NostradamusEstrademe
JF-Expert Member
- Jul 1, 2017
- 3,402
- 4,532
Juzi nilifungua simu yangu ya smart nikakutana na clip ya mchungaji flani sikuweza kujua ni wa kanisa gani ila maneno yake ni ya kweli kwa utafiti wangu hebu tuone alisemaje
Ukiona mtu amekukosea au anakukosea au anakufanyia mabaya mara kwa mara na hataki kukuomba radhi au kujirudi huna haja ya kulipa kisasi wewe muachie Mungu japo mungu sio wa kulipa visasi ila kuna mahali atakumbana na kisiki au atakutana na mtu atampa maudhi kama anayokupa.
Ukiona mwanamke anapenda kusemea watoto wa wenzake mabaya huku yeye bado ana watoto wadogo wanakuja.Muache tu hali kama hiyo hiyo itamkuta huko mbeleni na atakuwa hajui kuwa anapata malipizi.
Niliijaribu kutafakari nikaanza kuwaza mifano ambayo ni live kabisa.Kuna jamaa yangu alikuwa na urafiki na mimi lakini wa kinafiki sana alikuwa ananionea sana kijicho kwa maendeleo yangu na alishawahi kufanya majaribio ya kutaka kuniangamiza lakini pamoja na hayo siku moja akapata shida nikamgharamia matibabu yake lakini alivyopona shukrani yake bado ni kutaka kuniangamiza mimi.Lakini mungu akaona hii sio haki akaamua kumtanguliza yeye mbele za haki.
Yupo mama mmoja kijijini kwetu miaka ile UKIMWI ndio unaingia alikuwa ana tabia ya kutangaza watoto wa wenzake kuwa wana ukimwi kisa tu aliona kasimama na flani.Kilichotokea yule mama baada ya kupita miaka kadhaa watoto wake watano wakaja pata gonjwa hilo hilo na wakafariki alichanganyikiwa hadi mdomo ukaenda upande.
Yuko mzee mmoja jirani yangu alikuwa anatabia ya kukosoa malezi ya baadhi ya jirani zake wanayowapa watoto wao maana huyo mzee ni mtu wa dini kidogo lakini kiaina.Matokeo yake katika watoto wake akatokea mvuta bangi na kibaka na mmoja wa kike yuko nyumbani ana watoto kila mmoja na baba yake.
Chunguza sana watu washirikina au tuseme wachawi wanaoonea kijicho maendeleo ya wenzao na hujaribu kutumia nguvu za giza kumrudisha mtu nyuma kimaendeleo ikiwezekana kumzimisha kabisa lakini watu hao hao unakuta maisha wanaoishi ni ya ufukara wa kutupa