Yanga ina mashabiki wa ajabu sana. Sijaelewa hizi kejeli za Mukwala zinatokea wapi. Ndiyo anaweza na anahitajika kufanya vizuri zaidi ila kama chaguo la pili kama striker namba zake siyo mbaya kabisa.
Alifunga goli muhimu dhidi ya Mashujaa na nilisema wakati ule kuwa ule ushindi ndiyo unaenda kuipa Simba ubingwa. Nilisema vile maana nilijua unaenda kuamsha nini ndani ya wachezaji wa Simba. Wote tumeona mechi zingine ngumu ambazo Simba imepata ushindi ikiwemo wa dakika za jioni, chachu yake ilikuwa ile mechi ya Kigoma.
Usikute mnamsagia kunguni ili Simba imuache mumchukue.