Huyu mdada na mambo yake; simtaki tena

Huyu mdada na mambo yake; simtaki tena

Wewe ni handsome mzee au nini mbona wanawake wanakuganda sasa naenda kusema nyumbani kwa mama haiwezekani kila siku kaka anatoa nyuzi mpya kuhusiana na michepuko
Hizi changamoto zinatokea hapa duniani mkuu
 
Mbona unavyo vigezo vyote vya kulogwa mkuu,

unae yule, unae huyu hapo tayari unakuwa umekidhi vigezo vyote vya kurogwa. Na hupaswi kumlaumu mtu jilaumu mwenyewe.
Nataka nibaki njia kuu mkuu; namna ya kuachana nao ndio changamoto; usipopiga simu, utapigiwa.
 
Hakuna cha mganga wala nini kuna mtu atakuwa anampa ubuyu uyo kamweka infomer wa kumpa habar zako kuwa makini sana
 
Subiri Kurogwa au Mambo Yako Kuharibikiwa Huko mbeleni. Mnapenda Sana Wanawake na Kutembea Hovyo hovyo na Kila Mwanamke . Mnafikia Hatua Mnaingia Maagano na Majini
 
Siku za karibuni nilitembelewa na mpenzi (mchepuko) wangu, na ilipofika jana jioni nikaona nimtoe 'out' kidogo, tuende 'club' moja kusikiliza mziki pamoja na kuburudika.

Mpenzi wangu akaomba, huku akinilazimisha; avae kikaptula kifupi, pamoja na tshirt ya nyuzi nyuzi, kwa sababu kuvaa kwake hivyo ndio atajisikia vizuri; kwa sababu yeye ni mtu wa kwenda na wakati.

Nikatafakari, nikaona hakuna tatizo; ila baadaye nilikuja kugundua kuwa huwa anataka 'attention' za watu. Akipita mahali, kila mmoja amkodolee macho kwa uzuri alionao.

Ikabidi tuingie 'club', tukapiga vinywaji vyetu, pamoja na kucheza mziki. Ilipofika saa tisa, tukarudi nyumbani.

Leo majira ya saa tisa mchana nikapigiwa simu na mchepuko wangu wa zamani ambaye yupo mkoa mwingine, alipiga mara ya kwanza sikupokea, akapiga mara ya pili sikupokea pia. Ikabidi nimtumie ujumbe, nipo kwenye kikao nitafute baadaye.

Saa 12 jioni akanipigia; ikabidi nipokee simu yake, ili niweze kumsikiliza. Akasema alikuwa anataka anijulie hali tu, nami nikamwambia niko powa. Pia akasisitiza, ijumaa tuonane kwa ajili ya kukumbushia penzi. Nikamjibu, tutaanglia kama muda utaruhusu.

Baada ya mazungumzo hayo; akaniambia ameota ndoto mbaya juu yangu; mi nikamuuliza, inahusu nini? Akasema, nimeota juzi ulienda 'club' na mwanamke, alikuwa amevaa pensi ya rangi nyeusi, na pale 'club' mlifanya 1,2,3.

Ingawa aliyosema ni sahihi, ila kwenye siku alichanganya; mi nikamjibu hakuna kitu cha namna hiyo, nilikuwa nyumbani nafanya mambo yangu na wala sijatoka na mtu.

Basi, akasema; itakuwa ndoto yake si ya kweli. Hofu niliyonayo, huyu binti ni mtu anayependa sana mambo ya kwenda kwa babu, hasa kuhusu mambo ya biashara zake. Inawezekana, kwenda huko alijaribu kunipiga chabo; ndio akapewa hayo maelezo.

Hapa nilipo nimetafakari sana; nikaona Ijumaa hakuna ulazima wa kukutana naye, ingawa amesisitiza sana; hofu, ni kutotaka kuingia kwenye mtego nisioujua.

Wakuu, ushauri wenu muhimu.
Usiende kuonana nae Kuna mtego.... Na usijaribu kulala nae utajuta
 
Hahahaaa! Humu ndani Kuna utoto sana.

Huyo anapewa umbea na mtu wa karibu yako, ila taarifa ya umbea haikukamilika, ndio maana kajichanganya.. Sasa unakurupuka kuwaza uchawi [emoji23][emoji23]
Kuna mtu anakujua na anamjua huyo demu wako, aliwaona club ndio kampa taarifa.
 
Mpaka hapo hujajua kuwa huyo demu kavujisha mkanda mwenyewe?

Ukipata ukimwi utuambie pia
 
Back
Top Bottom