Sigara Kali
JF-Expert Member
- May 28, 2017
- 3,623
- 8,442
DUUH!! HUYU MWAJIRI NI SHIDAAA!!
Hebu soma hii
[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]
Baada ya miaka minne ya kuajiriwa bila hata kuongezwa mshahara au hata marupurupu, Bwana John aliamuankwenda kwa bosi wake kulalamika.
Jibu alilolipata kwa bosi wake ni kwamba hakupewa nyongeza wala marupurupu kwa sababu HAKUSTAHILI.
Akauliza kwa nini?
Akaambiwa katika miaka minne uliyofanya hapa, hujafikisha mwaka hata mmoja.
Akasimama na kuanza kufoka, akaambiwa kaa chini, na majibizano yakawa hivi;
Bosi; Mwaka una siku ngapi?
John: 365 au 366.
Bosi: Huwa unakuja kazini wikiendi?
John: Hapana
Bosi: Hebu piga hesabu mwaka una jumamosi na jumapili ngapi kisha zitoe katika 366
John: Jumamosi 52 na Jumapili 52 jumla unapata siku 104. Ukitoa katika siku 366 unabaki na siku 262.
Bosi: Siku ina masaa 24, wewe umafanya kazi masaa mangapi?
John: Masaa nane kwa siku
Bosi: Sasa nipigie hesabu masaa nane katika masaa 24. Nane kwa 24 inaingia mara ngapi?
John: Inaingia mara tatu mkuu
Bosi: Sasa ukizigawa zile siku 262 kwa masaa uliyofanya kazi yaani uigawe kwa tatu kulingana na masaa uliyofanya kazi unapata siku ngapi zilizokamilika?
John: 87
Bosi; Kwa mujibu wa saa ulizofanya kazi kwangu, ni sawa na siku 87, tuendelee na mahesabu?
John: Tuendelee
Bosi: Unakumbuka uliumwa wiki mbili nikakupa likizo? Na ulishachukua likizo yako ya kawaida siku 28 na ukaenda msibani wiki moja hebu piga hesabu vizuri.
John: 14 + 28 + 7 = 49
Bosi; Toa katika siku 87
John: 42
Bosi: Toa sikukuu za Idd, Maulid, Uhuru, Mapinduzi, Pasaka, Krismas, Nyerere Day, Mwaka mpya, Mei Mosi, Sabasaba, Nanenane na ile wiki iliyonyesha mvua kuuubwa nikawaruhusu mpumzike.
John: Bosi naomba nikaendelee na kazi
Bosi: Malalamiko vipi?
[emoji2534] [emoji2534] [emoji2534] [emoji2534] [emoji2534]