Huyu muigizaji wa filamu anaejiita mutrah1 huko instagram, ni sukari ya warembo aisee

Huyu muigizaji wa filamu anaejiita mutrah1 huko instagram, ni sukari ya warembo aisee

AlphaMale

JF-Expert Member
Joined
Oct 26, 2019
Posts
613
Reaction score
1,416
Professionally, huyu jamaa ni muigizaji maarufu kidogo, tena ni mtanzania anaeongea kiswahili, na ni mwanaume aliezaliwa na kukulia Dar, aliigiza kwenye ile movie inayoitwa huba, half kimuonekano jamaa hana hela, wala ha-post maisha ya kifahari kwenye Instagram page yake. Anaji-post yeye akiwa kifua wazi..

KINACHONIUMA:
Huyu jamaa kwa muonekano ni shombe shombe, aisee aki-post picha Instagram, kwenye hizo comments hao wadada jinsi wanavyojipendekeza kwake, dooh sijawahi ona, wadada hawajipendekezi kwenye instagram comments section ya rayvanny, mbosso, na mastaa wengine wa kiume hapa bongo, kama wanavyojipendekeza kwa huyu mutrah1, kwenye hio comments section sasa utaona mdada anasema anampenda mutrah, mdada mwingine atasema mutrah jibu comment yangu, wadada wengine wanatoa comments za kumtongoza mutrah kimapenzi... wakati kwenye comment section ya mastaa wengine wa kiume, utakuta comments za page za matangazo tu na emoji za fans wa kiume.. tena kila post ya mutrah1 huko insta ina-commentiwa na wadada tofauti sio chini ya wadada 8 au wadada 9 kwa kila post

Sie wengine tangu tumeanza kutumia Instagram, na Facebook hatujawahi pata hata comments 2 kutoka kwa wadada, nahisi huyu jamaa DM yake imejaa SMS za mapenzi kutoka kwa wadada
 
Huyu ni Jasiri kwa wanaofatilia pete, tatizo ni light skin ila yupo vizurii
 
Huyu ni Jasiri kwa wanaofatilia pete, tatizo ni light skin ila yupo vizurii
Amejitahidi sana kuwakilisha TZ katika tamthilia ile mzuri toka mwambao wa Kenya. Ni tamthilia mzuri, tatizo bado hajawa popular sana hapa home TZ na Wanaongalia Tv za kulipia wamegawanyika Azam, Startimes na Dstv hivyo wanaomjua ni wale wanaoangalia.

Ana Talent na muonekano mzuri ndio maana amekuwa kivutio kwa wanawake. (Hata wifey hupenda kuangalia, navutiwa na Nuru, sijui yeye! ) Arudi home afanye Movies na Tamthilia kadhaa.
 
Back
Top Bottom