Huyu Mdada Anateseka!...Kuna Namna Ya Kumsaidia...

Mijitu kama hiyo inakera kweli kweli hakuna namna wala sababu ya kuhalalisha ukatili na unyama anayemfanyie mkewe na watoto wake. Naruhusiwa kutumia AK 47 kwa hili jamani ?
 

wapi huko Fidel na miye unipeleke nikaokoe familia ?..
nway kulishwa huko alikutaka mwenyewe,alianzaje kwenda huko in the first place kama sio tamaa na carelessnes ya kipumbavu?
nampa pole huyo mama
 
Manaume mengine bana, kama hayawezi kuendesha ndoa zao kwanini yanaoa.......nimekasirika kweli!...wengine tunahaha kupata wake, mijitu mingine inatesa wake zao....aaaaaaaaaaarrrrrrrrrrgggggggg

Wewe unaye haha kutafuta mke, na huyo mwanaume aliyemsema Boflo wote lenu moja.
Huwa mnaanza hivyo hivyo. 'ooh nahaha kumtafuta mke..' mkishapata sasa.
Yani wanaume!! Mungu atawalipa.
 

kwan hilo limbwata linakuwaje? si ngono zembe tu? na isitoshe wanaume wenyewe wanaenda kutongoza na kudanganya cna mke! bi mdogo akijua ana mke ndo either anampiga chini au anamlimbwata!
 
Wewe unaye haha kutafuta mke, na huyo mwanaume aliyemsema Boflo wote lenu moja.
Huwa mnaanza hivyo hivyo. 'ooh nahaha kumtafuta mke..' mkishapata sasa.
Yani wanaume!! Mungu atawalipa.
Mh dada nawe ushakutana na design hizi nn, umesema kwa uchungu
 
tatizo bado lipo palepale,mama pamoja na kuchukiwa kote huko yanini kuzaa tena?kisha polisi ipo sheria zipo huyo mwanaume peleka kwenye sheria kisha mgawane mali ushike hamsini zako mama,ukiendelea kuvumilia iko siku atakutoa roho.
 
Yalishanikuta mpendwa na sina hamu.

ucjali tupo wengi, yote maisha na si umejifunza kitu pia dia? mi kwangu ilikua ka fundisho imenifanya niwe so strong!
 
Huu ndio mwisho wa dunia, sishangai hayo kwani yameekuwa ya kawaida siku hizi, muombe Mungu wako akunusuru na hizo taabu.
 
Jamani msisingizie pepo, hiyo ni tabia yake tu, na ukichunguza zaidi unaweza hata yeye alitoka katika familia iliyokuwa na style hiyo ya maisha. watoto wake mwenyewe kwanini asiwathamini?

Mbaya zaidi huyo dada asivyo jijali bado anaendela kuzaa na jamaa akikuletea Mdudu. ajua Tayari wamesha tengeneza Network ya wapenzi. yeye ana jiheshimu je huyo kimada!

Dada chunga sana maisha yako
 
KAMA NI KWELI................
1.Mme na mke kuvumiliana ni muhimu.Swala la ngono nje ya ndoa ufumbuzi wake ni talaka,Kama ana uthibitisho kuwa mmewe ana mtu nje,hana haja ya kuendelea kuvumilia.
2.Mwambie arudi kwao kama hana ndugu aende kwa marafiki au schoolmate,office mate wanaosali pamoja nk
3.Njaa haivumiliki,mwambie aachane nae.Akili yangu inaniambia kuwa asipoangalia atauawa aidha na mmewe au na hawara ya mumewe.
4.Kama amekosa kabisa cha kufanya,basi amtafute kijana,ampe pesa kidogo tu,halafu ampe kazi ya kumfuatilia mumewe,akijua yupo wapi,mchezo unakuwa rahisi awachukue watoto wote kama saa 3 hivi usiku aende akamkabidhi wanawe,ikiwezekana apitie kwa mjumbe wa nyumba kumi.
5.Aaache kabisa hasira na kulia,hasira hukaa kifuani mwa mpumbavu.atulie,amwombe Mungu atampa suluhisho sahihi.
6.Aaanze biashara yoyote,kwa jinsi ilivyo,akimwelezea mtu yoyote,anaweza pata pesa japo kidogo za kuanzia kabiashara.
7.Mwambie kuna kitu kinandelea nje ya ndoa yake,lakini haya mambo ni temporary,kuna wakati atastuka na kurudi kwake.
8.Kwa sasa afute kabisa kichwani kama ana mme,hii itamsaidia kuendesha maisha.
9.Mweleze pia asisahau kuvaa zile condomu za kike,akizivaa kama zinavyotakiwa mumewe hatajua kuwa kamvalia condom
10.Anaweza kwenda pia ustawi wa jamii akaeleze kuwa,mumewe hampatii yeye na wanawe haki zao za msingi.
11.Mmewe huyo keshapaikana lakini bado anaakili yake,ndio maana alikumbuka kuja kumtoa hospitali japo baada ya siku tano.
12.Nadhani bado anampenda mkewe asingempenda angeshamfukuza siku nyingi tu,ngoja aibiweibiwe huko nje atarudi tu pesa zikiisha.
13.Asiende kwa mganga, ANAWEZA akajikuta yupo kwa mganga yuleyule mganga wa mwizi wake?yaani mganga wa adui yake ni hapo sasa atakapogeuzwa nyau.Elewa kuwa mwizi wake kama yupo anammonitor yeye kila siku anafanya nini,hakuna mwanamke anaetembea na mme wa mtu asijue data za mke wa huyo jamaa,hivyo huyo mama mfano akienda kwa mganga akatoa sh 30,000 hivi mfano,yule mwizi/mke mwenzie anaweza kwenda pale pale akatoa sh 60,000/ unasemaje hapo?kwa nini kibao kisigeuzwe
14.Baada ya kukupa dawa utasikia mganga akisena'' nenda salama mganga ni mungu,au tuombe Mungu''hii inaonyesha kuwa hata yeye mganga anategemea Mungu.....kwanini usimwombe wewe Mungu wako moja kwa moja?.Au hujui kuomba?...Jifundishe..
15.Binafsi nilishaomba mambo mengi tu na hapo hapo napata nikitakacho...pasipo kukosa. wakati mwingine kabla hata ya kusema AMINA.NAJIBIWA NA KUPATA NITAKACHO.
Mwisho kwa wanaume na wanawake wote wa hapa JF TUWENI NA HURUMA jamani, unakaa/kumzuia mpenzio hata chakula asipeleke kwake? oooooh NO. hata mambo yenu hayawezi kufanikiwa kabisa.
 
asante mkuu, nimerudi salama....mambo niliyoyakuta huko sina hamu na wakenya..hawafai

mmmmmm mnona ukatujumlisha sote jamani. tumefanya nini? pole ila wakenya wengine kaa mimi wasataarabu kupita kiasi! kina fatuma na zuena wamekutenda nini??
 
Watu wengi wanadandia hoja nakutoa tuhuma bila kusikiliza upande wapili, Je mnyajua huyo mama alifanyanini mpaka jamaa amkaamua kufanya hivyo? mahusiano ni taasisi tata, siyo rahisi mtu kuanza tu nakumuona mtu aliyekuwa anamwita darling kama mtua asiyefaa kwake. nakumbuka kuwa kwenya mahusiona tunatafuta faraja,kusaidiana, kuoneana hurumu,kupeana pole na vijambo vingine vidogovidogo na wala si mambo makubwa sana, hayo wakati mwingine uliyapata hata bilakuwa na mtu wako wakaribu.

Tambueni nimuhimu huyo mama aangalie wapi aliruhusu akatekwa na shetani na kitumbua kijaa mchanga, kisha atumie utaratabu wa kimahusiano kudisha nyumu Moyo wa mume wake ilindoa yao irudi kama kawa.

Angalizo kwa mama angalia mlipojikwaa kaa muongee hatakama ni miezi sita ijayo. Huyu ni Mumeo pambana kumkomboa.
 
amwombe Mungu sana tena sana aichoke, tafute ndugu wa karibu ili ata wamsaidie chakula jamani mama aliyejifungua inabidi pia apate msaada.
mijinaume bwana aarrh afu utamsikia mtu anasema nimeoa na nina watoto WTF. bora ata aanze biashara ya kuchoma mahindi ili mradi tu awe na kipato kidogo cha sumsuport.
poor woman.
 
My dear kwanza pole sana pia hongera kwa kuwa mwanamke mwenye uvumilivu kwa kizazi hiki ni wachache sana wanaoweza kuishi kwenye mateso na mkunguto kama wewe! ingekuwa mimi nilishaondoka! samahani dada kwani huna ndugu jamani? na je ni nini kikubwa hicho unachongangania kwa huyo bwana? ondoka unasubiri aje akuulie huko ndani! ondoka nenda kwenye ofisi haki za binadamu watakusaidia samahani kwa kukushauri uondoke nimeumia sana! hawa wahaume siku hizi wameingiliwa na ungojwa wa kusahau maagano yao timua usisubiri aje akumalizie huko ndani....ninazo kesi nyingi nimeziona na kuzisikia za aina hii wanawake wanateseka...jamani kama kuna mwanaume katika forum hii ana hii tabia aache!! mwisho wa dunia cha moto utakiona...pole dada lakini ushauri wangu miaka kumi unapigwa sasa itakuja miaka inayokuja kuuliwa ondoka nenda kwa ndugu wakusaidie huku unafuatilia haya mambo sehemu zinazohusika...
 

hapo kwenye ntekundu kwa kweli panahitaji imani kama ya kichaa, MTUME YAKOBO ANAKWAMBIA IMANI LAZIMA IAMBATANE NA MATENDO, HUYO MAMA ANA SHIDA HATA CHAKULA NI SHIDA, NA WEWE UNAMPA USHAURI WA KWENDA KUSHINDA KANISANI, HUU USHAURI UMEWAPOTEZA WENGI SANA KULIKO WALIOFAIDIKA,

HUYO MME WAKE TAYARI ANA MJI SEHEMU NYINGINE NA ANA WATOTO, SASA AKIRUDI HUKU KULE KWENYE WALE WATOTO WENGINE SI ITAKUWA HIVYOHIVYO TU?,
HUYO MAMA ANAHITAJI ZAIDI MSAADA WA KIMAENDELEO NA KISHA KIROHO, SIDHANI KAMA ATAKUWA NA MOYO WA KUSIKILIZA NA KUOMBA KWA IMANI KAMILI KAMA WATOTO HAWAJALA, HAWANA MATIBABU, HAWAENDI SHULE,
 
Libwata siku hizi dili mama,
Mtu anamlisha mwanaume kwa matakwa yake binafsi na akili za mwanaume zinahamia kwa huyo kimada.

Hakuna kitu kinachoitwa Limbwata, ni visingizio tu. How does it work? yaani mtu unapewa dawa (?) ili akili ihame na umsahau mkeo - na kweli dawa inafanya kazi?

I would like to test it!
 

Kama unataka kuolewa haraka matokeo yake ndo haya,lkn ukimchunguza vizuri sana mwanaume wako kwa muda wa kutosha hutababika naye sababu unamjua mpaka tabia zake mpaka hobby zake mpaka kwenye mizizi huko kwao na mengineyo.

Sasa wanawake wengi huwa hamko makini katika kuchagua waume sanasana mnaangalia vilivyo vyepesi mfano ana tabia nzuri mpole mwema hapana si hivyo,chunguzeni hadi myaone makucha ya mwanaume wako ndo hapo utajua alaa kuumbe yuko hivyo.Vilevile kama wewe na Mungu mko karibu haya si rahisi kukukuta Mungu hawezi kukupa mwanaume atayekukusumbua wewe milele katika maisha yako na kama amekupa msumbufu anajua atabadilika kwako na hatimaye anakuwa mwanaume mzuri tu.
 
Sawa mm naona kila mmoja anayechangia anatoa pole hakuna solution. ilitakiwa tumuulize kasomea nn , au ana ujuzi gani ili kama kuna mtu humu ndani kwenye JF ana Influence somewhere amsaidie ili apate kipato cha kujikimu na watoto wake. hata kama ni kazi ya Kufagia itamsaidia kuliko kumsubiri huyo mbaba aje kuleta pesa ya matumizi. IHALI AMESHASHIKWA MASIKIO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…