Huyu mwalimu wa Rais Samia alisomea combination gani?

Huyu mwalimu wa Rais Samia alisomea combination gani?

Nepotism inapamba Moto watu wake walewale sie wakulima tutasota na majembe yetu ya mkono na kudhulumiwa haki zetu
 
Bi Khadija alimfundisha Mh. Rais Hesabu na Kiingereza alipokuwa form two/three.

Je, huyu Mwl Khadija alisomea combination gani mpaka akaja kufundisha Hesabu na Kiingereza?

View attachment 2232770
Chukulia scenerio hii kwa urahisi zaidi. Mimi hapa niliwahi kuongoza mtihani wa Hesabu wa Mock FIV na mtihani wa NECTA FIV nilikuwa na "A" ya Kiingereza. Chukulia sasa ningekuwa mwalimu wa Sekondari nafundisha hesabu; je kwa muda wangu wa ziada, nitashindwa kumfundisha mtoto wa Sekondari Kiingereza?
 
Inawezekana hata kwa mtu aliyesoma HGL kufundisha hesabu kama kuna uhaba wa mwalimu wa hesabu.

Ninao ushahidi mnamo mwaka 2012 halmashauri ya manispaa ya shinyanga(jina la shule kapuni) kuna mwalimu alikuwa anafundisha civics form four na basic mathematics form one.Hivi vitu ukiwa unaambiwa tu unaweza usiamini kwa kuwa pengine umepita shule zisizokuwa na changamoto.Hiki ni kitu nilichoshuhudia kwa macho yangu.

Mungu amlaze mahali pema peponi mwalimu huyu,maana alishatangulia mbele ya haki.
Walimu wengi tu wa arts wanafundisha mathematics kwa upande wa O-level.
Shida ya wengi wamekariri et waliosoma art Basi walifeli hesabu ,sio kweli Kuna walimu kibao tu O-level walikua hawakamatiki kwenye hesabu bahat mbaya wakachaguliwa hgl ,hkl ,hge ila kwa upande wa hesabu ni wa Moto balaa pengine kuzid hao waliosoma hesab huko advance .
Kwa upande wa olevel ni wengi mno walimu wa hivyo hasa shule zenye changamoto za walimu wa hesabu .

Ila kwa upande wa advanced level Hilo halipo maana ule mziki lazima uingie darasan haswa ila olevel kawaida Sana .
 
Huyu bi Khadija kaapishwa kushika wadhifa gani?
Hongera bi. Khadija
 
Chukulia scenerio hii kwa urahisi zaidi. Mimi hapa niliwahi kuongoza mtihani wa Hesabu wa Mock FIV na mtihani wa NECTA FIV nilikuwa na "A" ya Kiingereza. Chukulia sasa ningekuwa mwalimu wa Sekondari nafundisha hesabu; je kwa muda wangu wa ziada, nitashindwa kumfundisha mtoto wa Sekondari Kiingereza?

Huo ufafanuzi wako ni bure tu hapa, bibie hajasema hayo….. suala sio kuweza wala kushindwa kufundisha.
 
Huo ufafanuzi wako ni bure tu hapa, bibie hajasema hayo….. suala sio kuweza wala kushindwa kufundisha.
Sijasema kuwa kasema hivyo. Nimesema chukulia scenerio........ Kiswahili kigumu
 
Kichwa chako ni sanduku la kuhifadhia meno tu.
Pinga ufafanuzi kwa hoja zenye mantiki

Nimekutolea mfano mimi ninamfahamu mwalimu wangu wa shule ya msingi alikuwa anafundisha kiingereza na hisabati

Baadaye alijiendeleza kimasomo na sasa anafundisha sekondari, ni mwalimu mzuri tu wa kiiingereza na hisabati
 
Ukiachia mbali hoja ya combination, na kama alimfundisha sekondari ya kawaida, bado kuna maswali mengi.
Ikiwa rais ana 60+yrs, huyo mwalimu wake ana umri gani?

Je, ni kulipa fadhila au kuna tija kwa taifa?
Halafu collegemate wake anaonekana mzee kuliko mwalimu wake.
Duh nchi hii, kazi kweli!
Kweli kabisa hii inafikirisha kidogo na imekaa mkao wa kulipa fadhila na hapo kwenye umri ndio shida kidogo
 
Alisomea combination sound, combinenga, mwalimu mkuu man water na kilanja alikuwa 20%!
 
Huyu mama yuko vizuri kwa kulipa fadhila; redio mbao zinasema kuwa mama yake na yule mwandishi wa habari bibisi alikuwa akimsaidia kwenye mitihani
 
Kwani! Mbona mi nimesoma hgl lakini Nina A ya hesabu o level na Kuna hamaa nimesoma naye ana C ya hesbu lakini amesoma pcm. Does it mean tayari amenizidi hesabu kwa sababu ya choice yangu? Au kila anayesoma art kwa uelewa wako finyu unaamini kafeli sayansi!! Refer to Tundu lisu aliamua kusoma hgl lakini ana A zote yaani physics, chemistry, biology nk
Bila shaka PCM. Then akajiongeza/akaombwa kufundisha English kwa kuwa labda hakukuwa na waalimu

Aliyesoma HGL hawezi kusogea kufundisha Mathematics
 
Kwa walimu wa sampuli hiyo,inaakisi matokeo ya upande wa pili wa muungano.

Hiyo ni "Goli kona" hakuna tahasusi hapo.
Umetumia msamiati mgumu: "Goli kona", "tahasusi" - ni kama maneno yatumikayo upande wa pili wa muungano!

"Goli kona", yaani kona iliyokwenda moja kwa moja golini?, nashindwa kuunganisha na habari iliyopo hapa.

Ningependa kutumia msamiati huu nikijua maana yake.
 
Back
Top Bottom