Uchaguzi 2020 Huyu MC kwenye mikutano ya kampeni ya Tundu Lissu ni nani?

Uchaguzi 2020 Huyu MC kwenye mikutano ya kampeni ya Tundu Lissu ni nani?

Anaitwa Amani Golugwa ni katibu wa chama kanda ya kaskazini. Yupo vizuri sana kwenye kampeni.
 
Nikajua ni MC wa michano aisee kumbe ni master of ceremony. Sawa.
 
Kwa sisi ambao hatushabikii upande wowote wa kisiasa na tunaofuatilia kampeni za uchaguzi mkuu wa Rais kuna huyu "mwamba" MC wa CHADEMA mwenye sauti na punch nzito sijui anaitwa nani.

Hakika CHADEMA mmelamba dume kuliko uchaguzi wa 2015 ambapo aliyetumika kama MC, ndugu John Mrema alionekana kupwaya mno.

Huyu jamaa wa sasa ana ubunifu na amsha amsha ya hatari. Nadhani atakua ni mmojawapo wa viongozi waandamizi wa chama pamoja na timu ya kampeni.

Ningependa tumfahamu kidogo

NB: Kwenye picha ndio huyo aliyevaa suti
Yani mwanaume anasifia sauti ya mwanaume mwenzake, kama wewe ni mdada sina shaka na ilo ila kama kidume again familia inakutegemea aiseee! umeizalilisha sana familia yako.
 
Back
Top Bottom