Huyu mrembo Diamond hawezi kumuacha hivihivi

Huyu mrembo Diamond hawezi kumuacha hivihivi

Haha naona siku hizi watu hatuna mpango na sura wala sauti, wowowoww ndo mpango mzma na nafikiri ndo sababu ambayo inatufanya wengi tumetamani kuona video akiwa kasimama.
Mkuu kumbe na wewe umeunga mkono hoja ya mlengwa kusimama? 😀😀
 
Hisia zangu zinanituma wewe ndio huyo dada, unajipigia promo ili Diamond akugonge. Ila uzuri Mond sio mchoyo[emoji16]
Mkuu umenifanyia shambulio la aibu, itabidi ukapimwe mkojo central, hakuna namna
 
Kichwa chake kina misuli kama yule mdogo wake Alikiba.

Kaimba vizuri.
Ana sura pana sana na hizo rasta alizosuka ndo zinamfanya anaonekana ana bonge la kichwa kama....anyway beauty is in the eyez of an individual....
 
Mbona anaimba nje ya key...

Embu msikieni huyu.
 
Wakuu, heshima kwenu! Katika pitapita yangu kwenye mitandao ya kijamii, nimekutana na huyu mrembo, jina lake anaitwa Precious Mary akiwa amefanya cover ya wimbo wa msanii wa muziki wa kizazi kipya, Diamond Platnumz akiwa na Omarion, African Beauty.

Nikiri kwamba sijawahi kusikia habari zake mahali popote lakini baada ya kuiona cover hiyo, nimeshawishika kuamini kwamba endapo Simba naye ataiona, hawezi kumuacha mwanadada huyu hivihivi!

Ukiachilia mbali sauti yenye uwezo wa 'kumtoa nyoka pangoni', huyu msichana ni mrembo wa haja na anajua pozi za kucheza na kamera. Enyi wafuasi wa Simba, hebu muonesheni bosi wenu hii cover ili afanye mambo kwa huyu mrembo.

Ni matumaini yangu na natoa RAI kwamba mambo atakayoyafanya Simba, yatahusiana na kumnyanyua mrembo huyu kisanii ili kesho na keshokutwa naye aje kuwa icon mkubwa katika muziki huu wa Bongo Fleva na si vinginevyo.
Wasalaam!


Domo kazoea vitu "YUZID" mileage zaidi ya 300,000kms haya mambo anayasikia kwa watu tu.
 
Back
Top Bottom