio, anavyojiposition nk.

Simba namponda kwakuwa hawana striker bora mfano wake.

HONGERA MAYELE, HONGERA YANGA
Mayele huyu ambaye mechi ya Yanga vs simba aliondoka bila kuona ile milingoti 3 ya goli iko wapi? Au kuna mayele mwingine?
 
Ongeza goli vs Geita lililokataliwa kimagumashi. Weka na nafasi mbili za wazi alizodhulumiwa VS Mbeya city. Usisahau magoli aliyofunga kombe la Azam confederation
Goli 12 tunapata tabu hivi, angefikisha 20+....
Ingekuwaje wakuu.
 
Mayele ni stricker mzuri sababu ni kinara wa kufunga magoli.

Sifa kuu ya stricker ni kufunga magoli.

Swali ni je'atadumu kwa misimu mingapi kuwa kinara wa ufungaji na pia ataendeleza ubabe wake wa ufungaji kwenye mechi za kimataifa? Ngoja tusubiri.
umeongea ki mpira haswa,ndugu yangu Leo hujala kande,[emoji1]?
 
Eti miaka 10[emoji23][emoji23][emoji23]hivi unamjua OKWI wewe?huyu mayele hata kagere tu hawezi fikia rekodi zake

Sent from my PBBM00 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom