Huyu mrembo Diamond hawezi kumuacha hivihivi

Hashpower7113

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
1,353
Reaction score
2,142
Wakuu, heshima kwenu! Katika pitapita yangu kwenye mitandao ya kijamii, nimekutana na huyu mrembo, jina lake anaitwa Precious Mary akiwa amefanya cover ya wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz akiwa na Omarion, African Beauty.

Nikiri kwamba sijawahi kusikia habari zake mahali popote lakini baada ya kuiona cover hiyo, nimeshawishika kuamini kwamba endapo Simba naye ataiona, hawezi kumuacha mwanadada huyu hivihivi!

Ukiachilia mbali sauti yenye uwezo wa 'kumtoa nyoka pangoni', huyu msichana ni mrembo wa haja na anajua pozi za kucheza na kamera. Enyi wafuasi wa Simba, hebu muonesheni bosi wenu hii cover ili afanye mambo kwa huyu mrembo.

Ni matumaini yangu na natoa RAI kwamba mambo atakayoyafanya Simba, yatahusiana na kumnyanyua mrembo huyu kisanii ili kesho na keshokutwa naye aje kuwa icon mkubwa katika muziki huu wa Bongo Fleva na si vinginevyo.
Wasalaam!

 
Anamidomo mizuri ya kulamba koni,ila kuna wenzie wameimba zaidi yake hyo ngoma
 
Na mondi huwa anayafanyia kazi maoni ya jf atamchukua mkuu kumbuka lavalava
Kweli mkuu, ndiyo maana nikalileta hapa maana najua hapa watu wa kila kada wanafuatilia kinachoendelea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…