Huyu mtu /Hii kampuni inayorudishia rangi kwenye barabara (zebra) wanapoteza muda na hela

Wapigwe tuu

Senior Member
Joined
Jan 31, 2015
Posts
173
Reaction score
224
Siku hizi 5 nikiwa napita usiku naona wanarudishia rangi kwa zebra! Bagamoyo road na Mwaikibaki Rd. Kama ni msaada waendelee ila kama serikali inawalipa basi naona huu ni ujinga na viongozi pia ni hivyo hivyo!

Rangi sijui ya nyumba ile wanapaka. Wakiweka rangi usiku asubuhi ukipita imeisha. Whats the point? Usiku wanafunga njia kuleta shida na ajali. Hawana vitendea kazi na hata weledi ukiwaona tu unajua something is very wrong!

Mfano Kawe round about walipaka usiku now mkaangalie na pia barabara ya bagamoyo kituo cha Mbuyuni.

Walichopaka kishatoka au kufutika ndani ya masaa.
 
Hamna picha ya kuthibitisha maelezo yako?! Au tuielekeze Jf kituo cha polisi maana unalenga kuikashifu tanroad kama wale 29&40 walioidhihaki serikali.
 
Mkuu kuwa na huruma, Kuna wenzako wameaga wake zao kuwa wanaelekea kazini.
 
Ndiyo Bongo hiyo bwana. Kila kitu ni magumashi. Hiyo rangi inaonekana wanachakachua ili kupiga faida kubwa. Watu wakitumbulia mnasema rais mbaya. Tanzania inahitaji wa-Magufuli kama milioni moja ili ku-deal na uzembe kama huu. Hapo utakuta kama ni tenda walipewa hao hao waliotangaza tenda, wakaenda kuchukua machinga na rangi za kopo za kuweka alama. Mbona utaalam wa kuchora hizi alama umekuwa sana sisi tunashindwa nini kununua mashine ambazo ni rahisi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…