Huyu Mo ni tapeli, Magufuli atusaidie kumdhibiti

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Hivi huyu Mo anawezaje bila aibu kusema bado hajawekeza Bilion 20 Kwa mujibu wa mkataba Ila anachofanya sasa ni kuipa Simba 'ruzuku' ya bilioni 3 kila mwaka?

Simba sio timu ya kupewa ruzuku.
Timu kubwa kuliko zote east Africa Kwa fan base inampa yeye Mo 'free promo ya Bidhaa zake zote. Hadi anaweza kuwazidi Azam Kwa sales...hadi Diamond kampa free promo Kwa kupitia Simba.


Toka ajihusishe na Simba mauzo ya Bidhaa zake yame tripple na amekusanya zaidi ya hizo bilion 3 kila siku Kwa faida..halafu bila aibu anakuja kusema anatoa ruzuku Simba.

Magufuli atusaidie kumdhibiti huyu Mo..agharamie matangazo yote ya Bidhaa zake kimkataba na atoe hela Kwa mujibu wa mkataba
 
Ndo leo leo tangu nimeingia jf, nimeona The boss umeandika utopolo. Hivi mtu anatoa mabilioni analipa mishahara na kusajili wachezaji Bado mnaona utapeli.

Wewe uliwahi kununua hata jezi yasimba kuchangia klabu au kutoa mchango was hata 800,000 kwa wafanyakazi wa klabu ? Kabla ya kusema Mo tapeli think twice!

Je bila Mo mna power ya kusavaivu kwa muda upi. Wenye chokochoko Wengi unakuta huna hata kadi ya uanachama hapo.
#mchakato bado
 

Kwa Nini msirekebishe mikataba au mfute hile isiyo na tija...
 
Jamaa kaongea kipuuzi sana
Mo anawekaje hiyo 20b wakati mchakato bado haujakamilika?
 
Bro we ni Boya kweli, Simba ipo kwa miaka mingapi na imechukua ubingwa mara ngapi bila Mwamedi kuwepo. Mwamedi haisaidii Simba bali amekuja Simba ili afaidike, Kama ni hivyo Simba nayo inapaswa kufaidika aweke 20b alizoahidi aache ujanja ujanja. Mbona African Lion aliikimbia Kama hakuna anachopata Simba. Mwamedi anajhitaji zaidi Simba kuliko imavyomhitaji sema tu basi timu zenyewe zina watu viazi Kama wewe!
 
Ndio ujue mswahili mswahili tu

Mwisho wa siku hata Mo akiweka hiyo pesa kwenye account italiwa na waswahili halafu mambo yote ya usajili, mishahara na kila kitu wataendelea kumtegemea yeye.

Haya yeye Mo mwenye hisa 49% anatoa pesa ya usajili, mishahara na kajenga uwanja.

Tuambizane wenye hisa 51% wameshatoa nini ?
 
Rais wako aliyepita alikwambia , "ukitaka kula, kubali kuliwa".
 
Mpira wa kibongo miyeyusho.

Timu hua hazijifunzi.

Zitapitia shida ile ile kila mwaka ila hamna kujifunza hata punje.

Walianza Yanga. Manji anaihitaji Yanga kuliko Yanga inavyomhitaji Manji.

Yakatokea ya kutokea hadi leo timu inasua sua.

Naon Simba wanajiandaa kufuata mkumbo. Kwamba Mo anaihitaji Simba kuliko Simba inavyomhitaji Mo? Au siyo?

Yaani hapa Bongo Yanga akizingua na kua omba omba msimu huu usishangae misimu miwili mbele Simba ikafuata mkondo huo huo.

Na hawajui kujitegemea na hawajawahi kua na mipango ya kujitegemea
 
Umeandika ukweli ila sidhani kama hawa mikia watakuelewa! Na Mwamedi ameshawajulia......!.
 
Mkataba unasemaje kuhusu billion 20 ?

Tuanzie hapo kwanza.
 
Simba imeporwa na mafisadi ki mafia.
Azam tv anatoa bilion 5 za matangazo
Sportspesa anatoa billion 5
Voda 5 billion
Yeye anaetumia brand ya simba atakavo ndo anatoa 3 b ? Ndio apewe simba kuimiliki by 70% ?
Katika Masharti ya "kumuuzia" club yetu ni kujenga uwanja a mpira wa kisasa na kutoa premium ya 20billion itayo wekezwa ili kuondoa utegemezi.
Yote hajafanya hilo. Ni kinyume na mkataba hivo kisheria umevunjika.
Utapeli alioufanya ili kuwadhibiti wanachama ni kuwapa share wote kwa kugawana 20% ya shares.
Hivo kawaziba mdomo kwani wamepata hisa bila kulipa kitu.
Haji manara ndio mpiga domo wake kubabaisha watanzania juu ya utapeli huu.
Ametumia vyombo vya dola kuwadhibiti wapinzani wa fisadi huu.
Mo imetapeli viwanda na ma gowdown kibao yalio kuwa RTC sasa ametapeli Simba timu iliojengwa kwa jasho na wazee wetu.
 
Mchakato haujakamilika ? Au Hawa taki kuukamilisha!!

Niwaambie tu mnaosema sijui anatoa hisani ya 3bil a year na haingizi chochote ni hvi halina CAPITALIST duniani anayefanya biashara ya hasara.
Kwani nani kasema anafanya kwa hasara?

Saiv wanaweka mambo sawa ili baada ya mchakato ndipo waanze kupata faida.

Hamna biashara utapata faida bila kuwekeza mkuu
 
Acha ushabiki maandazi wewe

Hiv unajua spotpesa anatoa hiyo blion 5 kwa mda gani?

Voda nae anatoa hiyo hela kwa mda gani?
 
Nyinyi paka fc mmezidiwa maarifa na mdosi, mmeuza timu kwa kipande cha kioo kama mwanachama wenu na babu yenu Chief Mangungu alivyouza Tanganyika kwa mjerumani
 
Mchakato haujakamilika ? Au Hawa taki kuukamilisha!!

Niwaambie tu mnaosema sijui anatoa hisani ya 3bil a year na haingizi chochote ni hvi hakuna CAPITALIST duniani anayefanya biashara ya hasara.
Utopolo mtapata shida sana.
Kudadeki
 
Wewe ni moja kati ya wale mnaofanya serikali icheleweshe bangi kuruhusiwa!

Eti Voda B Azam B Sportpesa B yani unaandika kama umeshikwa na tumbo la kuhara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…